2485; Haiwezekani mpaka itakapofanyika.
Kila kitu ambacho hakijawahi kufanyika, hakiwezekani.
Hakiwezekani siyo kwa sababu hakiwezekani kweli, ila kwa sababu watu hawajawahi kuona kikifanyika.
Hivyo kama kuna kitu unataka kufanya na wengine wanakuambia hakiwezekani, jua siyo kwamba hakiwezekani, ila watu hao hawajawaji kuona kitu hicho kikifanyika.
Ni wajibu wako kukifanya ili kupata unachotaka na pia kuwaonyesha wengine inawezekana.
Watu wa kawaida huwa wanaendana na dunia jinsi ilivyo. Watu wasio wa kawaida huwa wanaifanya dunia iendane nao.
Hivyo maendeleo ya dunia yamekuwa yanaletwa na watu wasio wa kawaida.
Je wewe umechagua upande upi? Wa kawaida au wasio wa kawaida? Chagua upande sahihi na uuishi.
Hatua ya kuchukua;
Ni vitu gani umekuwa unataka sana kufanya ila watu wamekuwa wanakuambia haviwezekani? Kuanzia sasa amini vinawezekana na vifanyie kazi mpaka viwezekane kweli.
Tafakari;
Utakapoamini kisichowezekana kinawezekana, wengi watadhani umechanganyikiwa na watakupinga na kukukatisha tamaa. Utakapoendelea kuamini hivyo na kuchukua hatua hatimaye ukafanikiwa watu hao hao watakuita shujaa.
Cha kusikiliza siyo watu wanasemaje, bali nini unachotaka.
Kocha.
Asante Sana kocha. Mafanikio ni haki yangu ya kuzaliwa, kuyapata ni wajibu wangu mkubwa kwenye Maisha. Hakuna cha Kunirudisha nyuma. Kama wengine wanasema Mafanikio hayawezekani mimi nimechagua upande wa kuwezekana na ninafanyia Kazi ili kufikia hilo kwenye maisha yangu.
LikeLike
Safi sana Tumaini.
LikeLike