#SheriaYaLeo (67/366); Iweke akili kwenye mwendo.
Tulipokuwa watoto, akili zetu hazikuwa zikisimama.
Tulikuwa wazi kwa ajili ya mawazo ba uzoefu mpya.
Tulijifunza kwa kasi kwa sababu dunia ilitushangaza.
Pale tulipokwama, tulitafuta njia ya kibunifu ya kuvuka kinachotukwamisha.
Akili yetu ilikuwa kwenye mwendo muda wote na mara zote tulijawa na shauku na udadisi.
Aristotle alifikiri na kuamini kwamba maisha yapo kwenye mwendo.
Chochote ambacho kipo kwenye mwendo kipo hai.
Na chochote ambacho hakipo kwenye mwendo kimekufa.
Wote tunayaanza maisha tukiwa na akili zenye mwendo.
Lakini kadiri tunavyozeeka, akili zetu zinazidi kuuacha mwendo na kusimama.
Unaweza kudhani unahitaji kurudisha afya na mwonekano wako wa ujana, lakini unachohitaji hasa ni kurudisha mwendo wa akili yako.
Kila unapojikuta mawazo yako yakiamini na kusimama kwenye kitu kimoja pekee, isukume kuvuka kitu hicho na kwenda kwenye vitu vingine.
Kila mara tafuta kitu kipya cha kuiondoa akili yako kwenye mazoea yake.
Usilazimishe vitu ambavyo huwezi kubadili, endelea na mwendo kwenye vitu vingine vipya.
Sheria ya leo; Nenda na mambo jinsi yanavyokwenda. Iache akili yako iwe kwenye mwendo, kutoka wazo moja kwenda jingine na jukumu moja kwenda jingine. Ni akili iliyo kwenye mwendo ndiyo inakuwa na ubunifu wa hali ya juu na kukuwezesha kufikia na kudumu kwenye ubobezi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu