2951; Njia yangu au njia kuu.
Rafiki yangu mpendwa,
Zipo njia nyingi sana za kuweza kumfikisha mtu kwenye mafanikio anayoyataka.
Uwepo wa njia hizo nyingi ulipaswa uwe ni uhuru mkubwa kwa wengi, kwa kuwaonyesha wanaweza kupata wanachotaka.
Lakini badala yake njia hizo nyingi zimegeuka kuwa usumbufu mkubwa kwa wengi.
Kwani watu hawakai kwenye njia moja kwa muda wa kutosha kuwaletea matokeo wanayotaka.
Wanakaa kwenye njia moja kwa muda mfupi na pale wanapoona matokeo yanachelewa, wanahamia kwenye njia nyingine.
Huo umekuwa ndiyo mzunguko wa wengi kwenye maisha na kusababisha wasifanikiwe, siyo kwa sababu hawazijui njia, ila kwa sababu wamepotezwa na njia nyingi zilizopo.
Kuna mambo mawili makubwa ya kufanya kwenye hili;
Moja ni kuchagua njia yako ya mafanikio.
Katika njia nyingi zilizopo, chagua njia yako itakayokuwa kuu na ya msimamo kufika kwenye mafanikio makubwa.
Kaa kwenye njia hiyo bila kuyumbishwa na chochote.
Endelea kujifanya kuwa bora zaidi kadiri unavyokwenda.
Mbili ni watu unaojihusisha nao.
Unapaswa kuwazuia wasiwe watu wa kuhangaika na kila njia, kwani wataweza kukusumbua na hayo mahangaiko yao.
Ili usionekane unawalazimisha, wape njia mbili; watumie njia yako au watumie njia kuu.
Unajaribu kuwazuia watu unaojihusisha nao wasihangaike na njia nyingi na kupoteza nguvu na muda wao.
Unawataka wafuate njia yako ili muweze kushirikiana na kwenda vizuri pamoja.
Au unawataka watumie njia kuu, ambayo inaeleweka na ni ya uhakika.
Njia kuu ni ile ambayo ina ushahidi wa wengi kuitumia na wakaweza kupata matokeo bora kwa uhakika.
Usiwape nafasi ya kuhangaika na kila njia huku wakiwa hawazalishi matokeo unayoyataka.
Hii inahusisha wafanyakazi wako, washirika wako, wateja na wengine wote wanaojihusisha na wewe.
Kama kuna mtu unashirikiana naye na kila mara amekuwa anakuja na njia mpya ya kufanya mambo wakati njia za nyuma bado hazijaleta matokeo mazuri, mweleze njia mbili za kushirikiana na wewe, njia yako au njia kuu.
Watu wanapenda sana njia za mkato.
Lakini kiuhalisia, njia za mkato huwa ni ndefu kuliko njia zilizo sahihi.
Hivyo mtu anayeiacha njia sahihi kwa sababu ameona anachelewa, huyo anakwenda kujichelewesha zaidi.
Ili usicheleweshwe na uzembe wa watu kutokuelewa hiyo dhana ya njia sahihi na matokeo, watake watu wanaoshirikiana na wewe wafuate njia yako au njia kuu.
Hilo linawasaidia kuondokana na usumbufu wa njia nyingi.
Na pia inawafanya watu wakae kwenye njia moja kwa muda mrefu mpaka kupata matokeo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Njia ya mkato mara nyingi ndio inakuwa ndefu na yenye garama kubwa sana.
LikeLike
Asante sana kocha ni hakika nimejifunza kitu hapa
LikeLike
Ahsante kocha.
LikeLike
Nabaki njia kuu, Kwa msimamo,naacha kuhangaika na njia nyingi,nakomaa Hadi nipate matokeo.
LikeLike
Komaa hapo.
LikeLike
Asante Kocha; kitu cha muhimu ni mimi kufuata njia yangu au njia kuu. Njia zingine sitajihusisha nazo.
LikeLike
Nakaa kwenye njia yangu kuu itakayonifikisha kwenye mafanikio makubwa, Asante sana Kocha.
LikeLike
Asante kocha,kwa makala nitafanya kila njia kuwaelewesha ninaoshirikiana nao wafuate njia yangu au njia kuu.
LikeLike
Hakika!
It’s my way, or it’s highway.
LikeLike
Asante kocha
Nitajitahidi kukaa kwenye njia yangu na wanaojihusisha na mimi watatakiwa kukaa kwenye njia yangu au kukaa kwenye njia kuu kinyume na hapo ni kujichelewesha kufika nakotaka kwenda au kutokufika kabisa kwa kuhangaika na mambo mengi
LikeLike
Asante Kocha kwa kunijulisha njia yangu ama njia kuu
LikeLike
NJIA NI MBILI TU!
1. Njia yangu
2. Njia kuu
Wote ninaoshirikiana nao wanatakiwa wafuate njia yangu au njia kuu, kinyume Cha hapo ni kuhangaika na kupoteza na njiani.
LikeLike
Tusipoteze muda kwa mahangaiko ya njia zisizo na uhakika.
LikeLike
Hakika tupo kipindi ambapo Kuna njia nyingi za kutufikis
a ktk mafanikio tunayoyataka. Kwa hiyo, wale wanaoshili
Kiana nasi Wana machaguo mawili tu. 1. kufuata maeleke
zo yetu (mchakato) au wakafanye mamba Yao ,watuache
Sisi tunaendelea na mchakato wetu kwa msimamo na bila kuyumbiswa na chochote kile
Asante Sana kocha kwa makala ya leo
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante sana kocha kweli njia ya mkato ndio ndefu kuliko njia kuu
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ahsante sana Kocha
LikeLike
Asante sana Kocha, kama unavyo tufundisha katika dhana ya UKIBI , kujenga Mfumo, Team na Kukuza Mauzo kupitia kujenga wateja waamifu yatupaswa wote kufuata either njia yangu au njia kuu. Kwa upande wa kampuni yangu, njia itakuwa ni moja tu, ile inayoelezwa kupitia mfumo wetu wa uendeshaji kampuni yetu. Asante sana Kocha 🙏🏽
LikeLike
Asante sana Kocha, kama unavyo tufundisha katika dhana ya UKIBI , kujenga Mfumo, Team na Kukuza Mauzo kupitia kujenga wateja waamifu yatupaswa wote kufuata either njia yangu au njia kuu. Kwa upande wa kampuni yangu, njia itakuwa ni moja tu, ile inayoelezwa kupitia mfumo wetu wa uendeshaji kampuni yetu. 🙏🏽
LikeLike
Sure sure
Nitachagua njia yangu ya mafanikio. Njia ambayo itakuwa kuu na nitaifanya kwa msimamo na kuendelea kuifanya kwa UBORA sana.
Asante sana kocha
LikeLike
Ni ukweli kabisa kocha bila kuchagua njia moja kuu tutajikuta kila siku tunaanza upya Miluzi mingi ndio inayompoteza mbwa.Mimi na wote ninaojihusisha nao hatuna budi kuchagua njia moja kuu na kuifuata bila kuacha ili kufikia mafanikio makubwa
LikeLike
Njia yako au njia kuu. Njia ya mkato Ina gharama kubwa na haina thamani…ni kubabaisha
LikeLike
Njia ya mkato ni ndefu ila siyo sahihi.Na njia ya mkato ndiyo inayopendwa.Njia sahihi inachelewa lakini kuna kufanikiwa na ndiyo njia kuu mimi kuifuata.
Asante kwa hili Dr Amani
LikeLike
Asante sana kocha haya ndio mambo tuliokuwa tunaangaika nayo muda mrefu na kushindwa Kupiga hatua tunakuwa tunaruka kama nyani kwenye matawi
Asante
LikeLike
Ahsante sana kocha kwa makala hii, ntajitahidi kukaa kwenye njia kuu badala ya kuhangaika na njia nyingi ambazo hazinifikishi kule niendako
LikeLike
Asante Kocha. Nitabaki na Amsha Uwezo kama njia yangu kuu ya kufikia mafanikio makubwa
LikeLike
Asante sana kocha, hakika kukaa kwenye njia moja kwa muda mrefu na kufanya mambo kwa ubunifu kunalipa kuliko kuhama hama njia
LikeLike
ni au njia yangu au njia kuu. hamna zaidi ya hapo
LikeLike
Katika njia nyingi zilizopo, chagua njia yako itakayokuwa kuu na ya msimamo kufika kwenye mafanikio makubwa.
Kaa kwenye njia hiyo bila kuyumbishwa na chochote.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo zuri ni muhimu sana kukaa kwenye njia moja hadi kufika ulipokusudia kufika. Kwani hakuna aliyewahi kutumia njia mbili hadi tatu kwa wakati mmoja na akafika popote.
LikeLike
Mara nyingine unaweza ukaona unafaidi kweli kakini ni kwa muda mfupi tu muda mwingi wanaofaidi kwa muda mrefu ni wale wanaofanya mambo yao bila kutumia njia ya mkato tufanye biashara kwa kunyooka kazi zetu kwa kunyooka
LikeLike
Njia ya mkato ni ndefu zaidi.
LikeLike