#SheriaYaLeo (185/366); Usijiangalie mwenyewe, waangalie wengine.
Wanaotaka kushawishi wengine huwa hawajiangalii wao wenyewe, bali huwa wanawaangalia zaidi wengine. Hawajiangalii zaidi ndani yao, bali wanaangalia zaidi nje.
Hiyo ni kwa sababu kubwa mbili;
Moja ni kujiangalia mwenyewe badala ya wengine ni dalili za kutokujiamini.
Na pale unapokuwa hujiamini huwezi kuwa na ushawishi kwa wengine.
Kila mtu huwa ana hali ya kutokujiamini kwenye mambo fulani, lakini washawishi huwa wanadhibiti hali hiyo isionekane kwa nje.
Badala ya kujiangalia wao wenyewe, wanawaangalia zaidi wengine.
Hilo linawafanya watu kuvutiwa kwao.
Mbili ni unapowaangalia zaidi wengine inakupa fursa ya kuwaelewa vizuri maana unakuwa umevaa viatu vyao. Hilo linakupa fursa ya kupata taarifa zaidi kutoka kwao na kukuwezesha kuwa na ushawishi mkubwa kwao.
Kwa kuwa na taarifa nyingi kuhusu wengine inawapa washawishi nguvu ya kukubalika na watu hao na kuweza kumpa kile anachotaka.
Kwenye dunia ambayo kila mtu anajiangalia zaidi yeye mwenyewe, kuweza kuwaangalia wengine kunakupa nguvu ya kipekee na kuweza kuwashawishi zaidi.
Sheria ya leo; Pale unapokutana na mtu, hatua ya kwanza unayopaswa kuchukua ni kuingia ndani ya ngozi ya mtu huyo, kuweza kuiona dunia kwa namna anavyoiona yeye. Hilo litakupa nguvu ya kuwa na ushawishi mkubwa kwake.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji