3071; Maamuzi na utekelezaji.
Rafiki yangu mpendwa,
Tunajua jinsi ambavyo wanaoyataka mafanikio ni wengi, lakini wanaoyapata wakiwa wachache sana.
Tumeshajifunza sababu nyingi zinazowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Hapa tunakwenda kuangalia eneo moja ambalo siyo kwamba halifanyiki kabisa, bali halifanyiki kwa usahihi.
Eneo hilo ni kufanya maamuzi na utekelezaji wa maamuzi hayo.
Watu wasiofanikiwa huwa wanachelewa sana kufanya maamuzi.
Na hata wakishayafanya, hawayawekei mkazo kwenye utekelezaji.
Na wapo haraka sana kwenye kuvunja maamuzi hayo pale wanapokutana na magumu.
Kwa njia hii, wanafanya mengi, lakini hawafanikiwi.
Mafanikio yanataka vitu vitatu vifanyike kwa uhakika kwenye eneo la maamuzi.
Moja ni maamuzi kufanyika haraka.
Mbili ni maamuzi kutekelezwa kwa juhudi kubwa.
Na tatu ni maamuzi kutekelezwa kwa msimamo bila kuacha.
Ni muhimu sana kufanya maamuzi haraka kwa sababu huwa kuna dirisha dogo sana la muda wa kunufaika na fursa yoyote inayokuwa imejitokeza.
Wengi huchelewa kufanya maamuzi kwa sababu wanasubiri mpaka wawe tayari kwa kila kitu.
Kusubiri uwe tayari ni kujichelewesha na kujipotosha.
Unapaswa kufanya maamuzi kwanza halafu kuendelea kujiandaa kadiri unavyokwenda.
Kama kitu ni muhimu, fanya maamuzi hata kama bado hujawa na maandalizi ya kila kitu.
Ukishafanya maamuzi, kinachofuata ni kuyafanyia kazi kwa uhakika.
Wengi wakishaamua wanakuwa kama wanajaribu.
Hawaweki juhudi zao zote kwenye maamuzi waliyofanya.
Badala yake wanakuwa kama wanabahatisha.
Kinachotokea ni wanakutana na magumu na changamoto, ambazo zinawayumbisha sana.
Chochote unachoamua, lazima ukifanyie kazi kwa juhudi kubwa sana, hata kama huna uhakika nacho.
Fanya kila kinachopaswa kufanyika ili maamuzi uliyofanya yazalishe matunda mazuri.
Msimamo kwenye kutekeleza maamuzi yaliyofanyika ni kitu ambacho kinakosekana sana kwa walio wengi.
Wengi hufanya maamuzi kwa kuchelewa, hawayafanyii kazi kwa uhakika na pale wanapokutana na vikwazo au changamoto, wanaacha kufanya.
Kama kukutana tu na changamoto kunakukatisha tamaa na unaacha, hautaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote lile.
Kwa sababu magumu, vikwazo na changamoto ni sehemu ya safari ya mafanikio.
Na kwa sababu unafanya maamuzi kwa haraka, kuna mengi utakuwa huna maandalizi nayo.
Unatakiwa kuwa na msimamo mkali sana kwenye kuyatekeleza maamuzi uliyoyafanya.
Umefanya maamuzi kwa sababu kuna matokeo unataka kuyapata, usivunje maamuzi hayo kama hujapata matokeo uliyotaka.
Unachoweza kufanya ni kuendelea kuboresha kadiri unavyokwenda.
Unapoyafanyia kazi maamuzi yoyote yale kwa msimamo bila kuacha, unajiweka kwenye nafasi ya kupata matokeo bora.
Ni hayo ya msingi kabisa kwenye maamuzi,
Fanya maamuzi haraka, usisubiri mpaka uwe umekamilika.
Weka juhudi kubwa kwenye maamuzi unayofanya, usijaribu, fanya kwa uhakika.
Kuwa na msimamo kwenye kufanyia kazi maamuzi yako, usiache kwa sababu ya changamoto, badala yake endelea kama ulivyoamua, matokeo mazuri huwa yapo mbele.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante kocho . Nitakuwa na maamuzi sahihi na kuchukua hatua mara Moja.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Unapofanyia kazi maamuzi yoyote yale kwa msimamo bila kuacha unajiweka kwenye nafasi ya kupata matokeo bora
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Weka juhudi kubwa kwenye maamuzi unayofanya, usijaribu, fanya kwa uhakika.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitafanyia kazi maamuzi kwa haraka bila kujata tamaa wala sitasubiri mpaka kila kitu kikamilike.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nakwenda kufanya maamuzi kwa haraka na sitosubiri mpaka nime mimekamikika.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Maamuzi ndio kitu pekee ambacho ni Muhimu sana katika kufikia ndoto kubwa za maisha yangu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mtapambana na maamuzi haya matatu mara zote katika kutimiza malengo kwenye maisha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Maamuzi na utekelezaji, hapa ndiyo mahali wengi tunakwama. Nitajitahidi kulifanyia kazi eneo hili. Asante kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitafanyia kazi maamuzi na Utekelezaji kwa haraka
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitafanya maamuzi kwa haraka, sitasubiri niwe nimekamilika. Nitayafanyia kazi maamuzi hayo kwa juhudi na msimamo mkali. Nitakaa kikamilifu kwenye mchakato, sitahangaikia matokeo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Maamuzi na utekelezaji
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Chochote unachoamua kukifanya lazima ukifanye kwa juhudi kubwa sana hata kama huna uhakika sana. Magumu, vikwazo na changamoto ni sehemu ya maisha.
Nimekuelewa kocha nitafanyia kazi hili.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Maamuzi kufanyika haraka, kutekelezwa kwa juhudi kubwa na kutekelezwa kwa msimamo bila kuacha.
Asante sana Daktari Makirita Amani
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nakuwa na msimamo sahihi kwenye kufanyia kazi maamuzi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Dawa imewekwa Kwa kidonda
LikeLike
Safi.
LikeLike
Nitafanya maamuzi haraka na kuyatekeleza kwa msimamo.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Fanya maamuzi haraka usisubiri mpaka uwe umekamilika.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ukishafanya maamuzi, kinachofuata ni kuyafanyia kazi kwa uhakika.
Ni utekelezaji tu hakuna kingine
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya maamuzi na kuyatekeleza mara moja kwa msimamo.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Hakuna kufanya kwa kujaribu, ninaamua haraka na kufanya kwa uhakika mkubwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
asante sana,
usichelewe kuamua,na fanya ukisha amua
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Maaamuzi magumu, kuweka nguvu kwenye maamuzi bila ya kukata tamaa ndio Siri ya mafanikio yangu
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Hili limenikumbusha mbali sana siku moja nilitakiwa kulipia hela ajili ya kununua kiwanja fulami nikasema ngoja nijazie hela kilichotokea mwenzangu akapita nayo naenda kulipa nakuta kulipa nakutana na mikataba kumbe nilichokosa tu ni maamuzi na wakati mwinginee nakosa maamuzi kwa kua sijajiandaa kumbe maamuzi yanatakiwa yawe ni ya haraka na tena kuja kurekebisha baadae ili kupata matokeo mazuri
LikeLike
Ukishaamua, unatakiwa kutekeleza mara moja, kusubiri ni kujichelewesha.
LikeLike