#SheriaYaLeo (63/366); Jijengee nidhamu ya kazi.
Watu wote walioweza kubobea na kufanya makubwa kwenye maeneo waliyochagua siyo ambao walikuwa wanasukumwa na fedha au umaarufu.
Bali ni wale ambao walikuwa wamejijengea nidhamu kubwa ya kazi kwenye eneo walilochagua.
Walichagua kufanya kazi kwa ustadi wa hali ya juu na kujali sana kuhusu matokeo wanayozalisha.
Walichoangalia ni kufanya kazi ambayo wanajivunia nayo sana.
Walijiwekea viwango vyao wenyewe na kujisukuma kuvifikia, kwa sababu vilikuwa viwango vya juu.
Hicho ndiyo unachopaswa kujijengea kwenye safari yako ya ubobezi, kuwa na nidhamu kubwa ya kazi kwenye kile ambacho umechagua kufanya.
Jiwekee viwango vya juu kabisa kwenye eneo hilo na jisukume kuvifikia.
Usifanye tu kwa sababu unataka kupata fedha au umaarufu.
Bali fanya kwa sababu ndiyo kitu unachojali zaidi kufanya na unakifanya kwa moyo wako wote.
Penda kile unachofanya, jitoe kweli katika kukifanya na kifanye kwa viwango vya juu kabisa ili kuweza kufika na kudumu kwenye ubobezi.
Sheria ya leo; Jijengee nidhamu kubwa ya kazi na mara zote kumbuka kile unachofanya ndiyo kitu pekee na cha muhimu zaidi kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu