2673; Huo muda unaupata wapi?
Kama kuna changamoto unazopitia kwenye maisha yako, lakini bado pia unahangaika na mambo yasiyokuwa na tija, ni jambo la kushangaza.
Kama una ndoto kubwa ambazo bado hujazifikia, lakini una mambo yasiyohusiana na ndoto hizo ambayo yanakutinga, ni vigumu kueleweka.
Unapokuwa na changamoto zinazokukabili, inapaswa muda wako wote na juhudi zako upeleke kwenye kutatua changamoto hizo.
Unapokuwa na ndoto kubwa kabisa unazotaka kuzifikia, hakuna kingine kinachopaswa kuwa kipaumbele kwako zaidi ya ndoto hizo kubwa.
Hivyo vitu visivyo na tija havipaswi kupata muda wala umakini wako.
Changamoto zinawakwamisha wengi kwa sababu hawazipi muda na juhudi za kutosha. Hilo linasababishwa na mahangaiko wanayokuwa nayo kwenye mambo mengine.
Wengi hawazifikii ndoto zao kubwa kwa sababu hawazipi kipaumbele cha kwanza.
Wanahangaika na mengine yasiyo na tija, yanawachosha na kujikuta hawawezi kuhangaikia ndoto zao.
Hatua ya kuchukua;
Kila siku andika changamoto kubwa inayokukabili au ndoto kubwa unazotaka kufikia.
Hilo ndiyo linakuwa jukumu kubwa na la kipekee kabisa kwako.
Hakuna kingine chochote kinachopaswa kuondoa muda, umakini na juhudi zako kwenye hilo.
Na hivyo ndivyo unavyoweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Tafakari;
Biashara inakuhangaisha lakini bado unapata muda wa kuwa na michepuko, kushabikia michezo, kuperuzi mitandao na kufuatilia maisha ya wengine.
Halafu unalalamika mambo ni magumu, wewe mwenyewe ndiye unaleta ugumu kwa kuhangaika na yasiyokuwa na tija.
Kocha.
Ukweli mtupu kocha wangu miluzi mingi hutupoteza siyo vizuri kufanya kila fursa, hakika we ni mtu wa pekee atakaye tuvusha kutupeleka mahala sahihi yaani kwenye mafanikio ya kweli.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike