2713; Matamanio makubwa zaidi.
Hakuna ubaya wowote kwenye kuridhika haraka na kile ambacho mtu umekipata.
Lakini ili uweze kupata mafanikio makubwa zaidi, lazima mtu uwe na matamanio makubwa zaidi.
Ni matamanio makubwa ndiyo yaliyoisukuma dunia na kuifanya kuwa bora zaidi ya ilivyokuwa huko nyuma.
Ni watu ambao hawakuridhika na kile ambacho walikuwa wamepata ndiyo walioweza kupata zaidi.
Lakini jamii zetu kuna namna zimegeuza matamanio makubwa kuwa kitu kibaya kwa anayekitaka.
Wale wenye matamanio makubwa wamekuwa wakichukuliwa kama watu wasioridhika na wanaowanyonya wengine.
Bila ya kuvuka mtazamo huo hasi wa kijamii na kuwa na matamanio makubwa ambayo unayapambania bila kukata tamaa, hakuna makubwa utakayoweza kuyafanya kwenye maisha yako.
Bila ya kuendelea kuyakuza malengo yako kila unapoyafikia, utakwama kwenye mafanikio kidogo na kubaki kwenye mazoea ambayo yatakuletea anguko.
Mara zote dunia imekuwa inasukumwa na wale wenye matamanio makubwa, wale waliokataa kuridhika na yale ambayo wengine wameridhika nayo.
Hatua ya kuchukua;
Kuwa na matamanio makubwa kwenye maisha yako. Taka kupata makubwa na kufika ngazi za juu kabisa kwenye kile ambacho umekichagua.
Weka malengo makubwa na pambana kuyafikia.
Na unapoyafikia malengo uliyojiwekea, weka mengine ambayo ni makubwa zaidi.
Kila wakati hakikisha kuna malengo makubwa ambayo unayapambania.
Tafakari;
Kama huna matamanio makubwa ambayo jamii ya kawaida haiyaelewi, huna nafasi ya kufanya makubwa na kupata mafanikio makubwa.
Matamanio ni bure, hayauzwi au kutozwa.
Hivyo anza kwa kuwa nayo makubwa kisha kila siku yafanyie kazi mpaka uweze kuyafikia.
Usiridhike na chochote nje ya matamanio yako.
Na unapoyafikia matamanio hayo, weka mengine makubwa zaidi.
#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
Kweli kabisa kocha.
LikeLike
Karibu.
LikeLike