#SheriaYaLeo (307/366); Epuka kuvurugwa na hisia za wengine.
Ili ufanikiwe, lazima uweze kudhibiti hisia zako.
Lakini hata ukiweza kufanikisha hilo, bado hutaweza kudhibiti hisia za wale wanaokuzunguka.
Na hilo linakuwa hatari kubwa kwako.
Watu wengi wanaendeshwa kwa hisia. Kila mara wakiwa wakiwa wanalipuka na kukabiliana na migogoro mbalimbali.
Wanapokuona wewe una udhibiti na utulivu na hausumbuliwi na hisia kama wao, hawatafurahishwa na hilo.
Hivyo watajaribu kukuingiza kwenye hisia zao.
Watakuomba ukae upande wao au uwasaidie kutatua matatizo yao.
Kama utakubali, kidogo kidogo unajikuta ukiingia na kuvurugwa na hisia zao, kitu ambacho kitaharibu sana udhibiti na utulivu wako.
Usikubali huruma yoyote ikuingize kwenye hisia za wengine. Huo ni mchezo ambao huwezi kushinda kwa namna yoyote ile. Badala yake matatizo yatazidi kukua.
Unaweza kuhofia watu watakuona una roho mbaya na hujali mambo yao kwa kukataa kuvurugwa na hisia zao.
Lakini mwisho wa siku, kwa udhibiti na utulivu utakaokuwa nao, utakufanya ukubalike na kuheshimika zaidi na wengine.
Na hapo utaweza kuwasaidia kwa namna utakayoona ni sahihu kwako, ili kuendelea kulinda utulivu na udhibiti wako.
Sheria ya leo; Kumbuka muda wako na nguvu vina ukomo. Kila mara unapotumia kujihusisha na matatizo ya hisia za wengine, unapunguza uimara wako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji