#SheriaYaLeo (108/366); Usijiingize kwenye migogoro ya wengine.

Mara zote epuka sana kujiingiza kwenye migogoro ya watu wengine.
Hilo halina manufaa kwako kwenye malengo yako ya kupata mafanikio makubwa.

Watu watajaribu kukuvuta na kukushawishi uwe upande wao, lakini epuka sana ushawishi huo.

Onyesha kuwaelewa na kujali, lakini epuka sana kujiingiza kwenye migogoro yao.

Unapojiingiza kwenye migogoro ya wengine, unapoteza nguvu zako kwenye mapambano yasiyokuwa na tija yoyote kwako.

Okoa nguvu hizo na uziwekeze kwenye yale sahihi kwako kufikia mafanikio unayoyataka.

Ndani yako dumisha utulivu mkubwa ili uweze kuchukua hatua sahihi kuyafikia mafanikio yako.

Sheria ya leo; Mara zote kazana kutunza uhuru wako na epuka sana kujiingiza kwenye migogoro ya wengine. Usikubali kuchoshwa na kuvurugwa na mambo yasiyo na tija kwako. Kwenye kila mgogoro tayari kuna mpumbavu mmoja, usiende kuwa wa pili.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji