
Mstoa Marcus Aurelius amewahi kusema anashangazwa na tabia ya binadamu, huwa tunajipenda wenyewe zaidi ya tunavyowapenda wengine, lakini tunayathamini maoni ya wengine kuliko yetu wenyewe.
Hili ni tatizo linaloanzia kwenye kutokujiamini. Unapokuwa hujiamini wewe mwenyewe, kile unachofanya na kule unakotaka kufika, unashindwa pia kuyaamini maoni yako mwenyewe. Unaona maoni ya wengine ndiyo sahihi zaidi, unayafuata hayo na kinachotokea ni unaanguka vibaya.
Kipaumbele cha kwanza kwako ni ukweli, cha pili maoni yako na cha tatu ndiyo maoni ya wengine. Usiende kinyume na mtiririko huo.
Ukurasa wa kusoma ni yaweke maoni sehemu sahihi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/21/2425
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma