#SheriaYaLeo (95/366); Jua wakati wa kutoa na kupokea sifa.
Huwa tunapenda kupewa sifa kwa kile ambacho tumewezesha kifanyike au kikamilike.
Ni kawaida kwetu binadamu kupenda kusifiwa, kwani huwa tunaona tumethaminiwa zaidi.
Kama ambavyo tunajisikia vizuri tukisifiwa, ndivyo pia wengine wanajisikia vizuri wanaposifiwa.
Na hapa ndipo unapaswa kujua wakati gani wa kutoa na kupokea sifa ili isiwe kikwazo kwako kuyafikia mafanikio unayotaka.
Kwa wale walio juu yako, mara zote wape sifa.
Hata kama kitu ni wewe umefanya na ndiyo unastahili sifa zote, usihadaike na hilo. Wape sifa wale walio juu yako kwa kila matokeo mazuri yanayopatikana
Hilo litawafanya wajisikie vizuri na kuwa tayari kukupa fursa za kukua zaidi.
Kwa wale walio chini yako mara zote chukua sifa.
Kwa chochote kilichofanyika na walio chini yako, hakikisha sifa zote zinakuja kwako.
Kwa njia hiyo utaweza kuzitumia sifa hizo kupiga hatua zaidi kufika kule unakotaka kufika.
Sifa ni kitu kinachoweza kuonekana ni kidogo, lakini ukishindwa kukitumia vizuri kinaweza kuwa kikwazo kwako kufika ngazi za juu za mafanikio.
Sheria ya leo; Kwa wale walio chini yako, chukua sifa kwa matokeo yaliyopatikana. Kwa wale walio juu yako, wapo sifa kwa matokeo yaliyopatikana. Cheza na sifa kujenga kukubalika ili upate fursa nzuri unazozitaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji