Dhambi kuu mbili za kuepuka ili ufanikiwe.

Tumezoea kusikia dhambi kwenye mambo ya kiimani na kidini.
Dhambi ikiwa ni matendo unayofanya ambayo yanakukosesha kile kizuri ambacho ungeweza kukipata.

Kwenye mafanikio pia kuna dhambi zake, mambo ambayo ukiyafanya unajikosesha mafanikio wewe mwenyewe.

Kuna dhambi nyingi ambazo zimekuwa zinawazuia watu kufanikiwa.
Lakini kwa uzoefu wangu, hasa baada ya kufanya kazi na watu wengi kwenye eneo la mafanikio, kuna dhambi kubwa mbili ambazo ndiyo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wengi kufanikiwa.

Dhambi hizo ni UVIVU NA UZEMBE.

Uvivu ni pale unapojua unachopaswa kufanya, ila unachagua kutokukifanya.
Yaani unajua kabisa unapaswa ufanye nini ili ufanikiwe, lakini unachagua kutokufanya.

Unajua unapaswa kuamka asubuhi na mapema ili kuianza siku yako vyema, lakini bado unalala kupitiliza.
Unajua unapaswa kuweka juhudi zaidi kwenye kazi, lakini hufanyi hivyo.

Ukijikagua wewe mwenyewe, utagundua mafanikio yoyote ambayo hujayapata, imetokana na uvivu, kujua unachopaswa kufanya lakini bado hukukifanya.

Dhambi ya pili ya uzembe, hii unafanya vitu chini ya kiwango au kwa mazoea.
Hii inaweza kuonekana ni afadhali, kwamba angalau mtu anafanya.
Lakini ufanyaji wake unakuwa siyo wa kuridhisha na wakati mwingine unakuwa na hasara kuliko kutokufanya kabisa.

Uzembe siyo tu unakukosesha unachotaka, bali pia unatengeneza matatizo mapya na makubwa ambayo yanazidi kukudidimiza.
Fikiria kukosa nidhamu ya kifedha kunavyokuwa chanzo cha wengi kuingia kwenye madeni.
Au kukosa umakini kwenye biashara kunavyozalisha hasara na kupelekea biashara nyingi kufa.

Rafiki, leo nataka utubu hizi dhambi mbili na kuhakikisha unaziondoa kabisa kwenye maisha yako.
Ninayo njia ya uhakika ya kuhakikisha hurudi tena kwenye dhambi hizo mbili ambazo ndiyo zimekutesa mno kwenye maisha yako.

Na hilo linaanzia kwenye eneo la kipato, ambapo uvivu na uzembe vimechangia sana uwe na kipato kidogo pamoja na madeni.

Kuhakikisha unaondokana na hilo, nimekuandalia mpango maalumu wa KIPATO ZAIDI, kama bado hujaupata soma hapo chini;

👇👇👇

Kama unataka kuongeza kipato chako zaidi ya unavyopata sasa, na kama upo tayari kufanyia kazi mpango wa uhakika wa kufikia hilo, karibu sana tufanye kazi pamoja.

Fungua kiungo hiki; https://t.me/kochadrmakirita na andika ujumbe KIPATO ZAIDI halafu nitakupa mpango mzima.
Mpango huo ni rahisi na wa uhakika, lakini utakutaka uweke juhudi na muda.
Hivyo kama wewe ni mtu sahihi, karibu.

Rafiki, ambacho sikitaki kwako ni wewe kuyaweka matumaini yako ya kuongeza kipato kwa mtu mwingine.
Hicho ni kitu unachopaswa kukijenga wewe mwenyewe.

Ninachotaka kwako ni Mei Mosi ya mwaka 2023 ujiambie kwa uhakika kwamba nimeongeza kipato changu kwa asilimia Z.
Z ikiwa ni asilimia yoyote utakayokuwa umechagua utakapokuja tufanye kazi pamoja.

Rafiki, kama upo tayari kwa hili, fungua hapa sasa hivi; https://t.me/kochadrmakirita na andika ujumbe KIPATO ZAIDI na tutaanza mchakato mara moja wa kuhakikisha Mei Mosi ijayo unacheka kwa furaha huku wenzako wakiwa bado wana manung’uniko.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr Makirita Amani
https://t.me/kochadrmakirita