Sababu Moja (1) Kubwa Nyuma Ya Ugomvi Wowote Ule.

Rafiki Yangu,

Heri Ya Mwezi Mpya.

Mara ya kwanza niliposikia hiki unachokwenda kukisikia mda mchache ujao sikufichi kilinipa mshtuko wa moyo.

Na sio  mshituko tu ata simu yenyewe nilidondosha.

Na kwa kuwa napenda kusimama basi ikanibidi nikae.

Hili ni tukio la kutisha lililotokea Miaka Ya 90 Manispaa Ya Morogoro Tanzania.

Palikuwepo na VIPOFU 6 wa KIUME  ambao mara nyingi walikuwa wanapendelea kusimama pembezoni mwa barabara.

Na vikombe vyao na kutegemea kusaidiwa chochote kitu na wapita njia (watembea kwa miguu).

Kwa lugha rahisi sana, walijulikana kama ombaomba.

Gafla siku moja NDOVU alionekana ng’ambo maeneo ya karibu walipo VIPOFU.

Na kwa sababu VIPOFU hawaoni hawakujua kinachoendelea.

Kesho yake Asubuhi Yule NDOVU akaamua kuvuka barabara (upande alipokuwepo) na kuja upande wa pili walipo VIPOFU.

Na kwa kuwa wale VIPOFU walikuwa hawaoni wanahisi tu basi kwa mshangao walimzingira Yule NDOVU bila kujua kama ni NDOVU.

Na kwa kuwa walikuwa wanapenda kubishana sana.

Basi wote 6 kila mmoja akakimbilia kushika sehemu ya mwili wa NDOVU.

Na kwa kuwa walikuwa hawana wasiwasi wote ule.

Na chakushangaza Yule NDOVU alitulia kama kanyeshewa na mvua vile.

Kwa kuwa walikuwa 6 walishika sehemu 6.

Wakwanza(1) alishika MGONGO.

Wapili(2) alishika PEMBE-JINO.

Watatu(3) alishika MKONGA.

Wanne(4) alishika MGUU.

Watano(5) alishika SIKIO.

Na

Wasita(6) alishika MKIA.

Baada ya kila KIPOFU kushika Sehemu Yake.

Wakaanza kutambiana.

Na kwa sababu walizoea kubishana na kutambiana basi kila mmoja akawa anasifia kile alichokishika.

Na kwa kuwa hawaoni wakaambiana kila mmoja aseme kile alichoshika.

Yule wa KWANZA aliyeshika MGONGO akajigamba yeye KASHIKA UKUTA.

Yule Wa PILI aliyeshika PEMBE akaanza kumkosoa aliyeshika MGONGO akimwambia wewe huna bahati MIMI NIMESHIKILIA CHUMA KIKALI.

Yule wa TATU sasa aliyeshika MKONGA akaanza kuwakosoa wote wawili akiwaambia nyie hamjui chochote yani MIMI HATA SIOGOPI NIMEMSHIKA NYOKA NA AMETULIA TULITULI.

Yule wa NNE aliyeshika MGUU akaanza kwa kuwacheka wote watatu akiwaambia NYIE MNASHIKA VITU VYA AJABU SANA BADALA YA KUSHIKA MTI ULETAO MVUA Mnaanza kushika vitu ambavyo havina msaada wowote kwa jamii.

Yule wa TANO aliyeshika SIKIO akaanza kuwakosoa wote wanne waliotangulia huku akiwaambia mnaacha kukimbili FENI ambayo inawapa ka ubaridi kwa mbali mnaanza kuangaika na vitu vitakavyo wachosha.

Wa SITA sasa aliyeshika MKIA akaanza kwa kuwaambia AFADHALI MIMI NILIYE BAHATIKA KUSHIKA KAMBA KULIKO NYIE NYOTE  KWA SABABABU KAMBA ITANISAIDIA KUFUNGA VITU MBALIMBALI.

Akaanza kuwatambia wenzake na kujisifu yeye ndiye BABALAO na wakome kujilinganisha na yeye akiwa anamaanisha kwamba  Faida Za KAMBA hawawezi kuzilinganisha na UKUTA, CHUMA KIKALI,NYOKA, MTI, na FENI.

Sio kitu.

Yeye ndiye  kashikilia kitu cha maana zaidi kuliko wenzake.

Unaambiwa kati ya wale watano hakuna aliyekubali kashikilia kitu cha hovyo.

Kila mmoja alishikilia kile alichoamini ni sahihi kwa sababu wote hawaoni wanahisi tu kwa kushika.

SOMO;

Hilo tukio la kutisha linatukumbusha kuhusu uhalisia wa maisha yetu.

Na msingi wa matatizo tuliyonayo.

Mara nyingi watu ufikiri wapo sahihi muda wote na wengine ni wakosefu.

Lakini ukija kuchunguza kwa makini ni kwamba tu wanashindwa kuwaelewa wengine.

Na pale mtu anaposhindwa kuwaelewa wengine.

Apo ujue matokeo yake lazima atajiingiza kwenye ubishi.

Na ubishi mara nyingi husababisha ugomvi.

Hii ndio sababu leo hii magomvi kwenye familia yanaongezeka.

Magomvi kati ya rafiki na rafiki nayo yanaongezeka.

Magomvi kati ya Jamii moja na nyingine nayo yanaongezeka.

Magomvi kati ya waumini wa dini moja na nyingine nayo yanaongezeka.

Na sababu nyuma ya yote haya ni,

Wanashindwa kuelewa mitazamo ya wengine.

Na kama tutaweza kufungua  mbongo zetu na tukajaribu kuelewa mawazo ya wengine.

Basi migogoro kwenye dunia ingeisha watu wangeheshimiana na kuheshimu mawazo ya wengine.

Siku Ikifikia hali hii upendo utatawala sana hii dunia.

Na wengi wangeona hapa Duniani ni sehemu pazuri pa kuishi ,

… kwa sababu watu wangependana ukweli wa kupendana na sio kinafki tena.

Hata Hivyo, Rafiki yangu kama unataka uishi hapa duniani maisha ya AMANI na FURAHA.

Nakushauri usome SHERIA 100 ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Uzuri ni kwamba Sheira zote hizi utazikuta ndani ya kitabu hiki cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.

Tuwasiliane kwenye namba hii 0752977170 nikupe maelekezo ya kupata kitabu hiki.

Irudie 0752977170.

Nakupenda.

Shabiki Yako #1,

Bwana AmiriRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|