Rafiki yangu mpendwa,
Kama ambavyo nimekuwa nakushirikisha mara kwa mara, falsafa yangu kuu kwenye huduma ninazotoa ni hii; naweza kupata chochote ninachotaka kama nitawasaidia wengi zaidi kupata kile ninachotaka.

Ili kuweza kuiishi falsafa hiyo kikamilifu, mara kwa mara nimekuwa nakuuliza nini hasa unachotaka ili niweze kukusaidia kukipata.

Kwenye moja ya barua za kila wiki ninazotuma kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, niliuliza hilo kwa maswali matano ya msingi kabisa na kuweza kupata majibu mengi mazuri.

Kati ya majibu hayo mengi, yapo 12 ambayo yamejirudia rudia sana na hayo yamenipa picha ya vitu gani ambavyo watu wanahitaji sana.

Baada ya kuyapitia majibu hayo kwa kina, nimejitoa kuwapatia watu mambo haya 12 muhimu yatakayowawezesha kufika kwenye mafanikio makubwa.

Kwenye makala hii nimeshirikisha mambo hayo 12 na hatua ninazokwenda kuchukua ili uweze kunufaika zaidi.

Kama nilivyoeleza, kwenye barua niliyotuma, kulikuwa na maswali matano ya msingi.
Hapa nitashirikisha maswali hayo, kutoa ufafanuzi mfupi na kisha kushirikisha majibu yaliyojirudia sana na hatua ninazokwenda kuchukua.

Swalia kwanza; Kwa nini upo kwenye KISIMA CHA MAARIFA?

Swali hili lililenga kujua kwa nini mtu yupo kwenye KISIMA CHA MAARIFA, maana watu huwa hawafanyi mambo bila ya sababu.

Kuna majibu matatu ambayo yamejirudia rudia sana;
1. Kupata maarifa sahihi ya mafanikio.
2. Kupata hamasa ya kufanya makubwa.
3. Kuzungukwa na kushirikiana na watu sahihi wenye kiu ya mafanikio.

Ninayoenda kufanya.
1. Nitaendelea kushirikisha maarifa bora kabisa ya mafanikio ambayo hayapatikani mahali pengine popote.
2. Nitaendelea kutoa hamasa isiyopoa wala kulala ili kila mmoja apate nguvu ya kuendelea na mapambano ya mafanikio kila siku.
3. Nitaendelea kujenga ushirikiano wa karibu baina ya wanachama ili kila mmoja aweze kunufaika na kunufaisha wengine.

Swali la pili, Kipi kikubwa kimebadilika kwenye maisha yako?

Swali hili lililenga kujua jinsi gani KISIMA CHA MAARIFA kimekuwa na mchango wa tofauti kwenye maisha ya mtu. Yaani kitu gani mtu akiangalia kwenye maisha yake anasema hiki ni sababu ya KISIMA CHA MAARIFA.

Hapa pia palikuwa na majibu mengi, lakini matatu makubwa ni haya;
4. Fedha; kuondoka kwenye madeni, kuweka akiba na kuwekeza yamekuwa ni matokeo ambayo wengi wamepata kwenye eneo la fedha.
5. Biashara; wengi wameweza kuanzisha biashara na kuzikuza. Wengine wameweza kuachana kabisa na ajira na kufanya biashara zinazowapa uhuru zaidi.
6. Mtazamo; watu wamepata mabadiliko makubwa ya kimtazamo, kuanzia kwao wenyewe na kwa dunia inayowazunguka.

Ninayoenda kufanya.
4. Nitaendelea kutoa elimu ya fedha na usimamizi wa karibu ili kuhakikisha kila mwanakisima ameondoka kwenye madeni, ana akiba ya kumpa utulivu kwenye maisha na ana uwekezaji wa kumpa uhuru wa kifedha.
5. Nakwenda kuweka juhudi kubwa kuhakikisha kila manakisima anakuwa na biashara inayojiendesha yenyewe kwa mfumo ili kumpa uhuru kamili wa maisha.
6. Nitaendelea kuweka juhudi kuhakikisha kila mwanakisima anajijengea mtazamo sahihi na bora kabisa kwenye mafanikio, maana mtazamo una nguvu sana.

Swali la tatu; Kipi kimoja unataka sana kutoka kwa Kocha?

Swali hili lililenga kujua kitu gani ambacho mtu angependa kupata kwa kocha ili aweze kufikia mafanikio makubwa.

Katika majibu mengi yaliyotolewa, haya matatu yamejirudia zaidi.
7. Usimamizi; watu wanataka kusimamiwa kwa karibu zaidi katika malengo na mipango waliyojiwekea ili waweze kufikia.
8. Ukaribu; watu wanataka kupata ukaribu zaidi na Kocha ili waendelee kupata hamasa na msukumo wa kupambana kufanikiwa.
9. Uvumilivu; wengi wameomba kuvumiliwa pale wanapoteleza kwenye safari ya mafanikio.

Ninayoenda kufanya.
7. Nitakuwa na usimamizi na ufuatiliaji wa karibu zaidi kwa kila mwanakisima ili aweze kutimiza malengo na mipango yako.
8. Nitatoa muda zaidi kwa wanakisima ili kujenga ukaribu zaidi na kila mwanachama na apate msukumo zaidi wa mafanikio.
9. Nitakuwa na uvumilivu kwa wale waliojitoa kweli kufanikiwa hata kama wanaanguka au kupitia magumu mbalimbali, maana najua safari ya mafanikio siyo rahisi. Muhimu ni mtu awe na nia ya kweli na ajitoe kweli kufanikiwa.

Swali la nne; Nani unaweza kumzawadia uanachama wa KISIMA CHA MAARIFA?

Kama kitu kina manufaa kwako, utapenda kiwanufaishe na wengine wa karibu yako. Kama wanavyosema, kizuri kula na nduguyo.
Swali hili lililenga kujua ni mtu gani unaweza kumpa zawadi ya uanachama wa KISIMA.

Kulikuwa na majibu mawili yaliyojirudia sana kwenye swali hili;
10. Mwenza; mke au mume.
11. Rafiki wa karibu.

Ninachokwenda kufanya.
Kwa kipindi cha nyuma ukuaji wa KISIMA CHA MAARIFA ulitegemea zaidi wale niliowashawishi kupitia kazi zangu.
Kwa sasa ukuaji utakwenda kutegemea zaidi wanachama waliopo.
Hivyo nitaweka nguvu kubwa kwa kila mwanachama, ili apate matokeo makubwa sana.
Na nilishahakikisha kweli KISIMA kimekuwa na manufaa makubwa kwa mtu, nitampa nafasi ya kumpa mtu wake wa karibu zawadi ya uanachama.

Hili litafanya kazi hivi;
Kwa kuwa maisha yako yamebadilika sana, watu wako wa karibu watataka kujua nini siri yako.
Utawaeleza siri ni KISIMA CHA MAARIFA.
Utachagua katika watu hao wa karibu yupi unayemuona anafaa sana kuwa kwenye KISIMA na ataweza kuiishi hii falsafa.
Tutampa zawadi ya uanachama, ambapo atajiunga bila kulipa ada kwa kipindi fulani cha mwanzo.
Katika kipindi hicho cha mwanzo aliyemleta atakuwa ndiye menta wake na atapaswa kuiishi falsafa ya KISIMA ili maisha yake yawe bora pia.
Na baadaye ataanza kulipa ada, baada ya kuona kweli KISIMA CHA MAARIFA kinamfaa.
Hilo ndiyo tunakwenda kufanyia kazi.

Swali la tano; Je umejitoa kweli kuishi falsafa ya KISIMA CHA MAARIFA?

Swali hili lililenga kujua kama mtu amejitoa kweli kuiishi falsafa hii ya KISIMA kwa hiari yake mwenyewe na siyo kwa kulazimishwa.

Na jibu la wote lilikuwa ni;
12. NDIYO.

Hatua kuu ninayokwenda kuchukua kwenye hili ni kuchuja na kupata wale waliojitoa kweli.
Maana kuna wengi wanakuwa wanayatamani mafanikio ila hawajajitoa kweli kweli kuhakikisha wanayapata.
Wanaruhusu kila aina ya sababu na visingizio kuwa kikwazo kwenye safari yao.
Ninachoamini ni huwezi kumbadilisha au kumlazimisha mtu kuwa namna fulani.
Hilo linapaswa kutoka ndani ya mtu mwenyewe.

Rafiki yangu mpendwa, hayo ndiyo mambo 12 uliyoyaomba na mimi nimejitoa kuhakikisha unayapata ili uweze kufika kwenye mafanikio makubwa.

Ombi langu kuu kwako ni hili; usiniangushe. Nimekuamini sana kwenye hii safari ya mafanikio, nimejitoa kukupa kila unachohitaji ili ufanikiwe, ni wewe tu utumie fursa hii vizuri.

Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA tumia nafasi hii kujiunga ili unufaike na haya pamoja na mengine mengi. Tuwasiliane sasa kwa namba 0717 396 253 kupata nafasi hiyo.

Nikukumbushe pia kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, siku zimebaki chache kujipatia nafasi yako ya kushiriki semina hii.
Hiyo ndiyo nafasi pekee ya kukutana pamoja, kujifunza, kuhamasika na kutengeneza mtandao wa watu sahihi.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz