2950; Yule kuku aliyekuwa anataga sana.
Rafiki yangu mpendwa,
Kila kitu kwenye maisha huwa kinakuja na tarehe ya mwisho wa matumizi.
Kwa Kiingereza wanaita expire date.
Kila kitu, ikiwepo mimi na wewe.
Na hiyo haimaanishi tu kifo, bali mwisho wa matumizi ya uzalishaji mkubwa.
Kama umewahi kufuga, unakumbuka kuku uliyekuwa naye, ambaye alikuwa anataga sana. Kila mtu alimpenda sana kuku huyo. Lakini nini kilitokea?
Alifika mahali akawa hatagi tena na hatimaye kisu kikampitia, akawa kitoweo.
Wakati anataga vizuri hukufikiria kumchinja, lakini alipoanza kutokutaga vizuri, hukufikiria mara mbili kumchinja.
Inawezekana pia ni ng’ombe umewahi kuwa naye, ambaye alikuwa anatoa maziwa mengi mno.
Alitunzwa vizuri kipindi hicho akitoa maziwa mengi. Lakini alipoanza kupunguza maziwa anayotoa, shoka lilimpitia bila huruma.
Hukujiambia ng’ombe huyu alikuwa anatoa maziwa mengi huko nyuma, wacha tumsubirie atatoa tena.
Ulijua vyema, wakati wake wa uzalishaji nzuri umepita, kilichobaki ni awe kitoweo.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mimea, huenda umewahi kuwa na miti ya matunda ambayo ilikuwa inazalisha matunda kwa wingi. Labda ni machungwa, maembe au mapapai. Mimea hiyo ilipoacha kuzalisha matunda kwa wingi, ilikatwa pale ilipoonekana ina matumizi bora zaidi kwa kukatwa kwake.
Somo kubwa sana tunalojifunza kwenye mifano hii ya asili ni kila kitu kina matumizi wakati kina uzalishaji mzuri.
Lakini kipindi cha uzalishaji kinapopita, kitu hicho huwanyiwa matumizi mbadala.
Hakuna anayesubiri kitu hicho kirudi kwenye uzalishaji wake, maana inafahamika haiwezekani kurudi tena.
Tunaelewa hilo kwenye asili, lakini tunashindwa kulielewa kwa watu.
Kuna watu huwa wanakuwa na uzalishaji mzuri sana kwa kipindi fulani.
Tunafurahishwa na uzalishaji wao, kwa kuwa unatunufaisha sana.
Tunakuwa tayari hata kuwapa upendeleo, kwa sababu ya matokeo mazuri wanayotupa.
Halafu wanafika hatua ambayo hawana tena uzalishaji kama wa awali.
Wakishafika hatua hiyo, hatukubali kwamba muda wao wa uzalishajiu umeisha. Bali tunasubiri warudi kwenye uzalishaji wao wa nyuma, kitu ambacho hakitokei.
Tunasubiri huku wakiendelea kuwa mzigo kwetu.
Tunachosahau au kushindwa kuelewa na kukubali ni kipindi chao cha uzalishaji kimepita na hakiwezi kurudi tena.
Hivyo kinachofuata ni kuondolewa kwenye nafasi zao ili wawekwe watu wengine wanaoweza kuwa na uzalishaji mkubwa.
Tunachelewa sana kufanya hivyo, mpaka tunapata hasara kubwa.
Hii inatokea kwa wafanyakazi wazuri unaoweza kuwa nao kwenye biashara yako. Kuna kipindi wanakuwa wazuri sana, wanazalisha kwa wingi na unafurahia.
Lakini baada ya muda uzalishaji wao unapungua sana. Badala ya kukubaliana na asili kwamba muda wao umekwisha, wewe unaendelea kung’ang’ana nao, ukitegemea watarudi kwenye ubora wao wa awali.
Kitu ambacho huwa hakitokei na inatugharimu.
Inaweza kuwa ni wateja, ambao awali walikuwa wazuri sana, wananunua kwa wingi na kulipa kwa wakati. Wakawa chanzo cha faida nzuri kwetu, tukawapenda na kuwategemea.
Halafu wanafika hatua hawawezi tena kununua kwa wingi na wanasua sua kwenye malipo. Unatumia uzoefu wao wa nyuma kuendelea nao na wanakuwa chanzo cha matatizo makubwa.
Hata kwa upande wa wasambazaji, unaweza kuwa na wasambazaji wanaofanya vizuri, wanakupa mali kwa wakati katika hali bora. Halafu wanaanza kukusumbua.
Na pia inaweza kuwa ni wewe mwenyewe. Mwanzoni ulikuwa na shauku na msukumo mkubwa vilivyofanya uweke juhudi kubwa kwenye biashara zako. Baadaye inakuwa ni kama taa imezimwa, shauku na msukumo vinazima ghafla.
Unaendelea kujisukuma na kujiburuza kwenye biashara hiyo lakini hakuna jema linalotokea.
Unakuwa umefikia kipindi cha mwisho cha matumizi kwenye aina hiyo ya biashara na unapaswa kujiondoa kabla hujaiangusha kabisa.
Unadhani kwa nini makampuni makubwa huwa yanawaondoa viongozi wake wa juu.
Au timu za mpira zinafukuza makocha wake.
Kwa sababu kipindi cha matumizi kwao, katika hali wanayokuwepo, kinakuwa kimeisha.
Inapokuja kwa watu na hata kwako mwenyewe, endeleza kipimo unachotumia kwa mimea na wanyama. Kuna kipindi kizuri cha uzalishaji ambapo unanufaika. Na kipindi hicho kinapopita, inapaswa kuondolewa. Kisu, panga au shoka vinahusu.
Ndiyo, kuna wakati tatizo la uzalishaji linaweza kuwa la muda mfupi tu, ila baadaye uzalishaji ukarudi.
Lakini wote tunajua pale ambapo uzalishaji umefika mwisho na hauwezi kurudi tena.
Inapokuja kwenye biashara yako na mengine yanayokuhusu, chukua hatua sahihi kwa watu na hata kwako pia.
Pale uzalishaji unapokuwa vizuri kuwa hata na upendeleo.
Lakini uzalishaji unapokuwa na ukomo, usiendelee kung’ang’ana na kitu.
Chukua hatua sahihi kwa wakati badala ya kuendelea kukumbatia hasara.
Kumbuka kila kitu huwa kinakuja na tarehe ya mwisho ya matumizi yake.
Kwa watu tarehe hizo hazijaandikwa usoni.
Bali utaweza kuzipima kwa mwenendo wa uzalishaji.
Fuatilia sana mwenendo huo kwa kila unayejihusisha naye na usisite kuchukua hatua sahihi.
Matokeo ya nyuma yasikuzuie kufanya maamuzi sahihi sasa.
Jaribu kufanya kila njia kumsaidia mtu kuboresha uzalishaji wake.
Pale inaposhindikana, basi jua muda wa mwisho wa matumizi umefika.
Na kinachofuata ni kisu, panga au shoka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakika kocha ctokubali kuwa kitoweo
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante sana Kocha
LikeLike
Ni kweli ya kufikirisha. Kila kitu kina mwisho wake wa Matumizi. Na mwisho huo ufanyiwe maamuzi magumu kama kuku aliyeacha kutaga, Au ng’ombe aliyeacha kutoa maziwa Au mti ulioacha kuzaa matunda. Yaani uchinjwe Au kung’olewa kabisa
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante kwa makala hii kocha.Jitihada tunazozifanya kwenye biashara kwa kukaa kwenye mchakato kila siku ni muhimu kwani kwa kupitia hili washindani wetu hata kama wana nguvu kiasi gani itafikia kipindi watachoka na hapo na sisi katika ubora wetu tutaweza kuliteka soko.Pia tusiangalie watu kwa tulipotoka ila kwa uzalishaji walionao kwa wakati huo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana Kocha, Makala hii imenijenga sana kuchukua hatua kwa kila kitu, biashara, wafanyakazi hata mimi mwenyewe binafsi. 🙏🏽
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana Kocha. Ni kweli kabisa kila kitu kinaexpring date. Muhimu ni kujua kama muda wetu au muda wa watu tunaojihusisha nao wa kuexpire kwenye kila tunachofanya umeshafika. Hii itatusaidia kujitenga na madhara au hasara tunazo weza kuzisababisha. Muhimu: sisi binadamu; expiring date yetu haiko wazi kwa sababu tunafursa ya kukua zaidi au kujiupdate. Pale mtu anaposhindwa kukua au kujali eneo la maendeleo binafsi; lazima ataisha matumizi yake.
Asante
LikeLike
Kweli kabisa,
Expire date nyingi zinakuja kwa uzembe.
Mtu akitambua mapema na kuchukua hatua sahihi, hawezi ku expire
LikeLike
naepuka,shoka,kisu na kuisha muda wa matumizi kwa kukaa kwenye mchakato ili kuendelea kuwa bora zaidi kwa kuongeza maarifa kila siku
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante Sana kocha kwa makala nzuri. ni kweli kabisa kila
kitu huwa kina expire, kwa upande wetu binadamu tuna
weza kumtambua mtu kuwa ameexpire kwa kuangalia matokeo ktk kile anachofanya au alichokuwa anakifanya.
Katika makala hii nimejifunza mengi ,kubwa tathimini za kila siku, kila wiki ,na nk. Ni nyenzo mhimu Sana , sio kuandika tuu Bali ni kuziandika na kuzifuatilia kwa umakini mkubwa pia kwa msimamo ili kutambua pale ulipo .
LikeLike
Kisu panga au shoka kwa wale ambao hawafanyi uzalishaji kwenye biashara. Asante sana kocha kwa makala hii ya kipekee
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kila kitu kina mwanzo na mwisho kwenye .
Lazima kizaliwe, kukuwe na kife
LikeLike
Asante sana Kocha Kwa kutu kumbusha Hili. Sipo tayari kupata maumivu ya shoka. Nita jiepusha nalo Kwa namna yoyote Ile.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Renovation inahitajika kila siku,kujinoa ili kuwa mzalishaji na kuhitajika kutumika ili panga ,shoka ,kisu visinikumbe
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Ahsante sana Kocha, hii makala nzuri nzuri sana. Kweli kuna muda unafika mtu anakuwa hazalishi tena inabidi kisu, panga au shoka limpitie tu awe kitoweo bila huruma.
Nimeipenda sana🔥🔥
#NidhamUpendo
LikeLike
Kabisa
LikeLike
ahsante kocha kwa makala hii, kitakachosaidia kujua kama muda wa kisu, panga na shoka umefika ni pamoja na kufanya tathimini na upimaji wa ufanisi wa timu.
ahsante
LikeLike
Ndiyo, lazima uweze kupima kwa vigezo vya wazi kabisa ili usifanye maamuzi ya hisia.
LikeLike
Kila kitu kina mwisho wake wa kufanya vizuri ,pale ninapoona jambo halileti matokeo kama ilivyokua mwanzo basi mwisho wa hicho kitu umefika,ili kuepuka kuumia kwa kukingangania napaswa kukiondoa ili kuweka kitu kingine kitakachokua na matokeo mazuri zaidi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kila kitu huwa kinakuja na tarehe ya mwisho ya matumizi yake…..
LikeLike
Tujue wakati unapofika na kuchukua hatua sahihi.
LikeLike
Ahsante sana kocha kwa makala hii ntajitahidi kujisukuma ili nisiwe kama yule kuku anaetaga sana
LikeLike
Fanyia kazi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Tuwekeze sana ili tukifikia expired date tusiwe mizigo kwa wengine.
LikeLike
Asante sana kocha nimeanza na wateja lazima shoka liwapitie wengi kwani mazoea yameanza na inakuwa mzigo kwa biashara yangu. Asante na siku njema.
LikeLike
Chochote kikishafika Expire date hakina budi kuondolewa!
LikeLike
Nimekuelewa kocha hapa ni uzalishaji usiokuwa na ukomo
LikeLike
Ni muhimu kujiboresha kila Mara katika shughuri zetu ili kujiepusha na hali ya kutokua na matumizi na kujiepusha na hali ya ke expire.
LikeLike
Leo kuna comment nyingi!!!!!
LikeLike
Asante kocha,nitafanya maamuzi sahihi sio kukumbatia kitu chenye kureta asara.
LikeLike
Makampuni makubwa yanatunia dhana hii vizuri sana,mfano makampuni ya kutengeneza simu/ kutoa huduma.Kwa kutoa bidhaa mpya au huduma bora zaidi,
Yanakuwa na uhakika wa kumbakisha mteja kwenye matumizi wakati wote na hapoi. Na mini naenda kuitumia dhana hii kwenye kila eneo la shughuli zangu. 🙏🙏
LikeLike
Asante sana Kocha , kwa hakika nakaa kwenye mchakato kila siku ili niepuke shoga,panga na kisu. Najiboresha kila siku Ili siku za kuexpire kwangu kusifike mapema.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa ujumbe huu. Ni kweli tunachelewa sana kukubali matokeo hiyo inapelekea kushindwa Kusoma alama za nyakati
LikeLike
Kila kitu kina matumizi, wakati kina uzalishaji mzuri,
LikeLike
Matokeo ya nyuma hayatanizuia kufanya maamuzi sahihi,
LikeLike
Naepuka shoka Kwa kukaa kwenye mchakato, nawaondoa wote ambao muda wao umekwisha kwenye biashara au maisha yangu Kwa ujumla sitowangangania Tena.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Toa Thamani ama utakuwa umefika tarehe ya mwisho ya matumizi.
hapa njia ni moja tuu, kutoa THAMANI ZAIDI!
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala yenye uhalisia wa maisha kwa ujumla wake.
LikeLike