#SheriaYaLeo (218/366); Shinda kwa kutumia vitendo na siyo maneno.

Watu wengi huwa wanakazana sana kutumia maneno kwenye kuwashawishi wengine.

Lakini watu huwa ni wagumu sana kushawishika na kubadilika kwa kutumia maneno.

Kwa watu, matendo yana nguvu na ushawishi mkubwa kuliko maneno.

Hivyo pale inapowezekana kutumia vitendo, usihangaike sana na maneno.
Tumia vitendo ambavyo vina nguvu kubwa ya ushawishi kwa wengine ili waweze kukubaliana na wewe.

Sheria ya leo; Onyesha badala ya kueleza. Maonyesho yana nguvu kubwa ya ushawishi kuliko maneno matupu.
Kwa kila unachotaka kuwashawishi wengine wakubaliane na wewe, angalia ni hatua zipi unazoweza kuchukua na hilo litakuwa na ushawishi mkubwa zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji