2471; Watu wanaamini msimamo.
Kuahidi kila mtu anaweza na wengi wanafanya hivyo.
Kujaribu kufanya kila mtu anaweza na wengi huanza na kuacha.
Wanachohitaji watu ili wakuamini ni msimamo wako kwenye kile ulichoahidi.
Kama una biashara ambayo umeahidi kitu fulani, lakini mwanzoni huna wateja wengi, ni rahisi kutokutimiza ahadi hiyo, ukijiambia mpaka uwe na wateja wengi ndiyo utatimiza.
Ambacho hujui ni kwamba, wateja wapo, ila wanasubiri wakuone una msimamo gani kwenye kutekeleza ulichoahidi ndiyo waje kwako.
Hivyo wajibu wako mkubwa ni kusimamia kila ulichoahidi, bila ya kujali kitu kingine chochote.
Maana watu watakuamini kupitia msimamo wako, kwa yale unayofanya bila kuacha.
Hatua ya kuchukua;
Ni maeneo gani ya maisha yako, kazi yako au biashara yako ambayo umewahi kuahidi mambo mbalimbali ila hukuyatimiza kutokana na kutokupata mrejesho mzuri mwanzoni?
Rudi kwenye yale muhimu na yatekeleze kwa msimamo bila ya kuacha.
Utaona jinsi mapokeo yatakuwa mazuri baada ya kufanya kwa muda.
Maana wale unaowalenga, watakuamini zaidi kupitia msimamo wako kwenye kufanya na siyo maneno matupu.
Tafakari;
Kuahidi ni rahisi na kila mtu anafanya hivyo. Kufanya kwa msimamo ni kugumu na wachache sana ndiyo wanaofanya hivyo. Mambo magumu ndiyo yanayoleta mafanikio makubwa kwa kuwa yanafanywa na wachache. Kuwa mmoja kati ya hao wachache.
Kocha.
Asante sana kocha.
LikeLike