3021; Haina mjadala.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye maisha yangu sijawahi kusikia mtu anasema amekuwa bize sana kiasi kwamba amekosa muda wa kupumua.
Au mtu kusema ametingwa sana kiasi cha kushindwa kula chochote kwa siku nzima.
Kuna vitu ambavyo hata iweje lazima uvifanye kwenye kila siku yako.
Hata iwe umebanwa kiasi gani, lazima utapumua, utaoga, utakula, utajisaidia na utalala.
Unaumwa, una msiba, umesafiri au kingine chochote, bado utayafanya mambo hayo.
Unajua kwa nini lazima uyafanye mambo hayo?
Ni kwa sababu hayana mjadala.
Huna nafasi ya kuanza kujiuliza kama utafanya au la, jibu ni moja tu, kufanya ni lazima.
Hujiulizi kama una muda wa kuyafanya, ni lazima utenge muda na kuyafanya.
Lakini inapokuja kwenye mambo mengine muhimu kwenye maisha yako, mambo yanayokufikisha kwenye ndoto zako, unaruhusu mjadala.
Unaanza kujiuliza kama una muda au utulivu wa kutosha kuyafanya.
Na pale chochote kinapokuwa hakijakaa sawa kwenye maisha yako, unayaahirisha mambo hayo.
Hapa naongelea mambo kama kujifunza, kufanya kazi kwa kina, kuchukua hatua muhimu unazopaswa ili kufikia ndoto zako na majukumu mengine muhimu kwenye maisha yako.
Unaruhusu mjadala wa iwapo utafanya au la na kwa kuwa ni mambo magumu na ya kukuchosha, kila mara unapata sababu za kutokufanya.
Unajikuta unayasogeza mbele mambo hayo muhimu na kinachotokea ni huyafanyi au hata ukiyafanya siyo kwa uhakika.
Kama unataka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, ni lazima uwe na orodha ya mambo ambayo lazima utayafanya kwenye kila siku yako bila ya mjadala.
Yaani kama tu upo hai, lazima uyatengee muda wa kuyafanya.
Haijalishi kama unaumwa, una msiba, umesafiri au umetingwa kiasi gani.
Kama unapata muda wa kupumua, kula na kulala, unapata pia muda wa kuyafanya hayo muhimu.
Watu wanaweza kutofautiana kwenye orodha ya mambo gani ya kufanya kila siku bila mjadala.
Lakini kwa kila anayetaka mafanikio makubwa, lazima mambo haya yawe kwenye orodha yake.
1. Kujifunza vitu vipya, hasa kupitia usomaji wa vitabu.
2. Kuwa na muda wa kufanya kazi kwa kina, hasa kwenye biashara yake.
3. Kuingiza kipato na kujenga utajiri.
4. Kujenga afya ya mwili, akili, roho na hisia.
5. Kujenga na kuimarisha mahusiano na watu wengine wa muhimu kwake.
Mambo hayo na mengine kulingana na mtu ni ya muhimu sana kufanya kila siku bila ya kuruhusu mjadala wa iwapo ufanye au usifanye.
Huianzi siku yako kwa kujiuliza kama utapata muda wa kuyafanya hayo muhimu, badala yake unapanga kwenye orodha yako ya siku ni muda gani utayafanya mambo hayo muhimu.
Ni kufanya kwa msimamo bila kuacha ndiko kunakozalisha matokeo makubwa na mazuri.
Kama kuna kitu chochote kinachoweza kukuzuia usifanye yale ambayo ni muhimu kwako kufanya, kila mara kutakuwa na kitu cha kukuzuia.
Maisha hayatakuachia upenyo wa kuyafanya hayo muhimu, kila wakati utakuwa na kitu cha kukuzuia.
Lakini kama umeondoa kabisa mjadala wa iwe utafanya au la, kama kufanya ni lazima hata iweje, utaziona fursa nyingi za kukuwezesha kufanya.
Akili zetu huwa zina nguvu za ajabu sana, huwa zinatuonyesha kile tunachotaka kuona na kutupa fursa za kukamilisha yale hasa tuliyodhamiria.
Mtu mmoja amewahi kusema kama unataka kufanikiwa kama unavyotaka kupumua, hakuna kitakachokuzuia usifanikiwe.
Leo hii ukiwa na shida yoyote ya upumuaji utahangaika kwa kila namna kuhakikisha unapumua.
Lakini ukikwama kwenye safari yako ya mafanikio, unakata tamaa.
Haipaswi kuwa hivyo, safari yako ya mafanikio ni jambo ambalo halipaswi kuwa na mjadala kwako, ni lazima ufanye yale unayopaswa kufanya ili ufanikiwe, iwe unajisikia kufanya au la.
Ukiruhusu mjadala kwenye mambo muhimu kwako, utapata sababu za kutokuyafanya, kwa sababu mambo yote muhimu ni magumu.
Ukiondoa mjadala utayafanya, hata iweje.
Ondoa mjadala na kila siku weka kwenye orodha ya mambo muhimu kukamilisha na yakamilishe kama vile umewekewa bastola kwamba usipofanya inavyatuliwa.
Ni nidhamu ya viwango hivyo ndiyo itakayokufikisha kwenye mafanikio makubwa na unayoyataka.
Swali muhimu sana kwako ni hili; je ni mambo gani matatu ambayo lazima utayafanya kila siku ya maisha yako bila ya kuruhusu mjadala wowote wa iwe utafanya au la?
Yangu ni KUSOMA, KUANDIKA na KUFUNDISHA/KUKOCHI.
Shirikisha matatu yako kwenye maoni hapo chini.
Na kwenye kila siku yako onyesha ushahidi kwamba umeyakamilisha mambo hayo matatu muhimu kwako, kupitia orodha ya mambo yako ya kukamilisha kwenye siku na tathmini zako za kila siku.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante na hongera sana kwa kazi hii nzuri unayoendelea kuifanya Dr Makirita Amani.
KUANDIKA, KUSOMA NA KUFUNDISHA.
LikeLike
Karibu sana Mwl Deo.
Tukae humo, haina mjadala.
LikeLike
Mambo matatu ninayofanya kila siku
Kusoma na kujifunza,kuwasiliana na wateja na kusaka wateja wapya ,kuwa na to do list na kuitekeleza kama nilivyopanga.
LikeLike
Vizuri sana, kaa humo bila kuruhusu mjadala.
LikeLike
Asante kocha,mambo matatu ntakayofanya kila siku bila kuacha ni kusoma,biashara na kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Safi sana,
Usiruhusu mjadala.
LikeLike
MAMBO MATATU AMBAYO NAFANYA KILA SIKU 1. KUWEKA AKIBA 2. KUSOMA VITABU 3. KUWEKEZA KWENYE BIASHARA
LikeLike
Vizuri sana,
Usiruhusu mjadala kwenye hayo.
LikeLike
Hakuna mjadala mambo matatu nitakayoyafanya kila siku.
Kujifunza
Biashara.
Kazi
LikeLike
Safi sana,
Usiruhusu mjadala.
LikeLike
Hakuna mjadala kocha, Kujifunza, kukaa kwenye mchakato na Kujenga afya
LikeLike
Safi sana.
Usiruhusu mjadala kwenye hayo.
LikeLike
Nodahmiyya Hali ya juu sana,
Mambo yangu matatu ni kujifunza, kuandika na kuchukua hatua,
LikeLike
Safi sana,
Usiendekeze mjadala.
LikeLike
Mambo matatu.
Kusoma.
Kuandika.
Kuuza.
LikeLike
Kaa humo bila kuruhusu mjadala.
LikeLike
1.KUUZA(Kazi)
2.KUJIFUNZA
3.KUFIKIRI KWA UTOFAUTI KATIKA KUZIENDEA NDOTO KUBWA.
LikeLike
Safi sana.
Usiruhusu mjadala kwenye haya.
LikeLike
—kujifunza
—kujenga biashara
—kuishi kusudi la maisha yng duniani.
god blees kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
Usiruhusu mjadala.
LikeLike
Mambo yangu muhimu kila siku ni kupiga simu, kutafuta wateja na kusoma. Na nitayafanya kila siku bila kisingizio
LikeLike
Vizuri, usiruhusu mjadala.
LikeLike
Kuandika
Kusoma
Kazi
LikeLike
Vizuri, kaa kwenye haya bila kuruhusu mjadala.
LikeLike
asante,
NITASOMA/KUJIFUNZA(PROFESSIONAL AND DEVELOPMENTAL)
NITATIBU BINADAMU.
KUKAA KWA MCHAKATO WA BM
LikeLike
Safi sana, usiruhusu mjadala kwenye hayo.
LikeLike
Kujifunza, kuwekeza kufanya kazi,kuandika
Asante sana
LikeLike
Asante Sana Kocha kwaakala hii, imenifungua Sana na kunifanya nitafakari. Mambo matatu ambayo nitayafanya kila siku bila kuacha ni
1. KUSOMA AU KUJIFUNZA
2. KUFANYA MAZOEZI
3. KUSALI AU TAHAJUDI
Asante snaa
LikeLike
Asante Sana Kocha kwaakala hii, imenifungua Sana na kunifanya nitafakari. Mambo matatu ambayo nitayafanya kila siku bila kuacha ni
1. KUSOMA AU KUJIFUNZA
2. KUFANYA MAZOEZI
3. KUSALI AU TAHAJUDI
Asante snaa
LikeLike
Yangu ni
Kusoma
Kuwapigia wateja wangu simu
Kuwatembelea na kuwapa hadithi yangu
LikeLike
Mambo 3
Kusoma, Kujifunza na kukuza Biashara
LikeLike
Kusoma vitabu
Kujenga timu
Kuuza
LikeLike
Mambo matatu kusoma, kujifunza, kufuatilia wateja.
LikeLike
Asante kocha kwa makala hii. Mambo matatu ya kufanya ni;
* Kusoma
* Kukuza biashara na
* Kujenga timu.
LikeLike
MAMBO YANGU MATATU NI KUSOMA KITABU, KUHUDUMIA WATEJA NA KUFANYA IBADA
LikeLike
Kaa humo.
LikeLike
Asante Kocha
1. Sala na Tahajudi
2. Akiba na Uwekezaji
3. Kusoma na Kuandika
LikeLike
Vizuri sana.
Tungependa kuona uandishi wako.
LikeLike