2987; Hatua tano za kutatua tatizo lolote.
Rafiki yangu mpendwa,
Matatizo ni sehemu ya maisha.
Kadiri ndoto zako zinavyokuwa kubwa, ndivyo pia matatizo unayokutana nayo yanavyokuwa makubwa.
Hapa tunakwenda kujifunza hatua tano za uhakika za kutatua tatizo lolote lile.
Hatua ya kwanza ni kulijua tatizo.
Ipo kauli inayosema kulijua tatizo ni nusu ya kulitatua.
Kwa kujua tu kwamba kuna tatizo, unakuwa hatua ya mbele zaidi maana wengi hukataa uwepo wa tatizo.
Tatizo ni pale matokeo yanapokuwa tofauti na matarajio.
Hivyo kulijua tatizo ni kuanza na kujiuliza ni matokeo gani uliyoyataka na yapi ambayo umeyapata.
Kumbuka matokeo halisi yanapokuwa tofauti na matarajio yaliyokuwepo, kuna tatizo.
Hatua ya pili ni kujua chanzo au kisababishi cha tatizo.
Kila kitu kwenye maisha kinasababishwa.
Na kwa bahati mbaya au nzuri, matatizo yote kwenye maisha yetu yanasababishwa na watu, iwe ni sisi wenyewe au wengine.
Kujua chanzo au sababu ya tatizo unapaswa kujiuliza ni kitu gani watu wanafanya au hawafanyi na kupelekea tatizo kutokea.
Ni hivyo tu, tatizo litatokana na vitu ambavyo watu wanafanya au kushindwa kufanya. Ukichunguza hayo mawili utaweza kujua chanzo halisi kwa kila tatizo.
Hatua ya tatu ni kujua nini cha kufanya ili kutatua tatizo.
Baada ya kujua chanzo au kisababishi cha tatizo, kinachofuata ni utatuzi wa tatizo.
Kwenye kutatua tatizo, unapaswa kujiuliza nini cha kufanya ili kupata matokeo unayotarajia.
Umeshajua nini watu wanafanya au hawafanyi hivyo kusababisha tatizo.
Hivyo hatua ya utatuzi siyo ngumu, ni kufanya watu waache kufanya vitu fulani au waanze kufanya vitu fulani ili kuondokana na tatizo husika.
Hatua ya nne ni kupima usahihi wa suluhisho ulilochagua.
Kwa haraka unaweza kuwa umepata suluhisho la tatizo, lakini kabla hujalifanyia kazi unapaswa kujiuliza kama kwa kufanya hicho ulichopanga kufanya utapata matokeo unayotaka kufanya.
Kama jibu ni ndiyo basi unaendelea kufanya.
Kama jibu ni hapana unajiuliza kwa nini, kisha kuja na mapendekezo mengine.
Utaendelea kujiuliza swali hilo kwa kila pendekezo mpaka upate lile ambalo ni sahihi kabisa, linalokupa matokeo unayotaka kupata.
Hatua ya tano ni kufanyia kazi suluhisho ulilopata.
Katika kufanyia kazi unayapima matokeo na kulinganisha na matarajio.
Kama matokeo yanaendana na matarajio basi umeweza kulitatua tatizo.
Kama matokeo yanatofautiana na matarajio bado una tatizo.
Na kama bado una tatizo, rudi kwenye hatua ya kwanza na rudia mchakato mzima.
Kwa kufuata natua hizi nne kwa uhakika, utaweza kutatua kila tatizo ulilonalo.
Na kama kwa hatua hizi nne unashindwa kutatua tatizo lolote lile basi huenda hujalijua tatizo au ulilonalo siyo tatizo bali hali unayopaswa kuishi nayo.
Kama unataka kufanikiwa kwenye maisha, hupaswi kuyakimbia matatizo, bali unapaswa kuyakabili.
Yakabili matatizo uliyonayo na utakuwa imara na kuweza kufikia malengo makubwa uliyonayo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha Nimekuelewa vyema sana
LikeLike
Asante Kocha, kwa vyovyote vile matatizo mengi husabaishwa na sisi au watu wengine. Hapa nimeelewa vyema
LikeLike
Matatizo yanasababishwa na watu kufanya au kutokufanya kitu fulani.
LikeLike
Kadiri ndoto zako zinavyokuwa kubwa, ndivyo pia matatizo unayokutana nayo yanavyokuwa makubwa.
LikeLike
Asante kocha kwa makala ya leo
Napaswa kuyakabidhi matatizo niliyo nayo ili niwe imara zaidi na sipaswi kuyakimbia matatizo mana matatizo siwezi kuyakimbia.
LikeLike
Hakika ni hatua tano muhimu za kukabiliana na kila tatizo. Asante sana Kocha.
LikeLike
Ahsante sana kocha nitazifuata hatua hizi kutatua matatizo kila ninapokutana nayo
LikeLike
Ni muhimu kweli kuchukua hatua katika kutatua tatizo lolote lile tunashukuru kwa hatua hizi zitatusaidia kuwa mwongozo pale unapokutana na tatizo.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza kwa kukaa kwenye mchakato wa hizi hatua za kutatua tatizo na bado usipate ufumbuzi, basi hiyo ni hali ambayo unapaswa kuishi nayo.
LikeLike
Asante sana Kwa hatua hizi muhimu
LikeLike
Hatua 5
1. Kuliyanbua tatizo lililopo
2. Kujua chanzo Cha ttzo Hilo
3. Hatua za kulitatu
4. Kupima uwezo wa utatuzi
5. Bado lipo au halipo
LikeLike
Nimezisoma na kuzielewa hatua zote tano za kutatua tatizo. Nimefurahi Sana, ninakili ,nilikuwa sizijui kabisaa Asante Sana kocha.
LikeLike
👉kwanza kujua tatizo
👉Kujua chanzo au kisababishi cha tatizo
👉Kujua cha kufanya ili kutatua tatizo
👉Kupima usahihi wa suluhisho ulichaguliwa
👉Kufanyia kazi suluhisho ulilopata
Shukrani kocha nitazingatia haya ili Kufanya kwa bora.
LikeLike
Asante kocha kwa hatua hizi Tano muhimu
LikeLike
Huwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo chake.
LikeLike
Kama unataka kufanikiwa huna budi kuyakabili matatizo,matatizo ndio kipimo chetu Cha hatua tunzopitia
LikeLike
Asante sana kwa hatua hizi.Umechambua vyema.Matatizo yapo kila siku hayaishi na hatuwezinkuyakimbia,huu ni muongozo sahihi kutatua matatizo
LikeLike
Asante Sana kocha. Kweli kabisa kocha, kwa hatua hizi tano Tatizo lolote linatatulika.
LikeLike
Mafanikio ni kutatua changamoto tulizonazo, asante sana.
LikeLike
Nitatatua matatizo yote yanayonikabili ili niweze kufikia ndoto zangu.
LikeLike
Sitakimbia matatizo yangu Bali nitayakabili.
LikeLike
Ni mimi au watu wengine ndio chanzo.
LikeLike
Kwa kuwa nataka kufanikiwa kwenye maisha natakiwa kuyakabili matatizo.
LikeLike
Asante Kocha kwa recepi ya utatuzi wa matatizo
LikeLike
Nayakabili matatizo niliyonayo Ili kuweza kwenda mbali.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha kwa Makala KUNTU.
Nimejifunza kuwa sitakiwi kulikimbia tatizo bali kuangalia namna ya kulitatua, After all MATATIZO NI SEHEMU YA MAISHA NA NI BANDIKA BANDUA.
Nitatumia njia hizi tano katika kulikabili tatizo lolote.
1. kutambua uwepo wa tatizo
2. Kujua klichosababisha tatizo
3. Kujua nini cha kufanya ili kutatua tatizo
4. Kupima usahihi wa suluhisho ulilolichagua
5, Kuchukuwa hatua ili kulitatua tatizo.
Ikishindikana basi jibu la tatizo langu ni moja kati ya yafuatayo:-
1. SIJALIJUA TATIZO BADO
2. NI HALI AMBAYO NINAPASWA KUISHI NAYO. (hahahahahahha)
Asante sana KOCHA, Nimekuelewa kwa kweli,,,
LikeLike
Vizuri sana, tufuate kanuni hii rahisi ili kuyatatua matatizo tunayokabiliana nayo.
LikeLike
Hii ni njia nzuri kwakweli kocha naamini ningekua natumia ningekua bora sana nashukuru sana kocha ntaitumia kuwa bora
LikeLike
Vizuri Dickson, itumie.
LikeLike