3113; Una kitu, utafika mbali.
Rafiki yangu mpendwa,
Leo nataka nikupe maua yako, nikupe sifa kwa vitu ulivyonavyo, ambavyo ukiamua kuvitumia vizuri, utafanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Ni vitu ambavyo unaweza kuwa unavichukulia kawaida, lakini kama utavipa uzito, utaweza kufikia malengo makubwa uliyonayo.
Wewe kuwa hai mpaka sasa ni kitu kikubwa sana, ambacho ukiamua kukitumia vizuri, utafika mbali.
Sihitaji kuelezea sana umuhimu wa uhai, tunajua kabisa hakuna unachoweza kufanya ukiwa umekufa.
Lakini ukiwa hai, unakuwa na muda na nguvu za kufanya mambo.
Kama utalinda muda na nguvu hizo zisipotee na kuweka kwenye mambo sahihi, hutaweza kubaki hapo ulipo sasa.
Wewe kuwa na watu ambao tayari wanakuamini ni kitu kikubwa, ambacho ukikitumia utafika mbali. Mpaka sasa kuna watu ambao unashirikiana nao, ambao wanakuamini. Inaweza kuwa watu wako wa karibu, wateja kwenye biashara na wengine wanaokuzunguka.
Mafanikio huwa yanahitaji sana watu, ukiendelea kufanya yale yanayopelekea uaminike, utaweza kuwashawishi wengi na wakawa njia ya wewe kupata unachotaka.
Umeanzisha biashara ambayo mpaka sasa inakwenda. Hata kama biashara hiyo haijapata mafanikio makubwa, lakini umekuwa na uthubutu wa kuanzisha na umepambana nayo mpaka pale ilipofika sasa. Ni kitu kikubwa sana ambacho unacho, ambacho siyo wengi wanacho. Wengi hawana uthubutu wa kuanzisha biashara, licha ya kutaka sana. Na hata wale wanaoanzisha, wengi biashara hizo zinakufa ndani ya muda mfupi baada ya kuanzisha.
Wewe kuwa kwenye biashara kwa kipindi ambacho umekuwepo, ni kitu kikubwa, kitumie vizuri na utafika mbali zaidi.
Wewe kuwa na malengo makubwa ya kufikia ubilionea ni kitu cha kipekee sana. Swala tu la kufikiri ni kitu unachoweza kukifikia, linakutofautisha na wengi sana ambao wanaona ni kitu kisichowezekana kabisa. Hicho ni kitu kikubwa ulichonacho, ambacho ukikitumia vizuri, kwa kuendelea kuamini unaweza na kuchukua hatua, lazima utafikia lengo hilo.
Wewe kuwa ndani ya jamii bora kabisa ya KISIMA CHA MAARIFA na BILIONEA MAFUNZONI ni kitu kikubwa sana, ambacho ukikitumia vizuri, utafika mbali sana. Ni wengi sana wanatamani kuwa kwenye jamii ya aina hii lakini hawapati nafasi hiyo ambayo umeipata wewe. Ithamini nafasi hiyo na kuifanyia kazi kwa uhakika ili upate mafanikio makubwa unayoyataka.
Rafiki, haya niliyogusia hapa ni machache sana kati ya mengi mazuri ambayo tayari unayo.
Ninachotaka ni kukukumbusha kwamba tayari una kitu ndani yako, usijichukulie poa.
Lakini chochote ulichonacho ndani yako hakitakuletea matokeo yoyote chenyewe.
Bali unahitajika kukifanyia kazi kwa uhakika ndiyo kiweze kuzalisha matokeo makubwa.
Dhana kubwa sana ambayo nataka wote tuondoke nayo hapa ni kila mtu ana zawadi za kipekee alizonazo.
Wengine wanaita uwezo mkubwa, wengine wanaita vipaji.
Lakini ukweli ni kila mtu kuna vitu anaweza kufanys vizuri kuliko watu wengine.
Anakuwa na msukumo wa kufanya bila ya kuchoka, hata kama hakuna anayemlipa.
Wajibu wako mkubwa kwenye safari yako ya mafanikio ni kujua vitu ambavyo wewe unaweza kuvifanya kwa ubora kuliko watu wengine, unapata msukumo wa kuvifanya bila kuchoka hata kama hakuna anayekulipa.
Hivyo ndiyo vitu ambavyo unapaswa kuvifanya kwa ukubwa zaidi ili upate mafanikio makubwa unayoyataka.
Vingine waache wengine wafanye, wewe komaa na hivyo ambavyo una upekee navyo.
Uzuri ni kwamba, wewe tayari unao huo uwezo wa kipekee, una vitu unavyofanya kwa ubora kuliko watu wengine wote.
Hicho ndiyo kitu ambacho unacho, hivyo basi, unapaswa kukitumia vizuri ili uweze kufika mbali zaidi.
Fanya zaidi vitu ambavyo uko vizuri zaidi kwenye kuvifanya na utaweza kufanya makubwa zaidi.
Epuka kuiga wengine au kushindana nao.
Hapo unaacha kitu chako na kuhangaika na vitu vya wengine, kitu kitakachopelekea ushindwe vibaya sana.
Cheza kwenye uwanja wako wa nyumbani, kwa kutumia kile ambacho tayari kipo ndani yako.
Kwenye maoni hapo chini tushirikishe ni kitu gani cha kipekee unacho na unakitumiaje kufika mbali zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Uzuri ni kwamba tayari wewe unao uwezo wa kipekee, una vitu unavyovifanya kwa ubora kuliko watu wengine wote.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kufanya biashara kwa ubora mkubwa na tutafika mbali kwa maarifa baya yaliyopo kwenye jamii yetu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ninauwezo mkubwa Wa kuhimili changamoto za biashara bila kukata tamaa naendelea kujifunza Ili kuzibadili changamoto zangu kuwa fursa…nitapata ninachokitaka au nitakufa nikiwa nakipambania kurudi nyuma mwiko, mbele daima
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Wajibu wangu kwenye safari ya mafanikio ni kuchagua yale ninaweza kufanya kwa ubora, kubobea humo hata kama hakuna anayenilipa kwa kuyafanya hayo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kitu cha kipekee nilichonacho ni uthubutu wa kuchukua hatua kwa kila wazo ninalopata katika kuhakikisha biashara ninayofanya inafikia viwango vikubwa kwa kuhudumia watu wengi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kitu cha pekee nilichonacho na nakitumia kama siraha ni uvumilivu wa kuthubutu na ķuendelea kufanya hata kama sioni matokeo ya haraka
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nikufanya biashara kwa ubora wa Hali ya juu nakutumia haya maarifa ninayoyapata hapa ili kufikia lengo
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kitu cha pekee ambacho ninacho ni uthubutu wa kuamua na kufanya kitu, na pia kutumia maarifa haya kwa usahihi Ili niweze kujenga biashara bora kabisa kuwahi kutokea.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kuwa hai ni Zawadi ya kipekee
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha kwa kutukumbusha hili. Kuna wakati mambo yanakuwa magumu mpaka unatamani unyoshe mikono, kumbe pamoja na magumu tunayokutana nayo, kitendo tu cha kuwa hai,kinatakiwa kutupa sababu ya kuendelea.
Kitu nilichonacho sina uhakika kama ni cha pekee lakini kimekuwa kinanisaidia ni kutokata tamaa. Sijawahi kuishia njiani kwenye michakato yote muhimu niliyopitia, hii imekuwa inanipa nguvu ya kusonga mbele licha ya magumu ninayokutana nayo, huwa najiambia kama hiyo ya nyuma iliwezekana, huu pia utawezekana.
LikeLike
Hicho ni kitu kikubwa sana.
Maana zama hizi watu ni rahisi sana kukata tamaa.
LikeLike
Kitu Cha kipekee kwangu kutokuogopa hatari kudhubutu kufanya vitu vyenye hatari lakini vinavyoleta matokeo makubwa
LikeLike
Safi sana, tumia hicho na utafika mbali.
LikeLike
Asante Kocha. Kweli kila mtu anakitu, na kama akiamua kukitumia anafika mbali.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nitautumia vizuri uwanja wa nyumbani kufunga magoli ya ushindi
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kitu pekee ambacho ninacho ni uwezo wa kuandika, kujifunza, kufundisha na uwezo wa kuuza na nitavitumia hivi kusaidia jamii na kufika mbali zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Uzuri nina ujuzi, maarifa na connection zinazokuwa kila siku na nina utayari wa kupokea na kutoa thamani kubwa na adimu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kitu cha kipekee kwangu huwa sipo tayari kukata tamaa hata kama mambo yawe magumu huwa naamini yatakua mazuri tu,kwenye biashara yangu pamoja na kupitia changamoto nyingi lakin bado naamin kuna siku zitapita na nitakua nimejenga biashara imara sana.
Asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ninauwezo wa kufanya Jambo lolote kwa namna niyotaka na nikalitimiza . Hivi Sasa ninatumia uwezo huo kukamilisha yote niliyodhamilia kuyafikia.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kuaminiwa na wateja ni kitu muhimu.sana.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Uthubutu mkubwa ulio Ndani yangu na imani kubwa ya kufanya makubwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Hakika ni ubora
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Uaminifu hasa ktk mambo ya fedha, Kupiga Mahesabu ( kuchakata data ), Kuwa zaidi ya wengine ( Ushindani ktk biashara kwa maana kuwa price leader in the market ).
LikeLike
Vizuri sana, yatumie haya vizuri na yatakufikisha mbali sana.
LikeLike
Kitu cha pekee kwangu Ni Mchezo wa namba, Kuangalia Namba za biashara zinasemaje. Mapato na Matumizi, Faida na hasara, Lengo la namba linafikiwaje na kwa muda gani.
LikeLike
Vizuri sana, tumia hicho kufika mbali.
LikeLike
Kitu cha pekee ni kifuatilia watu na kiona watu wa kibadilika kwa sehemu kubwa
LikeLike
Vizuri, kitumie vyema kufika mbali.
LikeLike
Kitu pekee kwangu ni kutoa HUDUMA BORA Kwa wateja hapa nasimama upande WA WATEJA kuona HUDUMA ninayoitoa inamchango gani kwao,
LikeLike
Vizuri, tumia hicho kufika mbali zaidi
LikeLike
Kitu Cha kipee nilichonacho ni kupata msukumo wa kuanza mapema pale wazo jipya linapo nijia la kufanya kitu kisipo fanyika nakosa utulivu
LikeLike
Vizuri sana, tumia hicho na utafika mbali zaidi.
LikeLike
Kuwa na nidhamu ya kuwekeza kwa msimamo bila kuacha, pia nidhamu ya kuhakikisha fedha nilizopanga kwa ajili ya matumizi fulani sizigusi kwa matumizi mengine.
Na kusoma vitabu.
LikeLike
Vizuri sana, tumia hicho na utafika mbali.
LikeLike
Kitu kikubwa nilichonacho na ninachokipenda,ni kufuatilia, kupitia masoko na mauzo, napenda sana kuuza
LikeLike
Vizuri, kitumie ili kufika mbali zaidi.
LikeLike
Asante Sana kocha Mimi upekee wangu ni 1. Ung”ang”anizi, uvumilivu na uhudumiaji
LikeLike
Vizuri, utumie upekee huo kufanya makubwa zaidi.
LikeLike
Mapinduzi ya kibiashara niyofanya na kujenga timu, mifumo na mpangilio ili kuweza kufanya makubwa
LikeLike
Fanya kwa uhakika.
LikeLike
Kitu cha kipekee kwangu na ninajivunia kuwa nacho ni uvumilivu na ung’ang’anizi,huwa sipo tayari kukata tamaa pale changamoto zinapojitokeza,zaidi ninajifunza kwenye changamoto hizo na kusonga mbele.
LikeLike
Vizuri, tumia hayo kufanya makubwa zaidi.
LikeLike
Nashukur kuwa hai, Nimekuwa Najifunza taratibu na najivunia Uvumilivu nilio nao kwenye kupgania ndoto zangu na ninaamini nitafka mbali Sana
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Kitu pekee ni kuishi dunia i kwa kujua kwa nini yangu,kujua kile nilichoitiwa na kupenda kufanya kwa kua nimependa sijalazimishwa.Nitakua nasimamia ndoto yangu bila kukatishwa tamaa na kelele zozote.Ung’ang’anizi kufikia ndoto zangu na kuziishi duniani hapa
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike