2604; Kiashiria kwamba umepotea.
Kwenye safari ya mafanikio, kiashiria kikubwa kwamba umeshapotea njia ni pale unapojikuta upo upande wa wengi.
Iko hivi rafiki, kwenye kila jamii, huwa kuna upande wa wengi, ambao wanakubaliana kwenye mengi ila hawafanikiwi.
Halafu kuna upande wa wachache ambao hawakubaliani na yale ya wengi na ndiyo wanaofanikiwa sana.
Walio wengi hawapendi na hawapo tayari kujitesa na kujisukuma.
Hakuna mafanikio bila kujitesa na kujisukuma.
Walio wengi wanapenda kuwafurahisha na kuwaridhisha watu wote.
Hakuna mafanikio bila kuwaangusha baadhi ya watu.
Walio wengi wanajiendea tu kwa mazoea, hawana kitu chochote kikubwa kinachowasukuma kwenda tofauti.
Hakuna mafanikio kwenye mazoea.
Hatua za kuchukua;
Jitathmini kwenye lile eneo unalotaka kufanikiwa, ukijikuta upo upande wa wengi, jua umeshapotea njia, rudi kwenye misingi yako haraka ili ukae kwenye njia sahihi kwa mafanikio yako.
Usipokuwa mtu wa kujikagua mara kwa mara kwa kujifanyia tathmini, ni rahisi sana kupotea, maana ushawishi wa wengi ni mkubwa.
Tafakari;
Unapojikuta upo upande wa wengi na unakubaliana na kila mtu, ni wakati wa kujitathmini kwa kina maana unakuwa umeshaiacha njia yako ya mafanikio makubwa.
Wale waliokuwa wanakuona wa ajabu wanapoanza kukuelewa, jua umelegeza sana.
Kocha.
Leo najifanyia tathmin nirudi njia kuu..hii Safari kwa kweli sio rahisi Kama ambavyo kocha husema.
LikeLike
Unarudi kweli?
LikeLike