Rafiki yangu mpendwa,
Mafanikio ni dhana pana mno.
Hakuna maana moja ya mafanikio inayoweza kuwafaa watu wote.

Maana ya mafanikio inatofautiana kwa kila mtu.
Kwa sababu watu wanatofautiana, kuanzia uwezo, kusudi na hata ndoto, mafanikio hayawezi kufanana kwa wote.

Kwa maana rahisi kabisa, mafanikio ni pale mtu anapoweza kutumia uwezo wake wa ndani, kuishi kusudi lake na kufikia ndoto kubwa alizonazo.

Kwa maana hiyo, mafanikio yanaanzia ndani ya mtu na siyo nje. Hivyo mafanikio ya kweli kwa mtu ni yale yanayoanzia ndani yake.

Changamoto kubwa kwenye safari ya mafanikio ni watu kuhangaika na vitu visivyokuwa na tija kwao.
Watu wanakimbizana na mafanikio ambayo hayatoki ndani yao.

Watu wanakuwa wamehadaiwa na jamii ambayo imekuwa inawadanganya ukifanya hivi au kuwa vile ndiyo utakuwa umefanikiwa.
Wanapambana kweli kama walivyoambiwa, wanavifikia viwango hivyo walivyowekewa na jamii.

Lakini bado ndani yao wanakuwa na utupu mkubwa. Licha ya kuonekana wamefanikiwa kwa viwango vya nje, ndani wanakuwa hawana furaha. Hiyo ni kwa sababu mafanikio hayo hayajaanzia ndani yao.

Jamii ina ushawishi mkubwa sana wa kukuteka na kukuweka kwenye njia ya mafanikio ambayo haina maana kwako.
Jamii itakushindanisha na wengine na kukuonyesha kama hujawa kama wao basi una tatizo.

Usipokuwa na mwongozo sahihi unaoufuata kwenye maisha yako, utahangaika na mambo mengi lakini hutapata mafanikio ya kweli.
Utapambana kufikia mafanikio ambayo jamii imekuambia, lakini ndani yako hutapata ridhiko.
Na japo watu wanaweza kuona kwa nje umefanikiwa, ndani yako utajiona ukiwa mtupu na hujafanikiwa.

Ninayo furaha kukufahamisha kwamba kitabu kipya cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO kipo tayari kwa ajili yako.
Hiki ni kitabu kitakachokufundisha dhana moja kubwa na muhimu sana kwenye safari yako ya mafanikio.
Dhana hiyo inaitwa; KIMBIA MBIO ZAKO MWENYEWE.

Mafanikio kwenye maisha ni mbio ambazo hazifanani.
Kila mtu ana mbio zake.
Unapoacha mbio zako na kwenda kushiriki mbio za wengine, unakuwa umechagua wewe mwenyewe kujipoteza.

Upo usemi kwamba tatizo la kushiriki mbio za panya, hata ukishinda unabaki kuwa panya.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio. Kuhangaika na mafanikio ambayo hayajaanzia ndani yako, hata ukishinda bado unakuwa hujafanikiwa.
Mafanikio ya kweli ni yale yanayoanzia ndani yako mwenyewe.

Kwenye kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO utapata nafasi ya kujitafakari wewe mwenyewe kwa kina, kujitambua, kujua kusudi la maisha yako na ndoto kubwa ulizonazo na kisha kupambana na hayo.

Wakati wengine wanahangaika na mafanikio yasiyokuwa na maana kwao, wewe unakuwa unayajua mafanikio yenye maana kwako na ndiyo unapambana nayo.

Usikubali kuendelea kupotezwa na jamii ili uendelee kubaki kwenye mbio za panya. Maana hata ukishinda mbio hizo, unabaki kuwa panya.
Jipatie nakala yako ya kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO leo ili uanze kukimbia mbio zako mwenyewe na mafanikio utakayoyapata yawe na maana kwako.

Kitabu ni hardcopy na unaweza kukipata ukiwa popote ndani ya Afrika Mashariki.
Wasiliana na namba 0752 977 170 kupata kitabu chako leo hii ili uweze kupambana na mafanikio yenye maana kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana.
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.