Rafiki yangu mpendwa,

Kitu kimoja kikubwa ambacho nimejifunza kwenye uandishi ni kuna wakati sisi waandishi tunatumika kama chombo cha kupitisha maarifa yanayohitajika sana kwa watu kwenye wakati husika.

Yaani unaweza kuandika kitabu wewe mwenyewe, lakini unapokuja kukaa chini na kurudia kukisoma, unajifunza mambo mengi ambayo yanakuwa ni mapya kabisa kwako.

Hilo limekuwa linatokea mara nyingi, lakini kuna kitabu kimoja ambacho kimedhihirisha hilo kwangu na kwa wengine pia.

Kabla sijakuambia ni kitabu gani, nikushirikishe kwanza ushuhuda kutoka kwa msomaji mwenzetu aliyenufaika sana na kitabu hicho.

“Habari na hongera kwa majukumu Dr. Makirita. Kwa jina naitwa Justina nimesoma vitabu vyako viwili ila kwa leo Napenda sana kukushukuru kwa kuandika kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA. Kitabu hiki naweza kukiita kama msingi wa mambo mengi na hasa katika kuikomboa fikra kwa sababu mafanikio yote yamefungwa katika fikra.  Natumaini kwa wale wanaopenda kusoma maandiko na kutamani kujua mambo ya rohoni wakisoma kitabu hiki wataelewa zaidi kwa maana kila kitu afanyacho mwanadamu kinaanzia rohoni alafu baadaye ndio kinatokea katika ulimwengu wa mwili. Nashauri yeyote ambaye hajasoma kitabu chako chochote aanze na kitabu hiki cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kama msingi wa kumfungua katika kifungo cha fikra. Nasisitiza kwamba kwa wale pia wanaoamini unabii wajue ya kwamba Nabii wa kwanza ni mtu mwenyewe unapo amini kwamba unaweza kutenda jambo na ukachukua hatua lazima ufanikiwe vinginevyo hata ukipewa unabii na usipo amini na kuchukua hatua hakuna kitakachotokea. Mit 6:2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako. Hiyo inamaanisha kile unachokiri ndio kinachotokea, ukikiri kushinda basi utashinda na ukikiri kushindwa hakika utashindwa.”

Kama alivyotushirikisha rafiki yetu Justina, kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ni kitabu cha kipekee sana katika vitabu vyote ambavyo nimeshaandika mpaka sasa.
Ni kitabu ambacho kinakwenda kuamsha nguvu kubwa kabisa ambayo tayari ipo ndani yako, ila imelala tu.

Ni kitabu ambacho kinakuonyesha jinsi unabii wowote ule unavyoanzia ndani yako na namna ya kuzitumia fikrs zako kufanya makubwa.

Kitabu kitakusaidia kuvunja fikra za ukomo ambazo zimekutawala kwa muda mrefu na kujenga fikra mpya za uwezekano ambazo zitakuwezesha kufanya makubwa.

Tupo mwanzo kabisa wa mwaka 2022,  mwaka ambao wengi wana matumaini ya kufanya makubwa.
Lakini tatizo ni moja, watu wanaingia kwenye mwaka huo mpya wakiwa na fikra zile zile za mwaka 2021.

Hata ufanye kazi kama punda, kama fikra na mtazamo wako ni ule ule, hakuna hatua kubwa utakazoweza kupiga.

Hivyo basi rafiki yangu, kama kweli umedhamiria kufanya makubwa kwenye mwaka huu wa 2022, anza sasa kwa kusoma kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

Uanze mwaka huu ukiwa umezifungua kweli nguvu zako ili kila juhudi unayoweka iweze kuzalisha matokeo makubwa kweli kweli kwenye maisha yako.

Unaweza usielewe nguvu ya hili ninalokuambia sasa, lakini niamini mimi kama rafiki yako na upate na kusoma kitabu cha NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, utanishukuru sana baadaye.

Rafiki, wasiliana sasa na 0752 977 170 ili uweze kupata nakala yako ya kitabu na uanze kuukabili mwaka 2022 kwa namna ya kipekee.
Kama upo Dar utaletewa kitabu popote ulipo na kama umpo mkoani basi utatumiwa kwa njia ya basi.

Chukua hatua ya kupata na kusoma kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA leo ili mwaka wako 2022 uweze kuwa wa kipekee kabisa.
Na kama kuna watu unataka kuwapa zawadi mwaka 2022, basi kitabu hicho ni zawadi nzuri, kipate na uwapatie zawadi.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.