Rafiki yangu mpendwa,
Najua nikisema biashara unajua kabisa namaanisha nini.
Maana kwenye makala zilizopita nimekuonyesha tofauti ya kumiliki biashara na kumilikiwa na biashara.

Na pia nikakuonyesha tofauti ya kujiajiri ambao ni mfumo mwingine wa utumwa na kumiliki biashara ambayo ndiyo njia pekee ya kufika kwenye uhuru kamili.

Katika yote hayo nimekuwa nazungumzia sana mfumo wa biashara kujiendesha yenyewe.
Wengi wanaposikia hilo la mfumo wanachoka kabisa na kuona ni kitu kikubwa na kinachoweza kufanywa na watu wenye biashara kubwa tu.

Wengi huona wanahitaji kupata wataalamu wa biashara na waliobobea kabisa (MBA) ndiyo waweze kutengeneza mfumo wa kuendesha biashara.

Wengine huona hawawezi kutengeneza mfumo kwa sababu bado hawajawa na wafanyakazi. Hivyo wanaona wasubiri mpaka watakapoanza kuajiri ndiyo wafanye hivyo.

Lakini hayo siyo kweli, unaweza kutengeneza mfumo wa biashara yako wewe mwenyewe na hata kama uko peke yako na biashara ni ndogo.

Kwa hakika ni unapaswa kutengeneza mfumo wa kuiendesha biashara yako haraka iwezekanavyo la sivyo utajitengenezea gereza lako mwenyewe.

Wakati mzuri wa kujenga mfumo kwenye biashara yako ilikuwa wakati unaianza. Wakati mwingine mzuri ni sasa.
Hapa unakwenda kujifunza hatua tano rahisi za kutengeneza mfumo wa biashara yako na nitakushirikisha njia ya kujifunza hatua hizo kwa vitendo kabisa.

Hatua ya kwanza; orodhesha kila kinachofanyika kwenye biashara.

Kila kitu ambacho kinafanywa kwenye biashara, kiorodheshe.
Usiache hata kitu kimoja.

Hatua ya pili; gawa vitu hivyo kwenye makundi yanayoendana.

Vitu vinavyohusiana na mauzo vikae pamoja, vinavyohudiana na masoko vikae pamoja.
Kadhalika kwenye manunuzi, fedha na uendeshaji.

Hatua ya tatu; elezea kila kitu kinavyofanyika na kwa nini.

Hapa unapaswa kuelezea kila kinachofanyika kwenye biashara jinsi kinavyofanyika na kwa nini kinafanyika hivyo.
Hapa unaeleza mchakato mzima wa kufanya maamuzi kwenye kila eneo la biashara yako.

Hatua ya nne; andika mchakato wa ufanyaji.

Kwa kila maelezo uliyoandaa kwenye kile kinachofanyika kwenye biashara, andika kuwa mchakato ambao utafuatwa na yeyote aliye kwenye biashara.
Unauandika kuwa mwongozo wa kufanya maamuzi kwenye eneo husika ambao utatumiwa na anayefanyia kazi eneo hilo.

Hatua ya tano; hongera tayari una mfumo.

Sasa kusanya miongozo yote ya kila kinachofanyika kwenye biashara na huo ndiyo mfumo wa kuiendesha biashara yako.
Kila kitu kwenye biashara kinapaswa kufanyika kwa kutumia mwongozo huo.
Kila aliye kwenye biashara anapaswa kuusoma, kuuelewa na kuutumia mwongozo huo.

Lakini pia mwongozo huo siyo msaafu, kadiri unavyofanyiwa kazi na kugundua kuna mapungufu au maeneo ambayo hayakuelezewa vizuri, unapaswa kuendelea kuboreshwa kadiri unavyokwenda.

Rafiki, umejionea hapo mwenyewe, huhitaji elimu kubwa ndiyo uweze kutengeneza mfumo wa biashara.
Unachohitaji ni kukaa chini na kuandika yale ambayo tayari umeshayafanya na kuyageuza kuwa mwongozo.
Chukua hatua hizo tano sasa na utakuja kushukuru mno baadaye.

Kama nilivyokueleza hapo juu, kuna fursa ya kuweza kujifunza hatua hizo tano na kuzifanya kwa vitendo.

Najua wengi mnaosoma hapa mtasema nitafanya, lakini hamtafanya. Mtaendelea kuendesha biashara zenu kwa mazoea na hilo litakuwa kikwazo kwa ukuaji.

Ipo nafasi ya wewe kuchukua hatua hizi na kukamilisha zoezi hilo ndani ya siku moja, ukarudi kwenye biashara yako ukiwa na mwongozo wa kwenda kufanyia kazi.

Hilo unalipata kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo itafanyika jijini Dodoma tarehe 16 na 17 Oktoba 2021.

Hiyo siku ya tarehe 17 tumeitenga kwa ajili ya shughuli moja tu, kutengeneza mfumo wa biashara.
Hivyo kila mshiriki siku hiyo atachukua hatua zote za kutengeneza mfumo na mpaka anaondoka anakuwa na kitu anachokwenda kufanyia kazi.

Je umeshapata nafasi ya kushiriki semina hiyo? Kama jibu ni bado unajichelewesha, wasiliana sasa na 0717 396 253 kupata nafasi yako.

Na kama umeshajiwekea nafasi ila hujakamilisha malipo yako ya ada, kamilisha mapema ili usikose tukio hili muhimu sana kwako.

Huenda ndiyo unapata taarifa hizi za semina kwa mara ya kwanza, bado hujachelewa, maelezo kamili yako hapo chini.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz