Rafiki yangu mpendwa,
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wote ambao mmeweza kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo ilifanyika Tarehe 16 na 17 Oktoba jijini Dodoma.

Semina imeweza kufanyika kwa mafanikio makubwa sana na kila mshiriki ametoka akiwa na mkakati wa kwenda kufanyia kazi kwenye mwaka wa mafanikio 2021/2022.

Zilikuwa ni siku 2 za kujifunza, kuhamasika na kutengeneza mtandao sahihi kwa ajili ya mafanikio makubwa kwenye maisha.

Makubwa kabisa ambayo kila  mshiriki wa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ameonendoka nayo ni haya;

1. Kauli mbiu, ahadi na falsafa ya mafanikio ya kuiishi kila siku.

2. Mwongozo kamili wa mwaka wa mafanikio 2021/2022.

3. Mfumo wa kuendesha biashara kwa uhuru mkubwa na kuiwezesha kukua.

4. Kujenga imani, maono na mkakati wa kufika kwenye mafanikio makubwa.

5. Kulijua kusudi la maisha na kuchagua kuliishi kila siku.

6. Kujifunza uzoefu wa biashara kutoka kwa mwenzetu ambaye amekuwa kwenye biashara kwa miaka 10.

7. Kujifunza uzoefu wa kuendesha biashara kwa mfumo kutoka kwa mwenzetu ambaye anaendesha biashara kwa mfumo.

8. Kuzijua changamoto za biashara changa kutoka kwa mwenzetu ambaye anaanza biashara.

9. Kujifunza umuhimu wa mrejesho ba jinsi ya kutoa na kupokea mrejesho ili uweze kupiga hatua zaidi kwa chochote unachofanya.

10. Kupata maarifa sahihi ya kujenga na kuboresha mahusiano ya ndoa.

11. Kufanya mazoezi ya pamoja ambayo ni hitaji muhimu kwa upande wa afya.

12. Kupata nafasi ta kuongea ana kwa ana na Kocha na kuweka mkakati wa kufanyia kazi kwenye mwaka mzima wa mafanikio 2021/2022.

13. Kikubwa zaidi, kila mshiriki ameondoka na ahadi yake ya kiwango cha utajiri anachokwenda kufanyia kazi kwa mwaka wa mafanikio 2021/2022. Ahadi hii kila mmoja ameiandika kwa mkono wake mwenyewe na anakwenda kuiishi kila siku kwa kuchukua hatua sahihi mpaka kuifikia.
Pia kocha anakwenda kumfuatilia kila mmoja kwa karibu katika kuiishi ahadi hiyo.

Kwa wale walioshiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, wito wangu mkubwa kwako ni mmoja, nenda kaweke kwenye matendo yale yote uliyojifunza.
Najua umetoka na maarifa mengi sana.
Najua umetoka ukiwa na hamasa ya juu kabisa.
Lakini vitu hivyo ni rahisi kuyeyuka kama hautachukua hatua mara moja.
Hivyo anza kuchukua hatua sasa kabla kile ulichotoka nacho hakijapoa.
Na mchakamchaka uende hivyo kwa mwaka mzima.
Na wakati wowote unapokuwa na uhitaji wa jambo lolote kutoka kwa kocha, usisite kuwasiliana naye mara moja.

Kama hukupata nafasi ya kushiriki semina, pia sijakusahau.
Wewe kama rafiki yangu ambaye tumekuwa pamoja kwa muda mrefu, nakuthamini sana.
Na wajibu wangu mkubwa ni wewe upate mafanikio makubwa.
Hivyo kwenye muongo huu wa 2020 mpaka 2030 nimechagua kufanya kazi na wale waliojitoa kweli kufanikiwa.
Hivyo kama wewe ni mmoja wa waliojitoa kweli, hakikisha kitu hiki kimoja; unakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.
Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA nitatoa utaratibu kamili wa yale tunayokwenda kufanyia kazi ili kila mmoja aweze kupiga hatua.

Kwa bahati mbaya sana, nafasi za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA zinakwenda kuisha kufika tarehe 31/10/2021. Hivyo kama ulikuwa hujapata nafasi hiyo, chukua hatua sasa.
Baada ya tarehe hiyo, nafasi za wazi za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA hazitakuwepo tena.
Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili tuweze kufanya kazi kwa karibu kabisa na uweze kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Nina uhakika wa kupata chochote ninachotaka kwenye maisha yangu kwa sababu nipo tayari kuwapa wengine kile wanachotaka.
Je wewe ni nini unachotaka? Njoo tufanye kazi pamoja ili uweze kukipata.

Rafiki yako anayekupenda sana.
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.