Wakati wa kujifunza na kufanya kitu kipya, mishipa mingi ya fahamu huwa inazaliwa kwenye ubongo wa mbele.
Mishipa hiyo ndiyo inayotuwezesha sisi binadamu kujifunza na kufanya mambo mapya.
Wakati huo wa kujifunza ubongo huwa na kazi nyingi, huwa katika hali ya msongo.
Lakini kitu kikisharudiwa rudiwa kwa muda mrefu, kinakuwa sehemu ya ubongo na kuhamishiwa kwenye ubongo wa chini.
Hapo ubongo wa mbele unakuwa huru kujifunza vitu vingine vipya, unakuwa umerudi kwenye hali yake ya kawaida.
Hili linatuonyesha nguvu mbili kubwa za ubongo.
Nguvu ya kwanza ni ubongo haujai, hivyo mtu anaweza kujifunza mambo mengi awezavyo bila kufika hatua ya kuona ubongo umejaa na hauwezi kupokea tena.
Nguvu ya pili ni ukishajifunza kitu kwa kina kinakuwa sehemu yako, inakuwa rahisi kukifanya bila hata ya kufikiri sana.
Sheria ya leo; Kadiri unavyojifunza ujuzi mwingi, ndivyo ubongo wako unavyokuwa na uwezo mkubwa zaidi. Ni juu yako kuamua utumieje ubongo wako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji