2975; Huu ndiyo ushindi.
Rafiki yangu mpendwa,
Wote tulio hapa tuna lengo kubwa moja ambalo ni kufikia ubilionea.
Hilo ndiyo lengo kuu ambalo kila mmoja wetu analipambania.
Ni lengo ambalo tunaamini bila ya shaka yoyote kwamba tutakifikia.
Kwa sababu tupo tayari kulipambania bila ya kuchoka wala kukata tamaa.
Katika kufikia lengo hilo la ubilionea, kuna sehemu kuu mbili.
Sehemu ya kwanza ni juhudi ambazo tunaweka. Hii ni zile hatua tunazochukua ili kulifikia lengo.
Na sehemu ya pili ni matokeo yenyewe. Hapo ndipo kufikia lengo husika.
Katika sehemu hizo mbili, sehemu ya kwanza ipo ndani ya udhibiti wetu kwa asilimia 100. Tunaweza kuifanyia kazi kwa uhakika bila kushindwa kwa namna yoyote ile.
Lakini sehemu ya pili haipo ndani ya udhibiti wetu kwa asilimia 100. Ni zao la sehemu ya kwanza, ambalo hatuwezi kupangilia utokeaji wake.
Kitu kimoja tunachojua ni kwamba kama tutatekeleza sehemu ya kwanza kwa uhakika mkubwa, tunakuwa tumeathiri sana sehemu ya pili.
Kwa kukamilisha sehemu ya kwanza kwa asilimia 100 bila kushindwa, kuna nguvu kubwa ya kusababisha sehemu ya pili nayo ikamilike.
Sasa basi, watu wengi hupima ushindi kwa matokeo, kwa ukamilikaji wa sehemu ya pili.
Kwenye kipindi chote wanachokuwa wanafanyia kazi sehemu ya kwanza hawahesabu ushindi.
Ni mpaka pale wanapopata matokeo wanayotarajia ndiyo wanahesabu ushindi.
Hiyo siyo sahihi na ndiyo kimekuwa chanzo cha wengi kukata tamaa, hasa wanapokutana na magumu na changamoto.
Kadiri lengo na matokeo yanayotarajiwa yanavyokuwa makubwa, ndivyo muda mrefu zaidi unavyohitajika ili kufikia.
Sasa mtu anaposubiria ushindi kwenye matokeo, inakuwa rahisi kukata tamaa.
Ushindi sahihi wa kupima ni kwenye kukamilisha sehemu ya kwanza, yaani kuchukua hatua unaopaswa kuchukua.
Hii ndiyo tunayoita kukaa kwenye mchakato kwenye safari yetu ya ubilionea.
Kukaa kwenye mchakato, kwa asilimia 100 bila kuyumba ndiyo ushindi mkubwa sana kwetu.
Hiyo ni kwa sababu ndiyo kitu tunachoweza kukiathiri, lakini pia ndiyo chenye mchango kwenye matokeo tunayotaka kupata.
Kukaa kwenye mchakato ndiyo ushindi mkuu kwa sababu tungeweza tusikae.
Tungeweza kutoa sababu na visingizio mbalimbali kwa nini tumeshindwa kukaa kwenye mchakato.
Lakini pale tunapojisukuma kwa kila namna na kukamilisha kukaa kwenye mchakato tunakuwa tumepata ushindi mkubwa sana.
Ni kwa kuendelea kukaa kwenye mchakato kwa ushindi mara zote ndipo penye nguvu ya kupata kile tunachotaka.
Na huu ni ushindi mkubwa kwa sababu japo mchakato upo wazi kwa wote, siyo wengi wanaoweza kuukamilisha.
Wengi ni wavivu, wazembe na wajinga ambao hawataki kujisumbua kwa namna yoyote ile.
Wewe kuwa tu tayari kujisumbua kwa kukaa kwenye mchakato kwa asilimia 100 ni ushindi mkubwa bila kujali matokeo gani umepata.
Ili uweze kukaa kwenye mchakato kwa asilimia 100, lazima ujikubali na ukikubali sana kile unachofanya.
Lazima uuamini na kuupenda mchakato mzima.
Na lazima uwe na maono ambayo mchakato ndiyo njia sahihi ya kuyafikia.
Halafu wewe unapambana na mchakato wako, ukijua huo ndiyo ushindi mkubwa kwako.
Matokeo ya mwisho ni kitu cha ziada, ambacho kitakuwa kizuri kulingana na ukaaji wako kwenye mchakato.
Kukaa kwenye mchakato kwa asilimia 100 mara zote ndiyo ushindi mkubwa kwako.
Ndiyo kitu unachoweza kukiathiri moja kwa moja.
Na ndiyo kitu chenye nguvu ya kuathiri matokeo ya mwisho unayoyataka.
Usisumbuke sana na hayo matokeo ya mwisho, wewe sumbuka na kukusanya ushindi wako wa kila siku kwa kukaa kwenye mchakato kwa asilimia 100.
Hakuna namna unaweza kushindwa kama utafuata huu mwongozo kwa uhakika.
Ushindi ni kwako, labda tu uamue kushindwa wewe mwenyewe.
Maana hakuna chochote unachoweza kukisingizia kwa kushindwa kukaa kwenye mchakato.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Na kaa kwenye mchakato .
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kocha nitaendelea kukaa kwenye mchakato kikamilifu bila kuyumba
LikeLike
Vizuri, kaa kwenye mchakato kwa msimamo bila kuyumba.
LikeLike
Asante kocha,kitu muhimu sana ni kukaa kwenye mchakato,haijarishi ni matokeo gani umepata ila nidhamu ndo muhimu ili uweze kupata matokeo mazuri.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Sitaruhusu mambo haya matatu yaani Uvivu, Uzembe na Ujinga viwe chanzo cha mimi kushindwa kukaa kwenye mchakato.
Asante sana Kocha Dr. Makirita Amani
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha somo hili limenifanya nisimame kwenye kiti mara moja asante sana barikiwa sana
LikeLike
Vizuri sana, chukua hatua.
LikeLike
Nakaa kwenye mchakato wa ubilionea huo ndio ushind Wang
LikeLike
Hongera kwa ushindi.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato ndio kiashiria kikubwa cha Ushindi kwenye safari yoyote ile
LikeLike
Hakika, tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Asante sana Kocha. Kweli kukaa kwenye mchakato hakuna mbadala
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Ahsante sana Kocha kwa makala ya leo
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Hii kwa hakika ni sheria ya asili kocha hakuna matokeo bila kisababishi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato mara zote kwa aslimia 100. Ndio njia ya ushindi kuelekea malengo tuliyojiwekea
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Sisumbukii matokeo ya mwisho, ninakusanya ushindi wangu kila siku kwa kukaa kwenye mchakato kwa IOO%.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ushindi uko kwenye kukaa kwenye mchakato. Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Ushindi Wa kukaa kwenye mchakato ndio lengo namba moja, kukaa kwenye mchakato ipo ndani ya uwezo wangu Kwa asilimilia 100.
Nakaa kwenye mchakato bila kuyumba
LikeLike
Kaa kwenye mchakato, ipo ndani ya uwezo wako.
LikeLike
Asante sana Kocha, siyakubali kuwa mvivu, mzembe na mjinga, nitaendelea kushinda kupitia mchakato mpaka matokeo yajipendekeze yenyewe.
LikeLike
Kaa kwenye mchakato.
LikeLike
Nimechagua kukaa kwenye mchakato bila kujali ninalata matokeo gani bila kuyumbishwa na chochote kile
LikeLike
Kaa kwenye mchakato.
LikeLike
Kukaaa kwenye mchakato kwa asilimia 100,na kuona ushindi kila siku kwenye hatua za mchakato bila kuyumbishwa na matokeo
LikeLike
Kaa kwenye mchakato.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato matokeo yatakuja yenyewe
Asante
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nachagua kukaa kwenye mchakato Kwa asilimia 100. Asante sana Coach.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ahsante sana kocha nitakaa kwenye mchakato kwa asilimia 100
LikeLike
Kaa kwenye mchakato.
LikeLike
Hakuna njia nyingine zaidi ya kukaa kwenye mchakato kwa 100%
LikeLike
Kaa kwenye mchakato.
LikeLike
Ushindi wangu ni kukaa kwenye mchakato kila siku kwa 100% maana ndiyo kitu ninachoweza kukiathiri.
LikeLike
Kaa kwenye mchakato
LikeLike
Ushindi Upo kwenye kukaa kwenye mchakato. Nitakaa kwenye mchakato mara zote maana hii ndio ipo kwenye uwezo wangu.
LikeLike
Kaa kwenye mchakato
LikeLike
Hakuna namna unaweza kushindwa kama utafuata huu mwongozo kwa uhakika.
LikeLike
Hakika
LikeLike
kukaa kwenye mchakato ipo ndani ya uwezo wangu ,
matokea yatakuja yenyewe nikizingatia kanuni ya kwanza.
shukrani kocha.
LikeLike
Kaa kwenye mchakato.
LikeLike
100%
LikeLike
Nitaweka juhudi kubwa kuhakikisha nabaki kwenye mchakato,Sitajali kuhusu matokeo…
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato 100%
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato kwa asilimia 100 mara zote ndiyo ushindi mkubwa kwangu.
Ndiyo kitu ninachoweza kukiathiri moja kwa moja.
Na ndiyo kitu chenye nguvu ya kuathiri matokeo ya mwisho ninayoyataka.
Ahsante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
Najisukuma kukaa kwenye mchakato kwa 100%
LikeLike
Kumbe basi ushindi wa jambo lolote ni kukaa kwenye mchakato bila kujali chochote na matokeo yatakuja
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato kwa msimamo ni ushindi mkubwa.
LikeLike