Rafiki yangu mpendwa,

Baba wa taifa la Tanzania, Mwl J. K. Nyerere, baada ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni aligundua hii nchi ni ngumu sana kuiongoza.

Baada ya tafakari ya kina, akagundua licha ya wakoloni kuondoka, bado kulikuwa na maadui wakubwa watatu walioendelea kuwepo na ambao ndiyo kikwazo kwa maendeleo ya taifa.

Aliwataja maadui hao ni UJINGA, MARADHI NA UMASIKINI.
Maadui hawa wamekuwa wanashirikiana kwa ukaribu kudhoofisha mtu mmoja mmoja na hata taifa kwa ujumla.

Mtu akiwa mjinga hawezi kulinda afya yake, hilo litapelekea apate maradhi ambayo yanamgharimu sana na kupelekea abaki kwenye umasikini.

Kadhalika pia mtu akiwa masikini hawezi kupata elimu bora na hata akipata maradhi hawezi kupata tiba bora.

Pamoja na maadui hao watatu kushirikiana kwa karibu, naamini kuna adui mmoja amechimba mzizi mrefu zaidi ambaye tukiweza kumng’oa huyo, basi hao wengine watakimbia wengine.

Adui huyo ni UMASIKINI.
Tukiweza kuweka nguvu zetu zote katika kutokomeza umasikini, basi ujinga na maradhi vitakimbia vyenyewe.
Maana vitu hivyo haviwezi kupata nafasi pale mtu anapokuwa ameutokomeza kabisa umasikini.

Baada ya kujifunza kwa kina kubusu watu na mafanikio, nimegundua kitu kimoja, tabia zetu huwa zina nguvu kubwa sana ya kuamua ni aina gani ya maisha tunayokuwa nayo.

Hivyo nimekuwa nasema, kile ambacho watu wanakiita laana si kitu kingine bali ni tabia.
Hakuna mtu yeyote anayekuachia laana akasababisha maisha yako kuwa magumu.
Bali ni tabia ulizojijengea ndiyo zinafanya maisha yako kuwa magumu.

Na hivyo kama unataka kubadili maisha yako na kuvunja kila aina ya laana, anza kwa kubadili tabia zako.

Inapokuja kwenye utajiri na umasikini, tofauti ya kwanza kabisa inaanzia kwenye tabia.
Kuna tabia ambazo matajiri wanazo na zinawanufaisha.
Na kuna tabia ambazo masikini wanazo na zinawakwamisha.

Kwa kuwa kile ambacho watu wanakiita laana ni tabia na kwa kuwa umasikini nao ni matokeo ya tabia, ndiyo maana nasema; UMASIKINI NI LAANA KUBWA.

Kama umejisikia vibaya kwa kusikia hivyo, basi uko sahihi kabisa. Bado upo kwenye umasikini na hiyo ni laana.
Uzuri ni umeshajua jinsi ya kuvunja laana hiyo, kwa kubadili tabia zako.

Lakini huenda unajiuliza ni tabia gani zinazokukwamisha, maana kwa maisha yako yote umekuwa unaenda vile unavyoenda mpaka sasa.

Na hapa ndipo nina habari njema sana kwako.
Habari njema ni kwamba kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, kitabu ambacho kinakupa mwongozo wa kuvunja tabia za kimasilini na kujenga tabia za kitajiri kipo tayari.

Hiki ni kitabu muhimu sana cha kusomwa na kila ambaye ameshachoshwa na laana ya umasikini na hataki tena kuendelea hivyo.

Kitabu hiki ni silaha imara ya kumshinda adui mkuu wa maisha yetu ambaye ni UMASIKINI.

Karibu sana usome kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI, ujifunze kwa kina na kuondoka na silaha muhimu ya kwenda kuivunja laana ya umasikini ambayo imekuandama maisha yako yote.

JINSI YA KUPATA KITABU.

Kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy) na nakala tete (softcopy).
Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo kwa hardcopy au kama utanunua softcopy utatumiwa kwa email.
Na kama upo nje ya Dar es salaam utatumiwa kitabu kule ulipo.

Kujipatia nakala yako ya kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, wasiliana na namba 0752 977 170 au 0678 977 007.

ZAWADI YA KITABU.

Rafiki yangu mpendwa,

Kwa kuwa umekuwa unafuatilia mafunzo ninayotoa kwa muda mrefu, nakwenda kukupa kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI KAMA ZAWADI.

Hivyo kwa siku hizi chache utakipata kitabu hiki kwa bei ya punguzo ambayo ni tsh elfu kumi na tano (15,000/=), badala ya bei yake halisi ambayo ni tsh elfu 20

Kitabu hiki kina thamani ya mamilioni kwako, ila wewe unakipata sawa na bure kabisa, kwa tsh elfu 15 tu.

Lengo langu ni wewe usiwe na sababu yoyote ya kukikosa, kwa sababu nataka sana uyabadili na kuyaboresha maisha yako na maarifa yaliyo kwenye kitabu hiki ndiyo unayahitaji sana.

Chukua hatua sasa rafiki yangu, zawadi hii ni ya muda mfupi, bei ya kitabu itakuwa kubwa zaidi baadaye hivyo usikubali kukosa.

Utajiri ni haki na wajibu wako, kama wapo wengine walioweza kufikia utajiri, na wewe pia unaweza kuufikia. Unachohitaji ni kuijua kanuni sahihi na kuifuata.

Kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI kina kanuni hizo, wajibu wako ni kuzijua na kuzifuata na utajiri kwako unakuwa swala la muda tu.

Jipatie kitabu chako sasa kwa bei ya zawadi, wasiliana na 0752 977 170 kukipata kitabu popote pale ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.