3033; Wasiwe na pengine pa kwenda.
Rafiki yangu mpendwa,
Mafanikio makubwa unayoyataka kwenye maisha yako, yatatokana na watu.
Unahitaji sana watu ili kuweza kufikia ndoto kubwa ulizonazo.
Na kadiri ndoto zako zinavyokuwa kubwa, ndivyo unavyowahitaji watu wengi na kwa muda mrefu.
Lakini changamoto moja kubwa kwenye watu ni huwa hawaeleweki. Unaweza kuwapata watu na kuwapa kile wanachotaka, lakini bado wakakuacha na kwenda kwa wengine.
Hilo huwa linakatisha tamaa na kuona watu hawawezi kuaminika.
Kabla hatujaangalia ni kwa namna gani unaweza kuwafanya watu wakae na wewe kwa muda mrefu, tuangalie kwanza aina ya watu unaowahitaji kwenye safari yako ya mafanikio.
Kuna aina kubwa tatu za watu unaowahitaji kwenye safari yako ya mafanikio.
Moja ni watu wa kushirikiana nao, hawa ni wale wanaokuunga mkono kwenye kile unachofanya. Mfano watu wanaokuwa tayari kuwekeza kwenye biashara yako.
Mbili ni wafanyakazi ambao wanatekeleza majukumu yote muhimu kwenye biashara yako.
Na tatu ni wateja ambao wananunua kile mnachouza kwenye biashara yako.
Unahitaji sana watu bora kwenye maeneo yote matatu ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Lakini kama ambavyo tumeshaona, mara nyingi watu huwa hawakai.
Unaweza kuwapata hao bora, lakini baada ya muda wanakuacha na kwenda kwingine.
Swali ni unawezaje kuwafanya watu bora wabaki na wewe kwa muda mrefu ili uweze kupata mafanikio makubwa?
Jibu ni moja, wafanye wasiwe na pengine pa kwenda.
Wape vitu ambavyo hawawezi kuvipata mahali pengine popote isipokuwa kwako.
Kwa washirika wape manufaa ambayo hawawezi kuyapata mahali pengine popote.
Kwa wafanyakazi wape mazingira bora ya kufanya kazi ambayo hawawezi kuyapata mahali pengine.
Na kwa wateja wape huduma bora kabisa ambayo hawawezi kuipata mahali pengine popote.
Kikubwa sana ni kuwafanya watu wasiwe na sababu ya kutaka kuondoka kwako na kwenda kwingine.
Hilo litawezekana kama utaondoa mazoea kwenye kila eneo la biashara yako na maisha yako.
Iko hivi, sisi binadamu huwa tunazoea vitu haraka sana.
Wakati tunawatafuta watu, huwa tunawaahidi vitu vingi.
Na wakati tunawashawishi wakubaliane na sisi, huwa tunawapa vitu vizuri ambavyo hawawezi kuvipata mahali pengine.
Cha kushangaza ni wakishakubaliana na sisi, tunaacha kuwapa vitu hivyo vya tofauti na kuleta mazoea.
Tunaweka mazoea ambayo yanawachosha watu na kuwafanya watafute mahali pengine ambapo watapata mambo mapya.
Hivyo ni muhimu sana uvunje kila aina ya mazoea kwa watu unaohitaji kwenda nao kwa muda mrefu.
Kila wakati kuwa na mambo mapya ya kuwavutia kuendelea kuwa na wewe.
Wafanye wakose sababu ya kutaka kwenda mahali pengine.
Na hata ikitokea wameenda pengine, wafanye watake kurudi kwako kwa yale unayokuwa unawapa ambayo hawataweza kwenda kuyapata kwingine.
Na mambo ya kufanya ili watu wabaki na wewe haimaanishi upande wa fedha pekee, japo huo ni muhimu.
Wengi hudhani ili washirika wabaki na wewe, lazima uwape faida kubwa kwenye uwekezaji wao.
Ili wafanyakazi wabaki na wewe, lazima uwalipe mshahara mkubwa.
Na ili wateja wabaki na wewe, lazima uwauzie kwa bei ndogo kuliko wengine.
Ndiyo fedha ina umuhimu sana, lakini siyo peke yake.
Unaweza kuwapa watu faida kubwa na bado wasiwe tayari kushirikiana na wewe.
Unaweza kuwalipa wafanyakazi mshahara mkubwa na bado wakaondoka na kwenda kutafuta kazi pengine.
Na unaweza kuwapa wateja bei ndogo kabisa na bado wakaenda kununua pengine ambapo bei siyo ndogo kama yako.
Unapojihusisha na watu, kitu kikubwa kabisa unachopaswa kufanya ni kuwafanya wajisikie vizuri.
Wafanye wajione wapo sehemu salama na inayowapa nafasi ya kutoa mchango wao kwenye kitu chenye manufaa makubwa.
Hilo huwafanya watu wajivunie kuwa sehemu hiyo kutokana na fursa ya kufanya makubwa wanayoipata.
Kwa washirika wafanye waone kwa kushirikiana na wewe wanapata nafasi ya kuwa sehemu ya mambo makubwa yanayokwenda kufanyika.
Kwa wafanyakazi wafanye waone wanaenda kujenga kitu kinachokweda kufanya makubwa na hivyo kuwa sehemu ya historia.
Na kwa wateja wafanye waone wanakwenda kumiliki kitu ambacho hakipatikani kwa urahisi kila mahali.
Wewe mmiliki na kiongozi wa biashara kama kiungo kikuu cha watu kwenye biashara yako, unahitaji kufanya kazi kubwa na ya ziada ya kuwafanya watu watake kuja kwenye biashara yako na wakishakuja watake kuendelea kubaki.
Utaweza kukamilisha hilo kwa kujenga biashara ambayo ni bora na ya kipekee kabisa, ambayo inatoa fursa zisizoweza kupatikana kwingine.
Ni lazima uwe mbunifu kila wakati na kuchukua hatua za hatari.
Ni lazima uondokane na mazoea na kila wakati kuwa mbele ya wengine, kwa kuona fursa ambazo bado hazijafikiwa na kutumiwa na wengine.
Hayo yote yatawezekana kama utaifanya biashara yako kuwa kipaumbele cha kwanza kwako.
Kama utaweka umakini wako wote kwenye biashara yako, utaona fursa nyingi za kuifanya kuwa biashara bora kabisa kuwahi kutokea na kuwavutia watu bora kuja na kubaki.
Haya yote yanahitaji sana kazi kwa upande wako.
Kazi ambayo haina mwisho wala mapumziko.
Kazi namba moja kwako kwenye biashara inakuwa ni kupata watu bora na kuwafanya waendelee kubaki kwenye biashara yako.
Hiyo ni kwa washirika, wafanyakazi na wateja.
Ukiweza kutatua eneo la watu, utaweza kujenga biashara kubwa na bora kabisa.
Kuna njia za mkato ambazo watu huwa wanazitumia.
Moja ni ya tamaa, ambapo watu wanapewa kitu cha kuwafanya wasitake kuondoka.
Na mbili ni ya hofu, ambapo watu wanapewa mikataba ambayo hawapaswi kuivunja.
Njia hizi zinaweza kuwafanya watu waendelee kuwepo, lakini siyo wale bora.
Kwani walio bora wanaweza kupata tamaa kubwa zaidi pengine na kuvunja mkataba wowote unaoweza kuwa umewapa, kwani hata gharama za kuvunja mkataba huo zitakuwa tayari kulipwa na wengine wanaowataka.
Wafanye watu bora waje na kukaa kwenye biashara yako kwa muda mrefu kwa kuwapa fursa ya kuwa sehemu ya kujenga historia kubwa kwenye maisha yao.
Jenga biashara bora na ya kipekee kabisa, ambayo inawapa watu fursa nyingi ambazo hawawezi kuzipata mahali pengine.
Na kila wakati endelea kuwa bora na kubadilika ili kuondoa mazoea ambayo huwa yanawachosha watu.
Watu bora hawapatikani kirahisi na kuwatunza inahitajika kazi.
Kuwa tayari kuweka kazi hiyo ili uweze kujenga biashara kubwa na yenye mafanikio.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Unapaswa kujenga mahusiano na wale unaohusiana nao lakini pia kulinda maslahi yao kwa kuwafanya wasiwe na pengine pa kwenda ila kwako tu, hii ni kwa wateja, washirika na wafanyakazi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika na hilo linahitaji kazi kubwa sana.
LikeLike
Kila mara kubadilika ili kuondoa mazoea ambayo yanawachosha watu.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nitakuwa tayari kutafuta watu bora na kuwapa kile ambacho hawawezi kupata mahali pengine.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nahitaji sana watu bora katika
Ushirika wa kibiashara
Wafanyakazi bora
Wateja bora
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha kwa makala ya leo
Ili kuweza kupata watu bora na kukaa nao muda mrefu inanipasa mimi mwenyewe kuwa bora kwanza kwa kufanya yale yaliyo muhimu na bora kwenye maisha na biashara yangu ili kuwavutia wale walio bora kama mimi.
Nikishawapata nikuwaweka kwenye mchakato sahihi na kuwapa thamani kubwa ambayo itawafanya waendelee kuwa na mimi kwa muda mrefu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Watu Bora wanahitaji kazi sana.
LikeLike
Tena siyo kazi ndogo.
LikeLike
Ahsante sana Kocha🤝🤝
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Kweli kuwafanya watu wajisikie vizuri ni msingi mkubwa sana kwenye Mahusiano
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kupata watu Bora inahitaji kazi na siyo kazi rahisi, kuwatunza watu Bora inahitaji kazi zaidi hasa katika kuwa Bora na kuwahudumia Kwa ubora ambao hawawezi kupata pengine popote, Kwa kuwaonesha maono makubwa ya biashara na Kule tunapokwenda, kuboresha maisha yao na kujali Maslahi yao, kila siku watatamani kuendelea kuwepo na hata wakiondoka watatamani kurudi.
LikeLike
Kweli kabisa.
Tukae humo.
LikeLike
Kupata watu Bora ninahitaji niondoe mazoea,
Asante sana
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante sana Kocha, Nimejifunza kwamba ili wafanyakazi wasiende sio kwa kuwapa pesa nyingi tu au kwa kuwapunguzia bei wateja ktk bidhaa ambazo unauza. Kitu kikubwa kabisa ninachopaswa kufanya ni kuwafanya wajisikie vizuri.
Niwafanye wajione wapo sehemu salama na inayowapa nafasi ya kutoa mchango wao kwenye kitu chenye manufaa makubwa.
LikeLike
Vizuri sana, fanyia kazi.
LikeLike
shukrani sana kocha kwa makala bora kabisa. kuwafanya watu wajisikie vizuri,
wafanye wajione wapo sehemu salama na inayowapa nafasi ya kutoa mchango wao mkubwa
na kuacha hisitoria,hapo ni kwa washirika,wafanyakazi na wateja pia.
god blesss BM.
LikeLike
Vizuri sana,
Tukae humo.
LikeLike
Kujenga mahusiano Bora kuwajali wafanyakazi ,wateja na wadau wote kwenye lile eneo unalofanyia ka ni jambo la muhimu sana
Asante
LikeLike
Tuzingatie hayo.
LikeLike
Kweli kabisa kocha biashara ni Watu na kuwapata Watu walio Bora wa kufanya nao kazi kwenye biashara ni kazi pia
MBINU zinahitajika Ili kufanikisha kuwa na Watu Bora na kuimarisha biashara
LikeLike
Siyo rahisi.
LikeLike
Mafanikio ktk Maisha yanatokana na watu.
Hivyo unapojihushisha kitu muhimu unachopaswa kukifanya ni kuwafanya watu wajisikia vizuri kushiliana
na wewe na wajione wako sehemu salama na inayowapa
nafasi ya kutoa mchango wao.
Kwa kufanya hivyo itawafanya waendelee kuwa na wewe kwa muda mlefu.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Watu bora ni muhimu.
LikeLike
Sana
LikeLike
Kuwajali wateja washiriki na wafanyakazi ndiyo kipaumbele lakini pia kuwapa malipo mazuri na pia kuwauzia wateja vifaa kwa bei nzuri pia kuwapa mikataba ili wawe na uhakika
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Hakika Kocha.
Watu bora hawapatikani kirahisi na kuwatunza inahitajika kazi kwelikweli,ni kwa kujua mbinu stahiki za kuwafanya wabaki kwenye biashara zetu,ndiyo zitawafanya wasishawishike kwenda kwa wengine.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ili nipate watu Bora lazima na mimi niwe Bora zaidi.
LikeLike
Inaanza na wewe.
LikeLike
Asante sana kocha,kweli nahitaji watu bora,wafanyakazi,na wateja bora, lakini kwanza Mimi niwe bora zaidi kupitia kujifunza na kuwa chini ya usimamizi sahihi wa kocha.
LikeLike
Inaanza na wewe mwenyewe.
LikeLike
Na kweli hilo la mazoea lipo na ukipunguza thamani kama mlivyokubaliana tu basi anakuhama lna itachukua muda sana kumrudisha hivyo thamni ibaki palepale na ikiwezekana izidi
LikeLike
Kabisa
LikeLike