3060; Kuna vitu unafanya kwa usahihi.
Rafiki yangu mpendwa,
Takwimu nyingi za kibiashara zimekuwa zinasikitisha sana.
Biashara nyingi zinazoanzishwa huwa zinakufa ndani ya mwaka mmoja au miwili.
Vifo vya biashara hizo nyingi huwa vinatokana na changamoto mbalimbali ambazo waanzilishi hawakujua na kujiandaa nazo.
Lakini pia makosa, uvivu na uzembe vimekuwa vinachangia sana vifo vya biashara nyingi.
Kama umekuwa kwenye biashara moja kwa zaidi ya miaka miwili na haijafa, unatakiwa ujipongeze sana kwa sababu kuna vitu unavifanya kwa usahihi.
Unahitaji pongezi kubwa sana kama umeweza kuendesha biashara kwa zaidi ya miaka miwili bila ya kufa.
Haijalishi biashara ina ukubwa kiasi gani, kitendo tu cha kuweza kuwepo kwa zaidi ya miaka miwili bila kufa, ni cha kishujaa.
Kinachoua biashara nyingi ni mambo ya ndani na siyo ya nje ya biashara.
Wengi ambao biashara zao zinakufa hulalamikia sana hali ya uchumi, ushindani na changamoto nyingine kama sababu na biashara kufa.
Lakini ukweli ni sababu hizo za nje huwa zinamalizia tu kile kilichoanzia ndani.
Vifo vya biashara huwa vinaanzia ndani ya biashara yenyewe.
Uvivu, uzembe na tamaa vimesababisha vifo vya biashara nyingi.
Uvivu na uzembe ni kwenye ufanyaji wa mambo, huku tamaa ikiwa ndiyo inakuhamisha kibiashara na kukaribisha anguko.
Kwa mazingira yetu, kila wakati huwa kuna fursa mpya zinazokuja kila wakati.
Fursa hizo zinaonekana ni za muda mfupi na zinaisha kwa haraka, hivyo wengi wanaingia tamaa na kuzichangamkia.
Kinachotokea ni nguvu kupungua kwenye biashara kuu kutokana na umakini wa mtu kwenda kwenye kitu kingine.
Hilo linapelekea anguko kubwa la biashara.
Kwa wewe kuweza kukaa kwenye biashara kwa miaka zaidi ya miwili ni kitu kikubwa unachopaswa kukithamini.
Kuna mambo mazuri na sahihi sana unayoyafanya na ndiyo yanayosababisha biashara kuweza kuendelea kuwepo, licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.
Lakini basi, kuwa na vitu ambavyo umekuwa unavifanya kwa uzuri na usahihi haimaanishi umeshamaliza kila kitu.
Bali inamaanisha una kazi kubwa mbele yako ya kuvuka uzuri uliopo ili kufikia ubora zaidi.
Wanasema adui wa ubora ni uzuri.
Chochote mtu anachofanya vizuri huwa ni vigumu sana kujisukuma na kufanya kwa ubora.
Kwa sababu matokeo mazuri anayopata mtu huwa yanamlevya na kuona hana haja ya kubadili.
Matokeo mazuri ambayo umekuwa unayapata ndiyo yamekuwa kikwazo kwako kupata matokeo bora zaidi.
Ni kama umejiwekea ukomo kwenye matokeo unayokuwa unayapata.
Njia pekee ya kujinasua kwenye hilo ni mtu kuwa tayari kuboresha yote mazuri yanayofanyika.
Kwa kuangalia namna ya kufanya kwa ubora zaidi yale unayofanya kwa uzuri, utaziona fursa za ukuaji zaidi.
Zoezi muhimu la kufanya;
1. Orodhesha vitu vyote ambavyo umekuwa unafanya kwa uzuri na ubora kwenye biashara yako.
2. Kwa kila ulichoorodhesha, andika ni jinsi gani kimekuwa kikwazo kwako kukua zaidi ya hapo.
3. Weka mkakati wako wa ukuaji kibiashara kwenye maeneo yote ambayo tayari upo vizuri ili uweze kuwa bora kabisa.
Kilichokufikisha hapo ulipo sasa siyo kitakachokupeleka kule unakotaka kufika kesho.
Hili ni muhimu kulielewa na kuzingatia mara zote ili kuweza kujenga biashara inayoweza kukua na kufikia malengo makubwa.
Lakini hayo yote yanaanzia kwako wewe mwenyewe kwa kutambua na kujikubali kwa yale unayofanya vizuri, kisha kupata msukumo wa kuyafanya kwa ubora wa hali ya juu kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Uzuri ni kikwanzo cha ubora.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Vifo vya biashara huwa vinaanzia ndani ya biashara yenyewe.
Uvivu, uzembe na tamaa vimesababisha vifo vya biashara nyingi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Matokeo mazuri ambayo ninayapata ndio yamekuwa kikwazo kwangu kupata matokeo bora zaidi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
KUSHINDA UVIVU,UZEMBE NA TAMAA
ILI BIASHRA IWEZE KUKUA ZAIDI
KWA CHUKUA HATUA ZA TOFAUTI BILA
MAZOEA KILA JUKUMU.
asante kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Najipongeza kukaa zaidi ya miaka miwili kwenye biashara ya Restaurant, Kuna vitu nafanya vizuri, nakwenda kuboresha mbinu zilizonifikisha hapa Ili kuvuka ukomo Wa mazoea na kufika Kule ninapotaka kwenda…Chain and franchises Restaurants
Adui Wa ubora ni uzuri… napambana kuwa Bora zaidi nakataa kuwa Wa kawaida
LikeLike
Hongera sana na kila la kheri.
LikeLike
Uvivu, uzembe umeua biashara nyingi.
Matatizo mengi ya biashara huwa yanaanzia ndani.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Biashara yangu Ina mwaka mmoja na nusu lakini nina malengo, naimani nitaifikisha na kuivusha miaka miwili, muhimu ni kuendelea kujifunza zaidi na kuweka mifumo bora ya kufuata.
Asante kocha.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha, nitauzidi uzuri ili kuongeza ubora.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Lazima nielewe kuwa. Kilichonifikisha hapa nilipo sasa siyo kitakachonipeleka kule ninakotaka kufika kesho.✍️
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Vifo vya biashara vinaanzia ndani ya biashara.
Kama Uvivu, uzembe, tamaa .
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitajitahidi kuepuka uvivu, uzembe na tamaa. Asante kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana kocha kilicho nifikisha hapa nilipo sio kitakacho nifikisha kule ninakotaka kufika kwa hiyo nitaacha mazoea,uvivu,uzembe na tamaa
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Notaepuka uvivu, uzembe na tamaa ili kuiepusha Biashara yangu na kifo
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa kuwepo zaidi ya miaka 2 kwenye biashara ninayofanya maana yake Kuna mzuri na bora ninayoyafanya. Hivyo Leo ninaorodhesha yote haya ninayofanya kw Uzuri na ubora ili niweze kuyathmini, ili niweze kuyafanya kwa viwango vya juu na biashara yangu iweze kukuwa na kunipa faida kubwa zaidi.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike
Matokeo mazuri ni sehemu ya kumlevya mmiliki na asiweze kuwaza namna ya kusonga mbele tuangalie maeneo tunayofanya vizuri na kuona namna ya kuyabadili yawe bora zaidi ya hapo
LikeLike
Tuepuke sana huo ulevi.
LikeLike
Vifo vya biashara huwa vinaanzia ndani ya biashara yenyewe.
Uvivu, uzembe na tamaa vimesababisha vifo vya biashara nyingi.
Asante san
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kilichonifikisha hapa nilipo sasa siyo kitakachonipeleka kule ninakotaka kufika kesho.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Uvivu na uzembe ndio sumu ya kuua haraka Biashara na tabia za kitajiri, Kila siku naweka mikakati na mazoea ya kusjonda haya.
Zoezi linafikirisha sana kwa namna fulani najizuia kukuwa, mabadiliko ni sasa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana Kwa MAKALA ya leo nimefanya tathimin ya biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Uvivu,uzembe na tamaa vinasababisha vifo vya biashara nyingi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Sitakubali matokeo mazuri yawe kikwazoi kwangu kupata matokeo bora kabisa
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Uvivu ,uzembe na tamaa ndio vitu vinavyoua biashara ,nimechagua kufanya biashara moja kwanza hadi nione matokeo,bila kukimbilia biashara nyingime kwa tamaa ya kupata fedha zaidi kumbe ndio naenda kuuwa biashara yangu
Naacha uzembe na uvivu ili kuhakikisha nakuza hii biashara niliyonayo
Yale mazuri ninayofanya sasa kwenye biashara nitaendelea kuyaboresha kwa ukubwa ili niendelee kuwa bora zaid na kukuza biashara.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
NHitaji mfumo wa biashara
Nahitaji timu imara na weledi
Nahitaji kuwekeza mtaji ili kuwe na huduma ya uhakika na bidhaa isiyoisha
Nahitaji Kusaka wateja wengi zaidi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Uvivu, uzembe na tamaa vimesababisha vifo vya biashara. Naacha uzembe na uvivu Ili kuhakikisha nakuza biashara.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kinachoua biashara nyingi Ni mambo ya ndani ya biashara na siyo ya nje.
Mambo hayo ni kama uvivu uzembe na tamaa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,nitajisukuma kwa nguvu zote na ubora wa juu,ili nikuze biashara na kuacha uvivu na tamaa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitafanya biashara kwa miaka 50 na kwa hii miwili imebaki 48 Lazma itatoboa tu,Uvivu uzembe na tamaa ctovipa nafasi
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
adui wa ubora ni uzuri
LikeLike
Kabisa.
LikeLike