#SheriaYaLeo (273/366); Kuwa tayari kubadilika.

Kila kitu kwenye maisha huwa kinabadilika.
Hivyo unapaswa kuchukulia kila kitu kwa kuendana na hali uliyonayo.

Maji ndiyo kitu chenye nguvu zaidi duniani, kwa sababu huwa yapo tayari kubadilika.
Maji huchukua nafasi kwenye chombo chochote ambacho yanawekwa.

Hivyo kuwa tayari kubadilika kama maji ndiyo mkakati mkuu wa ushindi kwenye maisha.
Huo ni mkakati unaopingana na mikakati mingine.
Kwa sababu ni mkakati unaokutaka kupuuza sheria nyingine zote.

Unapaswa kufanya maamuzi kulingana na jinsi kitu kilivyo wakati unakikabili.
Unapaswa kuielewa hali ya kitu ambacho upo, kisha kuendana nacho badala ya kutumia mazoea.

Unapaswa kuyaona mambo kwa macho yako mwenyewe na kufanya maamuzi baada ya kufikiri kwa kina.
Unapaswa kupuuza ushauri ambao wengine wanakupa kila wakati.
Unaachana na sheria wanazohubiri wengine pamoja na vitabu wanavyoandika kukuambia nini cha kufanya.

Napoleon Bonabarte aliwahi kusema, sheria inayotawala hali fulani, inavunjwa na hali nyingine mpya.
Hivyo kwa kila hali mpya unayokutana nayo, badala ya kuikabili kwa mazoea, unapaswa kuwa tayari kubadilika.
Badilika kuendana na kila hali ili kuweza kupata matokeo mazuri.

Sheria ya leo; Kubaliana na ukweli kwamba hakuna kitu chochote ambacho ni cha uhakika au mkakati imara. Njia bora ya kujilinda ni kuwa tayari kubadilika kama maji, kubadilika kadiri mambo na hali zinavyobadilika.
Kila kitu kinabadilika, usibaki kwenye mazoea.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji