#SheriaYaLeo (318/366); Usivurugwe na wapumbavu.
Huwezi kuwa kila mahali na huwezi kupambana na kila mtu.
Muda wako na nguvu zako ni rasilimali zenye uhaba, unapaswa kujifunza jinsi ya kutunza rasilimali hizo.
Kuchoka na kuvurugwa ni matokeo ya upotevu wa rasilimali hizo na inavuruga sana uwepo wa kiakili.
Dunia imejaa wapumbavu – watu ambao hawawezi kusuburi ili kupata matokeo mazuri, wanaobadili mawazo yao kama upepo na wasioweza kuona zaidi ya pua zao.
Utakutana na wapumbavu hao kila mahali, kuanzia bosi asiye na maamuzi, mwenza asiyejali na wasaidizi wanaopagawa.
Unapokuwa unafanya kazi na wapumbavu, usipingane wala kuhangaika nao.
Badala yake wachukuliwe kama unavyowachukulia watoto au wanyama wadogo wadogo, ambao huruhusu wavuruge utulivu wako wa kiakili.
Uwezo wa kubaki na uchangamfu mbele ya wapumbavu ni ujuzi muhimu unaopaswa kujijengea na kuutumia.
Sheria ya leo; Jitenge na wapumbavu kihisia. Na wakati kwa ndani unawacheka kwa upumbavu wao, endelea kuwazamisha kwenye mawazo yao ya kipumbavu.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji