2992; Ukomo wa watu wengine.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi hawafanikiwi kwenye maisha yao kwa sababu wana ukomo ambao wamejiwekea kwenye fikra zao.
Wanakuwa wamefunga fikra zao kwa nini kinachowezekana na nini hakiwezekani.
Wanapokuona wewe ukiwa na fikra za kufanya makubwa, wanakuambia haiwezekani.
Kukuambia kwao haiwezekani, siyo kwamba haiwezekani kweli, bali huo ndiyo ukomo uliopo kwenye fikra zao.
Hakuna wa kuweza kukuambia wewe nini kinawezekana na nini hakiwezekani.
Hiyo ni kwa sababu hakuna mwenye maono kama uliyonayo wewe wala msukumo ulionao.
Watu wote walioweza kufanya makubwa hapa duniani, walipitia kupingwa na kukatishwa tamaa.
Wengine walionekana huenda wana matatizo ya akili.
Lakini kwa kuamini kwenye kile walichotaka sana na kung’ang’ana nacho, leo dunia inanufaika sana kupitia wao.
Unachukuliaje pale watu wanapokuambia ndoto kubwa ulizonazo haziwezekani?
Unachukuliaje pale wewe peke yako ndiye unayefanya kinyume na kundi kubwa la watu wanaokuzunguka?
Sisi binadamu ni rahisi kufuata mkumbo, lakini mafanikio makubwa hayajawahi kutokea kwenye mkumbo.
Ni lazima uweze kusimama mwenyewe, usimamie picha unayoiona kwenye fikra zako, utumie msukumo mkubwa ulio ndani yako.
Mafanikio makubwa yapo kwa wachache kwa sababu wao ndiyo wanaoweza kuvumilia upweke wa kusimama wenyewe, wanaoweza kupuuza kupingwa na kukatishwa tamaa na wengine.
Je wewe umejitoa kiasi gani kuhakikisha kweli unazifikia ndoto kubwa ulizonazo?
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Sitafuata mkunbo nitasimamia kile nilichokipamga hata kama kundi kubwa la watu linasema haiwezekani
LikeLike
👍
LikeLike
nitavumilia upweke wangu wa kusimama mwenyewe mpaka nifanikiwe.
ahsante
LikeLike
👍
LikeLike
Hakuna biashara inayoweza kukua kwa kufuata mkumbo hivyo ntasimamia vyema biashara ysngu kwa kuishi kwa mfumo.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
kweli kabisa kocha natakiwa kusimamia kile ninachoamini mimi maana mwingine anaweza kuona tofauti na
mimi na wengine wakaona kama hauna akili sawasawa kumbe ni mitazamo na fikira.
asante kocha kunujulisha ili na kuchukua hatua zng.
LikeLike
Hakuna anayeona unachoona, hivyo wasipokuelewa ni poa tu.
LikeLike
Dunia inanufaika kutokana na imani na ung’ang’anizi wa watu wachache kwa kile cha manufaa walichoamua kukifanya.
LikeLike
Vikundi vya watu wachache waliojitoa kweli ndiyo vimekuwa vinaibadili dunia.
LikeLike
Wengine hawaoni kile unachokiona wewe.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Sisi binadamu ni rahisi kufuata mkumbo, lakini mafanikio makubwa hayajawahi kutokea kwenye mkumbo.
LikeLike
Kufuata mkumbo ni kuambatana na watu wasiojua wanakokwenda.
LikeLike
Kile kilichopo ndani yangu hakuna anayeweza kukiona kama ninavyoona hivyo kwangu hakuna lisilowezekana nikiamini na kukaa kwenye mchakato
NIMEJIOA KWELI KUKAA KWENY MCHAKATO
NAUPENDA MCHAKATO
MIMI NI MWAMINIFU KWA KOCHA NA KLABU YANGU YA DEWJI
LikeLike
Safi sana,
Tusiyumbishwe na wasiojua wapi tunataka kufika.
LikeLike
Mafanikio makubwa hayajawahi kutokea kwenye mkumbo. Ahsante sana Kocha
Dr.Amani Makirita
LikeLike
Tuepuke mkumbo.
LikeLike
Hakika hakuna mtu anayeweza kunizuia kupata kile ninachokita. Naamini itawezekana.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Sitafuata mkumbo nitasimama mwenyewe kwenye kuzifikia ndoto zangu hata kama dunia itakuwa tofauti na mimi.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Wote wote walioweza kufanya makubwa hapa duniani walipata kupingwa na kukatishwa tamaa,nashkr kuyajua haya ili niendelee kupambana.
LikeLike
Ukitaka ukubalike na kila mtu utashindwa.
LikeLike
Kufuata mkumbo, kusimamia maono na kujisukuma Kuyafikia ndiyo mpango mzima hapa.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nitasimama mwenyewe,nitaushinda upweke na kupigania ndoto kubwa nilizonazo!
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitavumilia upweke, nitakaa kwenye mchakato kuhakikisha napata kile nachotaka kwenye maisha yangu.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mafanikio makubwa yanataka ujitoe hasa kwenye jamii inayotuzunguka ambayo ni jamii hasi,bila kijitofautisha na kujitoa sana hutapata mafanikio
Asante
LikeLike
Lazima uwe tayari kusimama mwenyewe mpaka tone la mwisho.
LikeLike
Kweli kabisa Kocha mafanikio makubwa sio kwa mkumbo, bali ni mimi binafsi kukaa kwenye mchakato wa BM na Chuo cha Mauzo kwa msimamo bila kuacha na kuzingatia kufanya kwa vitendo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana Kocha mafanikio makubwa sio kwa mkumbo, bali ni mimi binafsi kukaa kwenye mchakato wa BM na Chuo cha Mauzo kwa msimamo bila kuacha na kuzingatia kufanya kwa vitendo.
LikeLike
nitasimamia ndoto zangu kwq kua wao hawaoni ninachokiona na hawajui nakotaka kufika.Nitasimama hili
LikeLike
Hakuna anayeona kile unachoona.
LikeLike
MAFANIKIO huwa ni vigumu kuyafikia . Watu walioweza kufikia mafanikio makubwa , walioweza kuvumilia upweke na kusimamia wenyewe licha ya kupingwa na kukatiswa tamaa.
Asante Sana kocha kwa mafunzo mazuri.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kupingwa na kukatishwa tamaa ni sehemu ya mafanikio, Nipo tayar kusimama mwenyewe na kuvumilia upweke!
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kufuata mkumbo kuna hatari kubwa.
Kuwa na msimamo siyo hiari, ila ni lazima.
Mafanikio makubwa yapo kwa wachache kwa sababu wao ndiyo wanaoweza kuvumilia upweke wa kusimama wenyewe, wanaoweza kupuuza kupingwa na kukatishwa tamaa na wengine.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa kweli ugonjwa wa kufuata mkumbo unatumaliza wengi. Watu wanaogopa kufanyaabo tofauti na wengine hata kama ndani ya mioyo yao wanaamini kabisa kufamya hivyo ji kitu sahihi. Dhana ya wengi wape si sahihi wakati wote. Kama tunaamini kitu fulani ni kitu sahihi, hicho cha kufanya hata kama tutafanya pekee yetu
LikeLike
Sahihi ni sahihi hata kama haikubaliki na wengi.
LikeLike
Hakuna mwenye maono kama yangu wala wenye msukumo nilionao. Hivyo najisukuma na kukaa kwenye mchakato sahihi Ili kuyafikia ndoto na maono zangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni kiasi gani nimejitoa kweli kufikia ndoto zangu?Hili ni swali la msingi la kujiuliza kila siku
LikeLike
Vizuri sana kwa swali hilo muhimu.
LikeLike
Nimeamua kuukubali upweke Wa kusimama mwenyewe Hadi nipate ninachokitaka.
Hakuna Cha kunizuia.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike