2995; Ongoza.
Rafiki yangu mpendwa,
Viongozi huwa wana kazi kuu moja, ambayo ni kuongoza.
Na ili kuongoza vyema, huwa wanaondoa kila aina ya mashaka wanayokuwa nayo.
Wanajitoa kweli kweli kwenye kile ambacho wanakifanya.
Viongozi bora misimamo yao huwa inajulikana wazi.
Kama wapo ndani basi wapo ndani moja kwa moja.
Hawawi mguu mmoja ndani na nguu mwingine nje.
Wanaweza kufanya makosa mbalimbali kupitia maamuzi wanayofanya, lakini hayo hayawaondoi kwenye kujitoa hasa kufikia kile wanachotaka.
Viongozi bora wanajua ili waaminike na watu, wanapaswa kuamini sana kile wanachosimamia.
Wanajua watu hawataki sana kuamini anachoamini kiongozi, bali wanatama kiongozi awe anaamini kweli kile anachoamini.
Ni imani yake isiyoyumbishwa ndiyo inawavutia watu kuja kwake na kuwafanya waendelee kuwa naye.
Wewe ni kiongozi kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako.
Lakini eneo kuu ni biashara.
Mafanikio ya biashara yako yanategemea sana uongozi wako.
Usipokuwa kiongozi imara, huwezi kujenga timu imara na biashara yenye mafanikio.
Kila unapoona biashara inayoshindwa kukua, jua wazi kilichokosekana ni uongozi imara.
Biashara inaweza kuwa na wazo zuri na ikawa na wateja wenye uhitaji, lakini bila ya uongozi imara, haiwezi kukua.
Changamoto nyingi zinazotokana na ukuaji wa biashara huwa zinaanzia kwenye kukosekana kwa uongozi imara.
Kushindwa kujenga mfumo imara wa kuiendesha biashara ni kukosekana kwa uongozi mzuri.
Uongozi mzuri huwa na maono makubwa yanayomsukuma mtu kuweka mfumo wa kuhakikisha maono hayo yanaendelea hata kama hayupo.
Kushindwa kujenga timu imara ya kuendesha biashara ni kukosekana kwa uongozi mzuri.
Uongozi mzuri huwa unawaweka watu sahihi kwenye mfumo wa biashara na kuhakikisha wanafanya kile wanachopaswa kufanya.
Uongozi mbovu huwaacha watu wajiendee vile wanavyotaka wao wenyewe.
Hilo hupelekea watu wengi wazuri kupotea, kwa kukosa uongozi.
Na pia kushindwa kujenga wateja waaminifu kwenye biashara, ambao wanasababisha mauzo makubwa ni kukosekana kwa uongozi mzuri.
Wateja wanakaa pale ambapo wanathaminiwa na wanaona mwanga mkubwa mbele.
Kama unataka kujenga biashara yenye mafanikio makubwa, neno ni moja tu; ONGOZA.
Kila unapokwama na kukutana na changamoto jiulize ni wapi umeshindwa kuongoza vizuri.
Utaona na kuweza kuchukua hatua sahihi.
Uongozi bora siyo kuwafanya watu wajisikie vizuri kwa kuwaambia wanachotaka kusikia na kuwaacha wafanye wanachotaka kufanya.
Uongozi bora ni kuwafanya watu wafanikiwe kwa kuwaambia wanachopaswa kusikia na kuwafanya wafanye wasichotaka kufanya, lakini ni muhimu kwao.
Kuwa kiongozi bora kwa kuongoza.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante kocha, kila unaposhindwa au kukutana na changamoto jiulize wapi umeshindwa kuongoza?
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Uongozi ndiyo mpango mzima
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nitakuwa kiongozi bora siku zote kwenye biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nimeelewa kocha nahitaji kuwa kiongoz bora Ili biashara Yang ikuee
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nakua kiongozi bora wa biashara yangu ili kuwafanya wale ninaowaongoza kufanya kile kilicho sahihi na kutekeleza kile wasichotaka.
Asante kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kiongozi bora ana maono makubwa, anayaeleza kwa wafuasi wake na kuyasimamia muda wote hadi kufikia mafanikio makubwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha,umeeleza vuzuri kwenye kipindi cha amka BIT na kwenye makala hii, nahitaji kuwa kiongozi bora na mwenye maono kwenye biashara yangu hata ktk familia yangu.asante
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kiongozi bora lazima kuwa na msimamo thabiti, Asante kocha kwa Makala
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kweli maono mazuri pekee hayatoshi kwenye biashara
LikeLike
Uongozi ni muhimu sana.
LikeLike
Kuwa kiongozi ni muhimu kwa ajili ya ubora wa taasisi
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Shukrani kocha.
Nitawekeza nguvu nyingi kuwa bora kwenye uongozi ili kujenga timu,mifumo na wateja waaminifu .
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mimi ni kiongozi bora wa biashara yangu.
Ili biashara iweze kuwa Bora ni lazima uwe kiongozi bora.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kila kitu kinafanikiwa au kushindwa kutokana na uongozi.
LikeLike
Ndiyo maana wahenga walisema samaki huanza kuoza kichwani.
LikeLike
Swali la kujiuliza kila ninapopitia changamoto kwenye biashara yangu ni…..wapi nashidwa kuongoza vizuri?
LikeLike
Hapo utaona chanzo halisi cha tatizo.
LikeLike
Uongozi imara ndiyo kivutio Cha wengi kubakia kwenye biashara.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante Kocha,
Kuwa kiongozi bora maana yake ni:-
1. Kujenga mfumo imara wa kuiendesha biashara
2. kujenga timu imara ya kuiendesha biashara
3. kujenga wateja waaminifu kwenye biashara ambao wanasababisha mauzo makubwa.
Na hapa ndipo sisi akina Bilionea Mafunzoni tunafanyia kazi kila siku.
LikeLike
Tunakaa humo mpaka misingi imara ijengeke.
LikeLike
Tunapaswa kukaa humo kwa msimamo bila kuyumba.
LikeLike
Kuwa kiongozi Bora Kwa kuongoza
Uongozi Bora wa sio kuwafanya watu wajisikie vizuri Bali
Kufanya vitu sahihi vyenye maslahi Kwa watu wake
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nitahakikisha nakuwa kiongozi bora
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Usipokua kiongozi imara hutaweza kujenga timu imara ya biashara yenye mafanikio .
Asante kocha kwa makala nzuri.
LikeLike
Tuwe viongozi na tuongoze.
LikeLike
Uongozi bora ni kuwafanya watu wafanikiwe kwa kuwaambia wanachopaswa kusikia na kuwafanya wafanye wasichotaka kufanya, lakini ni muhimu kwao.
Let us lead.
Thank you coach Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika, Leaders Lead.
LikeLike
kila niapoona biashara yangu haiendi vizujri ni wazi ya kwamba shida ipo kwenye uongozi!
LikeLike
Matatizo yote huanzia juu.
LikeLike
Nakuwa kiongozi bora kwangu kwanza kwangu mwenyewe kwa familia, kwenye biashara na jamii kwa ujumla. Asante Kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nakuwa kiongozi bora kwangu kwanza kwangu mwenyewe kwa familia, kwenye biashara na jamii kwa ujumla. Asante Coach.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ninakuwa Kiongozi Bora,maana Kufanikiwa kwangu kunategemea uongozi Bora.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike