2970; Kosa la uzururaji.
Rafiki yangu mpendwa,
Kipindi nikiwa mdogo, nilikuwa nashangaa sana pale niliposikia kuna watu wamekamatwa na posili kwa kosa la uzururaji.
Nilikuwa nashangaa mtu mzima anazururaje.
Maana nilizoea unapoambiwa acha kuzurura, maana yake ni uache kwenda kila mahali na kutulia sehemu moja.
Baadaye nilikuja kujifunza kwamba kumbe uzururaji siyo tu kuzunguka kila mahali, bali hata kuwa eneo ambalo hukupaswa kuwa ni uzururaji.
Kwa mfano kama umekubwa upo baa wakati ambao ni wa kazi, hapo unazurura.
Ni kupitia maana hiyo ya uzururaji nimekuwa natafakari jinsi watu wengi kwenye maisha wanavyozurura.
Kwa maana ya uzururaji kwamba ni kuwa eneo ambalo hukupaswa kuwa, watu wengi sana wanazurura kwenye maisha yao.
Na kiashiria kikubwa kinachounga mkono hilo ni jinsi ambavyo watu wengi wanashindwa kupata mafanikio licha ya kuonekana ni wachapakazi saba.
Kwa nje tunaweza kuona mtu anajituma sana.
Lakini ni kwa ndani ndiyo tunaweza kuona kama anajituma kweli au anazurura tu.
Kama hulijui kusudi la maisha yako, kama huna ndoto kubwa unazozipigania, kama huna malengo na mipango unayojisukuma nayo, sehemu kubwa ya unayofanya yanakuwa ni uzururaji, maana hakuna yanakokupeleka.
Watu wengi kwa zama hizi wanaweza wasikamatwe kwa kosa la uzururaji, kwa sababu wanakuwa wanaonekana kama vile kuna kitu wanafanya na mahali wanaenda.
Lakini uhalisia ni wanajiendea tu, hawajui hata wapi wanaenda.
Dalili nzuri ya mtu mzururaji ni mambo mapya anauojihusisha nayo kila wakati.
Kila wakati kuna fursa mpya na inayolipa sana anayokuwa anazungumzia.
Kuwa mtu wa kukimbizana nafursa mpya kila wakati siyo sifa nzuri, bali ni kiashiria hakuna chochote kimoja ambacho umejitoa kweli kuhakikisha umekipata.
Kwa upande mmoja tunaita uzururaji ni kuhangaika na vitu vingi badala ya kuweka juhudi zako zote kwenye vitu vichache na vyenye tija.
Kwa upande wa pili, uzururaji ni kuwa sehemu ambayo hukupaswa kuwa.
Katika hali hiyo, unakutana na mambo ambayo hukuwa umepanga kukutana nayo, kitu kinachoweza kuwa usumbufu au kikwazo kwako.
Kwa mfano umeibiwa au kutapeliwa, hapo tatizo siyo wizi wala utapeli, bali tatizo ni wewe.
Ni wewe mwenyewe umejiweka kwenye hali ya kuibiwa na kutapeliwa kirahisi.
Nina imani kwamba kama ungekuwa umeweka umakini wako kwenye vitu sahihi kwako, usingepata nafasi ya kutapeliwa.
Kuzurura kwako ndiyo kumekuweka kwenye hatari ya kuibiwa na kutapeliwa.
Kadhalika, kama kuna watu wamekufanyia namna ambavyo hukuridhika, kosa linarudi kwako, uzururaji.
Ni wewe umejipeleka kwa watu au hali ambazo hazina heshima ya kutosha kwako.
Kama ungekuwa unajua kwa hakika kile unachotaka na kujitoa kukipata, ungepunguza mno kutendewa isivyo sahihi.
Sehemu kubwa ya watu tunaopishana nao kila siku wanaweza kuonekana kama kuna mahali wanaenda.
Lakini kwa hakika wengi ni wazururaji tu.
Nikupe mfano mzuri, pita barabarani na ukute kuna ajali imetokea. Utashangaa jinsi ambavyo utakuta watu wengi wamezingira eneo hilo na wanakaa hapo muda mrefu. Hata wale wanaopita wakiendesha magari, wanapunguza mwendo kuangalia nini kinachoendelea, kitu kinachopelekea foleni kubwa kubwa zaidi.
Wote hao hawana mahali pa muhimu wanaenda, wanazurura tu na maisha yao.
Maana naamini kama mtu kuna mkutano wa muhimu sana anaowahi na muda umekwenda, hatapoteza muda kuangalia nini kinaendelea, badala yake ataendelea na kasi yake ya kuwahi kule anaenda. Anajua kama kuna taarifa zozote muhimu anapaswa kuzijua, atazisikia kwa wengine.
Hapo hatujagusa wale wanaoamka na kujikuta wamevaa ajenda ya siku kwenye habari zinazoendelea.
Na wale wanaoshinda kwenye mitandao ya kijamii.
Na wanaobishana na kufuatilia mambo ya burudani zaidi.
Yote hayo ni uzururaji, kiashiria kwamba mtu hajui anakokwenda hivyo inakuwa rahisi kuchukua njia yoyote inayojitokeza mbele yake.
Ili kuondokana na uzururaji, kujua kwa hakika kile unachotaka na kukipambania muda wote ni muhimu.
Pale unachotaka kinapokuwa kikubwa na kukutaka wewe ujitoe sana ili kukipata, hupati kabisa nafasi ya kuzurura.
Muda wote unakuwa umetingwa na hicho unachotaka.
Hatua ya kwanza ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha ni kuacha kuzurura.
Hilo ni kosa ambalo lina adhabu kubwa ya kukunyima mafanikio bila ya wewe kujua.
Weka umakini wako wote kwenye vitu vichache muhimu na utaweza kufanya makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha. Kweli kuzurura sio kuzuri
LikeLike
Tunapoteza muda na nguvu nyingi huku hakuna matokeo tunayopata.
Tuache kuzurura.
LikeLike
Hatua ya kwanza ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha ni kuacha kuzurura.
Hilo ni kosa ambalo lina adhabu kubwa ya kukunyima mafanikio bila ya wewe kujua.
LikeLike
Hakika ujumbe huu ni sahihi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakika ujumbe huu ni sahihi na kweli kabisa.
LikeLike
Kuzurura inaweza kuonekana raha kwa wakati, lakini adhabu yake ni kukosa mafanikio makubwa.
Tuache kuzurura.
LikeLike
Kama hujui kile unachotaka kwenye maisha yako huo pia ni uzururaji.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Utajikuta unahangaika na mengi sana na hakuna hatua unayopiga, na huo ndiyo uzururaji wenyewe.
LikeLike
asante sana hii inanishangaza sana kila siku huwa napita mahali kuna watu kila siku mwaka mzima ahsubuh wapo kijiwe fulani asubuh na ni watu wazima,mchana ukipita bado wapo pale pale na kucheza karata au draft.
Akili za kamari,betting,na ushabiki wa mpirq na kujua kila ratiba ya mpira ligi za nje na ndani
LikeLike
Uzururaji wa kiwango cha juu sana huu.
Halafu watu hao hao utawakuta wakilaumu serikali kwa maisha yao magumu.
LikeLike
Naacha uzururaji hasa wa fb, Asante Kocha.
LikeLike
delete hiyo kitu kabisa Maureen
LikeLike
Humo kwenye mitandao ndiyo kuna uzururaji mkubwa sana.
Tujiepushe nayo kama haina manufaa ya moja kwa moja kibiashara.
LikeLike
Hakika kwa mifano hii kwa kweli wengi sana ni wazurulaji wakubwa kwenye maisha yao hata mimi kuna wakati mwingi national nilikuwa mzurulaji kwenye maisha yangu na huku nikisongwa na mambo ya siku hiyo bila kuangalia vipaumbele vyangu vikubwa.
LikeLike
Uzururaji huwezi kuugundua kwa haraka, unaweza kuona ndiyo maisha ya kawaida, kumbe unazurura.
Tuepuke sana uzururaji.
LikeLike
Daah
LikeLike
Umeona eh!
LikeLike
Uzururaji ni kuyapoteza maisha yako.
LikeLike
Kabisa yani.
Na wengi wanakuja kushtuka wameshapotea sana.
LikeLike
Kumbe hata ukiingia mtandaoni bila muda uliopanga kuingia kufika ni mzururaji leo nimepata kitu kipya kwangu
LikeLike
Tena ni uzururaji mkubwa sana huo.
Na wengi hawajui, hivyo wanapoteza muda mwingi sana.
LikeLike
Asante kocha,ili nipate mafanikio inabidi nijikite kwenye kazi sio kuzurura.
LikeLike
Uzururaji haujawahi kuwa na manufaa.
LikeLike
Asante kocha kwa hili.Nitaacha uzurulaji ili kupata mafanikio makubwa ninayoyataka.
LikeLike
Uzururaji ni sumu kubwa.
LikeLike
Tunapoteza muda mwingi kwa kuwa na ururaji wa hovyohovyo,asante Sana kocha kwa somo hili juu ya ururaji.
LikeLike
Tuache kuzurura.
LikeLike
Ila kuzurura kuna raha yake.
LikeLike
😂😂
Na chochote chenye raha huwa hakiishii pazuri.
LikeLike
Kumbe Kuna aina nyingi za uzurirajo na kama hatufanyi mambo makubwa nanayotishia maisha yetu tutakuwa wazuriraji
LikeLike
Kabisa,
Kwa sababu tayari uwezo wa kufanya makubwa unao, halafu huutumii kufanya makubwa. Hapo kuna nini kama siyo uzururaji?
LikeLike
Uzururaji ni pale ambapo:-
Hulijui kusudi la maisha yako
Huna ndoto kubwa unazopigania
Huna malengo na mipango unayojisukuma nayo
Ukiwa na ndoto kubwa ya kukutaka wewe ujitoe sana ili kuipambania ndoto yako basi hutapata kabisa nafasi ya kuzurura!!!
LikeLike
Huna vyote hivyo, halafu kila siku uko bize kweli kweli.
Haishangazi kwa nini watu wanaonekana kufanya kazi sana, lakini hakuna hatua wanazopiga, kwa sababu wanazurura.
LikeLike
Yeyoye anaezurura hajajua kusudi lake la kuwepo hapa dunianii pamoja na kuwa na lengo kubwa
Asante sana
LikeLike
Na bado watu hawajui hayo ila wapo bize. Kuzurura kuna gharama kubwa.
LikeLike
Kwa maana hiyo kweli wazururaji ni wengi.
LikeLike
Kuacha kuzurula kwa dhati bila kutoka hata maramoja. Ijaze ratiba yako na yaliyo muhimu kwako na vipaumbele kuhakikisha hakuna utupu maana Dunia au asili imejaa utele haipendi utupu.
LikeLike
Asili haipendi kabisa utupu,
Ukiwa na gape tu kwenye muda wako wa siku, unajikuta ukizurura.
LikeLike
Naweka umakini wangu kwenye vitu vichache vitakavyonipa mafanikio makubwa, naacha kuzurura Kwa kukimbilia fursa mpya naweka umakini na kuwa busy na ninachokifanya Hadi nikose muda Wa kufuatilia yasiyonihusu.
LikeLike
Kuwa bize sana na yale yaliyo muhimu ili usipate muda wa kuzurura.
LikeLike
Naweka kazi kwenye biashara yangu nifanikiwe, hakuna kingine muhimu Kwa Sasa.
LikeLike
Tekeleza hilo,
Kazi haijawahi kumtupa mtu.
LikeLike
Nitaacha kuzurura na kufanye kile ambacho natakiwa kufanya katika siku husika.
LikeLike
Vizuri, panga kisha fanya kama ulivyopanga.
LikeLike
nachagua mambo machache na kuweka juhudi zote ili kutojinyimaa mafanikio makubwa ..shukrani kocha
LikeLike
Muda na nguvu ni rasilimali zenye uhaba.
Tuzitumie vyema ili kufanya makubwa.
LikeLike
Kukosa vipaumbele ni uzururaji pia.
LikeLike
Kabisa, maana utafanya mengi ambayo hayakupaswa kufanywa kabisa.
LikeLike
Mara zote nakuwa bize na kazi zangu. Ziruri sehemu nyingine zaidi ya kwenye biashara yangu tu
LikeLike
Kukaa kwenye biashara zetu kwa uhakika inatosha kutochosha kiasi cha kushindwa kupata muda wa kuzurura.
Hivyo kama mtu unapata muda wa kuzurura, kuna namna unakuwa hujakaa kwenye biashara yako kwa uhakika.
LikeLike
Nimechagua kuacha kuzurura maana uzururaji hautaniletea matokeo makubwa nayotaka kwenye maisha yangu
LikeLike
Vizuri, uzururaji ni dhambi kubwa.
LikeLike