3000; Aftatu.
Rafiki yangu mpendwa,
Leo ni siku ya elfu tatu ya kuandika kila siku bila kuacha.
Siku hizo elfu 3 zilizopita, nilijipa changamoto ya kuhakikisha kila siku naandika.
Na sharti lilikuwa rahisi sana, kama kwenye siku napata muda wa kuoga, kula, kulala basi pia natakiwa kupata muda wa kuandika.
Sikuanza kujiambia vipi kama…
Wengi wanapotaka kujiwekea malengo au changamoto za aina hii huwa wanaanza na maswali ya vipi kama…
Vipi kama nitaumwa?
Vipi kama nitakosa kifaa cha kuandikia?
Vipi kama nitakuwa eneo lisilokuwa na mtandao?
Na mengine mengi ambayo watu wamekuwa wanatumia kama sababu.
Ushauri ambao nimekuwa nawapa watu pale wanapokuja na maswali ya vipi kama… ni huu; utavuka daraja utakapolifikia.
Kama kuna safari umepanga na njia unayopita ina daraja hatari, haitasaidia wewe kuhofia utalivukaje hilo daraja.
Badala yake unatakiwa kuendelea na safari ukijua kwamba daraja utalivuka pindi utakapolifikia.
Ushauri mwingine muhimu ni kutenga muda wa kufanya mambo muhimu kila siku.
Mambo yote ya msingi kwenye maisha yako, huwa unayafanya kila siku bila kuacha.
Hata uwe umetingwa kiasi gani, bado utatenga muda na kufanya yaliyo muhimu.
Kila siku utasafisha mwili wako, utapata chakula na utapumzika au kulala.
Hakuna siku unayokuwa umetingwa sana kiasi cha kuyaahirisha hayo ya msingi.
Kuna somo kubwa sana tunalojifunza hapo kwenye yale ya msingi.
Kama jambo ni muhimu kweli, muda wa kulifanya huwa unapatikana.
Jipe changamoto ya kufanya kitu kila siku bila ya kuacha hata mambo yaweje.
Chagua kitu kimoja ambacho utakifanya kila siku bila ya kuacha hata siku moja.
Unapochagua kitu hicho, usianze kujiuliza maswali ya vipi kama …..
Wewe jiambie utafanya halafu ufanye kweli bila kuruhusu sababu au visingizio vyovyote kukuzuia.
Kupanga kufanya kitu kila siku na kutekeleza kama ulivyopanga ni ushindi mkubwa sana kwenye siku ya maisha yako.
Kila siku kunakuwa na ushindi ambao unaupata bila kujali siku husika imeendaje.
Siku iwe nzuri au mbaya kwako, tayari kuna ushindi umeshaupata kwa kutekeleza kile ulichopanga kufanya kila siku bila kuacha.
Jambo la mwisho ni unapaswa kuwa na kichwa ngumu sana ili mambo yako yaende kama ulivyopanga.
Kwa sababu kuna mengi yatakayojitokeza na kutaka kuathiri yale uliyopanga.
Ukiruhusu hilo litokee, hata kwa mara chache tu, utajenga mazoea yasiyo sahihi na itakuwa kikwazo kwako kutekeleza kama ulivyopanga.
Kuwa mbishi na kuwa king’ang’anizi hasa ili uweze kufanya kama ulivyopanga.
Kuna wakati utajishawishi kwamba unaweza tu kuacha siku moja kwa yale unayokuwa unapitia.
Hapo ndipo unapopaswa kuelewa kwamba ukisharuhusu mara moja, utaruhusu tena na tena na tena.
Kuondokana na hilo ni kutokukubali sababu yoyote kuwa kikwazo kwako kwenye yale uliyoyapanga.
Je ni kitu gani ambacho umechagua kuwa unafanya kila siku bila kuacha hata siku moja?
Shirikisha kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hongera sana kwa ushindi wa kuandika siku elfu Tatu.
Nimechagua kuandika Kila siku tokea mwaka 2016.
LikeLike
Hongera sana Mwl Deo kwa msimamo kwenye uandishi.
Wajibu wetu ni kukaa kwenye mchakato, mengine yatakuja kwa wakati wake.
LikeLike
Kuweka akiba
LikeLike
Safi sana.
Chagua kiwango na wapi utaweka kisha weka kila siku bila kuacha.
LikeLike
Kitu ambacho nimechagua nitafanya kila siku bila kuachq ni kuweka AKIBA na kusoma vitabu
LikeLike
Hongera sana kwa haya, endelea kuyazingatia.
LikeLike
Asante Sana kwa makala hii, pia hongera sana kwa kutimiza siku elfu 3 toka ulipojipa jukumu la kuandika kila siku.
Mimi ninajipa jukumu kwamba nitajifunza Mambo mawili mapya kupitia kusoma , Mambo hayo yatakuwa ni Mambo maalumu kwa ajili ya program hii. Asante
LikeLike
Asante sana.
Kila la kheri.
LikeLike
Hongera Kocha, Leo tarehe 19/03/2023, naahidi apa kusoma na kuandika kwenye blog ya ElimuKodi kila siku, kuhusu Uhasibu na Kodi
LikeLike
Vizuri, andika.
LikeLike
Hongera sana kwa kutimiza siku elfu 3 toka ulipojipa jukumu la kuandika kila siku.
Mimi ninajipa jukumu kwamba nitajifunza Mambo mawili mapya kupitia kusoma , Mambo hayo yatakuwa ni Mambo maalumu kwa ajili ya program hii. Asante
LikeLike
Asante.
Kila la kheri.
LikeLike
Hongera sana kwa nidhamu hii kali sana. Ni nidhamu ya kipekee sana.
Mimi nimejipa jukumu la kusoma kila siku.
LikeLike
Asante sana.
Komaa kwenye hilo.
LikeLike
Hongera sana kocha kwa kutuonyesha kwamba inawezekana, Kila siku nitajifunza na kuandika lugha ya kiingereza bila kuacha.
LikeLike
Asante sana.
Kila la kheri.
LikeLike
Hongera sana kwa ushindi huo, hakika huu ni mfano na njia nzuri kwetu kujifunza zaidi, nitaendelea kujifunza kila siku
LikeLike
Asante sana.
Kila la kheri.
LikeLike
safi sana kwa siku 3000,,hakika kweli umepambana kwa msimamo.Hongera sana kwa hilo.
Nitajifunza kila siku bila kuacha kwa kupitia usomaji vitabu
LikeLike
Asante sana.
Kila la kheri.
LikeLike
Hongera Sana kocha kujiwekea msimamo na kufanya Kila siku.
Nimejiwekea Kuhakikisha Kila siku Naweka AKIBA na kuwekeza Kila siku
LikeLike
Asante sana.
Chagua unaweka wapi na uwe unatoa ushahidi.
LikeLike
Mimi najipa changamoto ya kuamka mapema saa 10 alfajir kila siku bila kuacha
LikeLike
Safi sana,
Kamilisha hilo.
LikeLike
Asante sana kocha Kwa nidhamu hii kubwa uliyonayo Kuna kitu kikubwa sana nimejifunza kutoka kwako.
Kwa upande wangu kitu Cha kufanya kila siku ni Kusoma na kujifunza hiyo ni kama kula chakula kwangu, lazima nisome
Asante
LikeLike
Asante sana.
Kila la kheri.
LikeLike
Nimechagua kukaa kwenye mchakato wa BM bila kuacha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nmepanga kuandika kila siku bila kucha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hongera sana Kocha kwa NIDHAMU hiyo kali.
Nimechagua kuandika kila siku bila kuacha.
LikeLike
Asante.
Kila la kheri.
LikeLike
Hongera kocha kwa nidhamu hii kali.Mimi nimechagua kuandika poster kuhusu malezi kila siku.
LikeLike
Asante,
Kila la kheri.
LikeLike
Nitaweka akiba ya shilingi elfu kumi kila siku!
LikeLike
Safi sana.
Kamilisha hilo.
LikeLike
Hongera sana, kwa kufanya bila kuacha kwa siku aelfu tatu,
Mimi nimejiekea kusoma kila siku lakini naona haitoshi inabidi kuwa kujifunza na kuchukua hatua kila siku.
LikeLike
Asante.
Kila la kheri.
LikeLike
Nimechagua kusoma na kujifunza kila siku
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Safi sana Kocha kwa alfu 3 ni nidhamu kubwa sana. Tulikufuata tulilegalega kwenye uandishi. Sasa narudi upya kuanzia leo 20.3.23 kuandika kila siku.
LikeLike
Asante sana.
Ushahidi wako wa kuandika kila siku tunaupata wapi?
LikeLike
Anza upya, kwa msimamo zaidi.
LikeLike
Hongera sana Kocha.
Nidhamu Yako si ya kitoto.
Nami kuanzia Leo Nimeianza kitu kimoja kila siku bila kuacha,
Kuamka mapema saa 10 alfajiri na kulala mapema saa Tano usiku kila siku bila kuacha Kwa siku 100 moja.
LikeLike
Asante,
Vizuri sana.
Kwa nini siku 100? Kwa nini isiwe ndiyo mtindo wako mpya wa maisha?
LikeLike
Mambo ya Aftatu ya kocha haya,,, lazima niyaige.
Nami naahdi kusoma kurasa kumi za kitabu kila siku bila bila kuacha.
Asante sana kocha.
LikeLike
😂😂
Karibu kwenye challenge.
LikeLike