2998; Amini.
Rafiki yangu mpendwa,
Kujenga timu bora ya kuendesha biashara kunahitaji watu.
Na watu huwa wanapenda kumfuata mtu anayejua wapi anakwenda na ana amini atafika kule anakokwenda.
Ili uweze kuwavuta watu sahihi kuja kwako, lazima uwe kiongozi mzuri, ambaye unajua unakokwenda na unaamini utafika unakokwenda.
Watu wanataka uwe na imani isiyoyumba kuhusu kufika kule unakokwenda.
Imani huwa inaambukizwa, unapoamini kile unachoamini, bila ya kuyumbishwa, watu nao wanakuamini.
Wanachotaka watu siyo wao waamini kile unachoamini, bali waamini unaamini unachoamini.
Bila ya kuwa na imani ya kule unakokwenda, hakuna mtu anaweza kuwa na imani na wewe na kukufuata.
Hivyo hata kama huna uhakika, unapaswa kuwa na imani isiyoyumba, siyo kwa ajili yako, bali kwa ajili ya watu wako.
Na imani hiyo haipaswi kuwa ya kuigiza, bali imani thabiti, ambapo unakuwa tayari kujitoa kafara kwa kile unachoamini.
Ni kujitoa kwako kafara ndiko kunakowapa watu uhakika wa kukufuata wewe.
Kwenye safari yetu ya kuelekea kwenye ubilionea, imani yako inapaswa kuwa ya sehemu nne;
Moja ni kuamini kwenye kitu kikubwa nje yako, hapa ni kuamini kwenye mchakato wa kuelekea kwenye ubilionea. Amini sana kwenye mchakato huo na kuufuata bila kuyumba.
Mbili ni kuamini kwenye ndoto kubwa ulizonazo, amini utazifikia bila ya shaka yoyote.
Tatu ni kujiamini wewe mwenyewe kwamba utaweza kupata kile unachotaka, bila ya kuwa na wasiwasi wowote.
Na nne ni kuwaamini wale unaoambatana nao kwamba ni watu sahihi katika safari uliyopo.
Imani ina nguvu kubwa sana kwenye safari yoyote uliyopo.
Hiyo ni kwa sababu matatizo, vikwazo na changamoto huwa haviishi.
Pale mambo yanapokuwa magumu, watu humwangalia kiongozi.
Na hapo ndipo kiongozi anapopaswa kuwa na imani kali juu ya kile anachoendea.
Kiongozi hapaswi kuwa na wasiwasi au kuonekana kukata tamaa.
Kiongozi akionyesha wasiwasi au kukata tamaa anakuwa amefanya usaliti mkubwa kwa wafuasi wake.
Wafuasi wanakosa uhakika na kutafuta mahali pengine pa kwenda, ambapo panawapa uhakika zaidi.
Wajibu wako mkubwa kama kiongozi ni kuamini.
Na haijalishi kama una uhakika au la, unapaswa kuamini kwanza ili kuipa timu yako uhakika.
Mara kwa mara ieleze timu yako wapi mnakwenda na mtaweza kufikaje kule mnakokwenda.
Watie watu moyo kwamba pamoja na magumu na changamoto mnzopitia, ushindi ni uhakika.
Kazi yako kubwa ni kukaa kwenye mchakato na kuhakikisha watu wako wanakaa kwenye mchakato.
Na kwa sababu mchakato ni sahihi, ni swala la muda tu kabla matokeo mazuri hayajaonekana.
Amua kile unachotaka, ambacho hapa ni kuwa bilionea.
Amini kwenye mchakato wa kufika kwenye ubilionea na ufanyie kazi bila kuyumba.
Amini kwamba utafika kwenye ubilionea huo na wewe ni mtu sahihi kabisa.
Amini watu unaoambatana nao kwamba wanaweza na wasaidie kukaa kwenye mchakato.
Usiwe na shaka yoyote kwenye hayo unayoamini.
Hata kama ndani yako una wasiwasi wowote, usiuonyeshe nje.
Wewe simama kwenye imani yako na onyesha kuwa na uhakika mkubwa.
Hilo siyo kwa ajili yako, bali kwa ajili ya wale wanaokufuata.
Uzuri ni kwamba asili huwa inafanya mambo yake kwa namna ya ajabu kabisa.
Asili huwa inalipa mchakato, hivyo kwa kuamini na kukaa kwenye mchakato bila kuyumba, matokeo yanakuja, hata kama huna uhakika.
Kukaa kwenye mchakato kunaleta matokeo, utake usitake.
Ndiyo maana sehemu ya kwanza kuwa na imani nayo ni mchakato.
Hakikisha wewe na timu yako mnaamini na kukaa kwenye mchakato bila kuyumbishwa na chochote kile.
Maisha ni kuchagua na unapochagua unapaswa kuwa na imani kubwa kwenye kile unachochagua.
Bila ya imani, hakuna kingine kitakachowezekana kwenye safari yako.
Na kwenye hili swala la imani usijiangalie wewe peke yako, bali waangalie wale wanaokufuata, unaowahitaji zaidi ili kufika unakotaka kufika.
Wao kuambatana na wewe inategemea zaidi imani uliyonayo kwenye safari uliyopo.
Ikiwa huna imani au imani yako inayumbishwa, watakukimbia haraka sana.
Wape watu uhakika kupitia imani kali uliyonayo na wataambatana na wewe popote unapokwenda.
Imani inakupa wewe ujasiri na watu wanapenda kuwafuata wale ambao ni jasiri.
Usisubiri mpaka uwe na uhakika ndiyo uwe na imani.
Wewe anza na imani na uhakika utajitengeneza kadiri unavyokwenda.
Wakumbushe watu wako mara kwa mara kuhusu kule mnakokwenda na mchakato mzima wa kuwafikisha kule.
Wape uhakika wa kufika mnakokwenda kupitia mchakato uliopo.
Kisha kuwa mfano kwa kukaa kwenye mchakato.
Hilo litawapa watu imani kubwa ya kuendelea kukufuata na kukaa kwenye mchakato.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana kocha, nitaendelea kukaa kwenye mchakato bila kuyumba.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha, Nitakuwa na imani siku zote ili niwe jasiri ni kukaa kwenye mchakato bila kuyumbishwa na chochote kile.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Imani Ina nguvu kwenye kila kitu.
Na adui mkubwa wa imani ni mashaka. Mara zote kuwa na Imani kwenye maisha yako.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitasimamia imani juu ya kule ninakotaka kwenda siku zote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Napaswa kujiamini na kujijengea imani kubwa kwenye kile ninachochagua kufanya kwenye maisha yangu.
Asante sana Kocha Dr.Makirita Amani.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Imani ni kuwa na hakika ya mambo yajayo japo siyaoini lakini kuwa na imani na kukaa kwenye mchakato kutawafanya hata ninaoambatana nao kuendelea kukaa na mimi kwani wanaona nasimamia ninachokiamini.
Asante kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Lazima niamini kwenye
1. Mchakato
2. Ndoto kubwa
3. Kujiamini binafsi
4. Kuwaamini walio pamoja nami kwenye safari
Asante Kocha
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Ili niweze kuwavuta watu sahihi kuja kwangu, lazima niwe kiongozi mzuri, ambaye najua ninakokwenda na naamini nitafika ninakokwenda.
Watu wanataka niwe na imani isiyoyumba kuhusu kufika kule ninakokwenda.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kwa somo la leo
Imani inapaswa kuwa ya sehemu 4;
1-Ni kuamini kwenye mchakato na kuufuata bila kuyumba.
2-Kuamini kwenye ndoto kubwa,utazifikia bila ya shaka yoyote.
3-Kujiamini mimi mwenyewe nitapata kile ninachotaka, bila ya wasiwasi wowote.
4-Kuwaamini wale ninaoambatana nao kuwa ni watu sahihi katika safari niliyopo.
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Mimi kingozi wa biashara yangu, imani na mchakato inanilipa, niweke kwa matendo na kuihubiri kwa timu yangu
LikeLike
Wanahitaji kusikia mara nyingi sana kutoka kwako.
LikeLike
Kinachoangusha watu wengi ni Ile how . Yaani inawezekanaje? Hili ndiyo tatizo kubwa tulilonalo. Tunataka kuiona safari ya kilomita 50 tukiwa kilomita 0. Hilo halitawezekana. Aza safari na matokeo utayakuta hukohuko njiani. Ndiyo nitakuwa bilionea swali linakuja hapa itawezekana Vipi? Mtego huu ,wewe amini tu itawezekana wewe kujua itawezekana Vipi SI juu Yako .wewe Kaa kwenye mchakato na matokeo utayaona.
LikeLike
Asili ina namna ya kufanya mambo yake ambayo hakuna anayeweza kuelewa.
Wajibu wetu ni kuamini na kukaa kwenye mchakato bila kuyumbishwa.
LikeLike
Imani ni jambo la msingi katika njia yetu ya mapambano.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Natakiwa niamini nguvu ya mchakato wa ubilionea bila shaka yoyote.
LikeLike
Hapaswi kuwa na shaka kabisa.
LikeLike
Ahsante sana kocha.
Nitakuwa na Imani na kuiwezesha team yangu kuona mbali tunapoelekea.
Hakika ni makala Bomba sana hii
LikeLike
Tuwahubirie kila mara.
LikeLike
Asante Kocha,
Najiwekea malengo na mipango, kisha ninaamini katika mchakato, ndoto yangu kubwa, kujiamini Mimi binafsi na imani kwa wale ninaoambatana nao.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Naamini bila ya shaka yoyote, naamini katika mchakato,naamini maono makubwa ya kufikia Ubilionea,najiamini na naamini watu ninaoshirikiana nao.
Imani ndiyo msingi mkuu Wa kuhamisha milima.
LikeLike
Safi sana.
Tusikubali kuyumbishwa.
LikeLike
Naamini bila ya shaka yoyote, naamini katika mchakato,naamini maono makubwa ya kufikia Ubilionea,najiamini na naamini watu ninaoshirikiana nao.
LikeLike
Tusimame imara kwa imani.
LikeLike
Watu hawahitaji kuamini bali wanataka kukuona wewe ukiamini.
LikeLike
Kabisa, usigangaike kuwaaminisha watu kile unachoamini, wewe kiamini bila ya shaka yoyote na wao watakuamini wewe kwa kukiamini.
LikeLike
Asante sana, imani inaweza kuhamisha mlima.
LikeLike
Maneno yaliyosemwa miaka mingi na bado yamesimama, kwa sababu ni ya kweli. Tuwe na imani.
LikeLike
Naamini kwenye mchakato na Nina Imani kubwa sana Kwa wale ninaoambatana nao kufika kwenye mafanikio makubwa
Asante
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Imani ndiyo kila kitu kikubwa kuamini na kuendelea kukaa kwenye mchakato Asante kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Kitu nilichojifunza kwenye Makala ya leo ni:-
Tunahitaji kuwa na timu bora ya watu ili kujenga biashara.
Watu hupenda kumfuata kiongozi anayejua wapi anakwenda
Kiongozi huyo anapaswa kuwa ni mtu mwenye Imani ya kufika kule anakotaka kufika.
Hivyi basi ni vizuri mimi kama kiongozi kuwa na IMANI ISIYOYUMBA ya kufika kule unakotaka kufika.
Asante
LikeLike
Umesema vyema, tukae humo.
LikeLike
Dawa kali kuliko zote hapa ni kuamini mchakato na kuwa na mchakato ambao ni sahihi..
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nahitaji kuwa na Imani ya kule ninakokwenda na kuendelea kuthibitisha Hilo kwa timu yangu. Bila Kujali wapi nilipo na nini ninapitia.
Kazi yangu Kama Kiongozi Ni kubaki kwenye Imani hiyo na kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kiongozi kukata tamaa ni kufanya usaliti mkubwa kwa wale unaowaongoza .
AMINI kwenye mchakato unaoufanyia kazi kufikia kwenye ubilionea na asili itakupa matokeo Bora kabisa
Asante sana kocho
LikeLike
Karibu
LikeLike
Hapo kwenye kuamini kile unachokiamini ndipo penye changamoto. Wengi hawaamini kile wanachoamini. Ndiyo maana hata kwenye imani za dini wengi huwa hawaishi kulingana na kile wanachofundishwa kwenye dini. Tukiweza kuamini kile tunachoamini hapo tutakuwa tumefaulu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Imani ndio kitu pekee ambacho ni muhimu sana katika safari yangu ya Ubilionea na mchakato ni lazima kuufuata..
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Imani yangu ndiyo kitulizo changu. Naamini nitafika na kuibuka mahindi. Njia Ni ngumu na majaribu ni mengi. Sitaki kukata tamaa na wale nilionao nawaonyesha kuwa ushindi ni uhakika Ila Ni swala la muda tu.
Kuchelewa kupo na kulaghaiwa kupo Ila nitashikiria mchakatopaka mwisho.
Asante Sana Kocha
LikeLike
Ushindi ni lazima.
LikeLike
Ni kweli mkurugenzi asipokua na imani walioko chini yake wanakata tamaa na kuyumbishwa kabisa na kuona hakuna mwanga mbele
LikeLike
Kabisa.
LikeLike