3040; Raha ya mchezo.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi huwa wanapenda kufuatilia michezo mbalimbali.
Japokuwa hakuna mtu anapenda kuona timu anayoshabikia ikifungwa, kama timu hiyo inaweza kushinda mara zote bila ya kusumbuka, mchezo hauwi na raha ya kuangalia.
Kadhalika sinema na maigizo mbalimbali.
Kama mhusika mkuu hakutani na changamoto mbalimbali kwenye safari yake, hainogi kuangalia.
Raha ya michezo mbalimbali ni ugumu ambao wachezaji wanakutana nao, uwezekano wa wao kushindwa.
Huo ndiyo unawasukuma kuweka juhudi zaidi ili kupata ushindi mkubwa.
Mchezo ukiwa rahisi sana watu hawafurahii kuuangalia, kwa sababu wanajua ushindi ni uhakika.
Na pia mchezo ukiwa mgumu sana watu wanakata tamaa kuuangalia, kwa sababu wanajua hakuna namna ya kushinda.
Hivyo raha kuu ya mchezo wowote ule ipo kwenye ugumu ambao upo ndani ya uwezo wa mku kuukabili.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu na mambo mengine yote tunayoyafanya.
Yakiwa rahisi sana yanatuchosha kufanya, maana hatupati msukumo wowote.
Na yakiwa magumu sana yanatukatisha tamaa, kwa kuwa tunaona hayawezekani kabisa.
Tunachohitaji ili kupambana na kujituma ni kiwango cha ugumu ambacho tukiweka juhudi tunaweza kupata matokeo ya tofauti.
Siyo rahisi sana kuwa na uhakika wa ushindi mara zote.
Na wala siyo ngumu sana kukosa kabisa tumaini lolote lile la ushindi.
Kwa upande mmoja tusikimbilie mambo rahisi tukidhani maisha yetu ndiyo yatakuwa ya raha.
Yatatuchosha haraka na kukosa maana.
Lakini pia tusijidanganye na mambo magumu sana ambayo hayawezi hata kufikiria, yatatukatisha tamaa.
Tuchague mambo yanayotusukuma kuwa bora kwa sababu ya nafasi iliyopo kwenye kushindwa, kisha tujisukume kuwa bora zaidi kwenye kuyafanya.
Na hata kama tunayopanga kufanya ni magumu sana, ili tusikate tamaa tuyagawe kwenye ngazi ambazo tunaweza kuzifikia.
Kwa kifikia ngazi kwa ngazi inakuwa rahisi kufikia chochote kigumu kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Tuchague mambo yanatotusukuma kuwa bora
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante Kocha raha ya mchezo wa biashara ni kufanya yale magumu lakini yapo ndani ya uwezo wetu kama kukaa kwenye mchakato kila siku
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Raha ya mchezo ni ule ugumu wake.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Raha ya mchezo ni kushinda, na kushinda kwetu ni kukamilisha mauzo. Tunakamilisha mauzo kwa kukaa kwenye mchakato wa mauzo.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Tusikimbile mambo rahisi.
LikeLike
Hayana thamani.
LikeLike
Raha ya mchezo ipo kwenye ugumu nikweli Asante sana kocha kwa makala mazuri
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitapambana siku na biashara kama mchezo bila kujali ni ugumu gani nakutana nao
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Raha ya mchezo ni ugumu Wake,
LikeLike
Tusikimbilie urahisi.
LikeLike
Tuchague yale yanayotusukuma kuwa bora
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Rahisi ni ghali tusikimbie rahisi ambayo haitadumu
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Raha ya mchezo ni ugumu wake, chochote unachokipata kwa ugumu unakithamini pia ila kile unachopata kirahisi hukithamini.
Hata kwenye MAUZO, MAUZO magumu ukiyakamilisha yanakupa raha kuliko mauzo rahisi.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Nitajituma ili kuvuka kiwango Cha ugumu kilichopo!
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Changamoto zipo ili kuniimarisha,ntayatumia magumu kama funzo ili niweze kuendelea na safar
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante Kocha,mambo rahisi
Yanatuchosha haraka na kukosa maana.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni kukabiliana na ugumu ndio mchezo unapendeza kwa watazamaji wakati biashara inakata mbuga kdg kdg
Shukrani kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha,raha ya mchezo ni ugumu uliopo kwenye mchezo husika , Asante sana kwa somo hili hasa pale ninapokuwa napambana na biashara yangu.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Raha ya mchezo ni ugumu ambao wachezaji wanakutana nao.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Machakato wa kitu ndiyo raha yenyewe
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Raha ya mchezo ipo katika ugumu
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Mchezo unakua na furaha pale unapokamilisha majukumu ya kupiga simu kutembelea kufuarilia na yale yahusuyo mchakato
LikeLike
Hakika
LikeLike
Raha ya huu mchezo ni kwamba ugumu wake unanipa hamasa ya kupambana na uwezekano Wa kufanikiwa ni mkubwa ninapokaa kwenye mchakato
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike