3137; Hivi kesho jua litachomoza?
Rafiki yangu mpendwa,
Hebu fikiria kama hilo ndiyo swali ambalo ungekuwa unajiuliza kila siku kabla ya kulala, iwapo jua litachomoza au la.
Fikiria ingebidi ujiulize hivyo kwa sababu jua linakuwa halieleweki, kuna siku linachomoza na kuna siku halichomozi kabisa au linachelewa.
Unadhani maisha yako yangekuwa sawa na yalivyo sasa?
Kwa hakika majibu ni hapana.
Kuchomoza na kuzama kwa jua kila siku ni kitu ambacho tuna uhakika wa kutokea kwake.
Hivyo mipango yetu yote tunaiweka kulingana na hali hiyo.
Na tunapanga hivyo kwa kujiamini, kwa sababu tuna uhakika wa huo mwenendo wa jua.
Kadhalika vitu vingine vingi kwenye asili vinaenda kwa mfumo huo, uhakika wa kutokea kwake.
Vitu vyote ambavyo tuna uhakika wa kutokea kwake, huwa tunavitegemea kwa uhakika.
Huwa hatuwi na wasiwasi wowote kuhusu kutokea kwake, kitu kinachotupa utulivu mkubwa.
Moja ya vitu ambavyo sisi binadamu tunavipenda sana ni uhakika.
Chochote ambacho tunaweza kuwa na uhakika nacho, tunakithamini zaidi.
Hilo pia linaenda hivyo kwa watu.
Watu ambao tunaweza kuwa na uhakika nao na kuwategemea kwenye yale wanayopaswa kufanya, ni watu ambao huwa tunawathamini zaidi.
Kwenye dunia ambayo ina uhaba mkubwa wa watu ambao wanaweza kutegemewa kwa uhakika, kuwa hivyo ni faida kubwa sana kwa mtu na njia itakayompa mafanikio makubwa.
Asilimia 99 ya watu hawawezi kutegemewa kwa uhakika kwenye jambo lolote lile.
Ni watu ambao hawawezi hata kutimiza mambo waliyoahidi wao wenyewe.
Na pale wanapopewa jukumu lolote la kukamilisha, wanalikamilisha kwa kiwango cha chini sana, kama hata watakamilisha kabisa.
Ni asilimia 1 tu ya watu ndiyo wanaoweza kutegemewa kwa uhakika kwenye jambo lolote lile.
Hawa ndiyo wanaotekeleza kila wanachopanga na wakipewa jukumu wanakamilisha kama wanavyotegemewa.
Na ni asilimia hiyo 1 ndiyo wanaopata mafanikio makubwa kwenye maisha yao.
Njia pekee ya wewe kuweza kuingia kwenye asilimia 1 ya watu wanaofikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao ni kutengeneza hali ya kuaminika na kutegemewa kwa uhakika na bila shaka yoyote.
Hapo unapaswa kuwa kama jua, mambo yako yote yanategemewa kwa uhakika.
Unatimiza kila unachoahidi mara zote.
Unahudhuria kwenye mambo yote kama unavyotegemewa.
Na unazalisha matokeo makubwa mara zote kwa uhakika kabisa.
Kuweza kutegemewa kwa uhakika mara zote kutakutofautisha sana na wengi ambao hawaeleweki nini wanafanya kwenye maisha yao.
Wengi wanaahidi vitu ila hawatekelezi na hilo wala haliwaumizi kwa namna yoyote.
Mahudhurio yao kwenye maeneo wanayotegemewa kuwa huwa siyo ya uhakika, sababu za kutokuhudhuria huwa ni nyingi.
Na matokeo wanayozalisha ni ya chini sana, kama hata watazalisha matokeo kabisa.
Unaweza kujionea mwenyewe kwa nini watu wengi hawajafanikiwa na hawataweza kufanikiwa.
Hilo linakuacha wewe na njia moja ya uhakika ya kuweza kupata mafanikio yoyote makubwa unayotaka kuyapata.
Njia hiyo ni KUWEZA KUTEGEMEWA KWA UHAKIKA MARA ZOTE.
Timiza kila unachoahidi, kwa kwenda hatua ya ziada.
Hudhuria zaidi ya unavyotegemewa kuhudhuria, mara zote kwa wakati na hata pale unapokuwa na sababu ambazo zingeweza kukuzuia usihudhurie.
Mara zote zalisha matokeo bora kabisa, zaidi ya inavyokuwa inategemewa.
Mambo hayo matatu ya kuzingatia hayaangalii umri wako, jinsia wala kiwango chako cha elimu.
Na ndiyo maana watu wa kila aina wanafanikiwa, bila ya kujali umri, jinsia au elimu.
Ufunguo wako wa mafanikio makubwa na ya uhakika upo kwenye mikono yako, ambapo ni KUTEGEMEWA KWA UHAKIKA.
Jijengee sifa ya kutegemewa kwa uhakika bila ya shaka yoyote ile na utaweza kupata chochote unachotaka.
Kuwa kama jua, tegemewa kwa uhakika kwenye mambo yako yote.
Ni sifa nzuri sana ya kuwa nayo kwenye zama ambazo wengi hawawezi kutegemewa kwa uhakika kwenye jambo lolote lile.
Kuweza kutegemewa kwa uhakika kunayafanya maisha ya watu wengine kuwa rahisi.
Watu wanapenda kujihusisha na wale wanaoyafanya maisha yao kuwa rahisi.
Hivyo unajionea hapo jinsi njia ya mafanikio makubwa ilivyo ya uhakika.
Siyo rahisi, lakini inawezekana.
Moja ya njia za kujijengea sifa ya kutegemewa kwa uhakika bila ya shaka yoyote ni kuwa na mchakato ambao tunaufuata mara zote kwa msimamo bila kuacha.
Kwa kuuweka mchakato wetu huo wazi kwa watu wote na kuutekeleza mara zote bila kuacha, kunakujengea sana sifa hiyo ya kutegemewa kwa uhakika.
Unapoenda hatua ya ziada katika kutekeleza mchakato wako hata pale mazingira yanapokuwa magumu, kunakujengea imani na heshima kubwa sana.
Unapoweza kutekeleza kila unachoahidi, kwa kufanya kila neno lako kuwa ndiyo sheria ambayo huivunji.
Kwa kuhudhuria mara zote na kwa wakati bila kuruhusu sababu au visingizio vyovyote kuwa kikwazo.
Ukiwa unazalisha matokeo bora zaidi kadiri unavyoendelea kwenda.
Kinachokuwa kimebakia ili kupata chochote unachotaka ni muda tu.
Hakuna kingine chochote kinachoweza kuwa kikwazo kwako.
TEGEMEWA KWA UHAKIKA NA BILA YA SHAKA YOYOTE na utaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ninajenga sifa ya KUTEGEMEWA KWA UHAKIKA NA BILA YA SHAKA YOYOTE na nitaweza kupata chochote ninachotaka kwenye maisha yangu.
Asante sana
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha. Nitatengeneza hali ya kuaminika na kutegemewa kwa uhakika na bila shaka yoyote.
Ninapaswa kuwa kama jua, mambo yangu yote yawe yanategemewa kwa uhakika.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nahitaji kuhakikisha nakuwa mtu wa kutegemewa kama asili, mara zote nakuwa mtu wa uhakika hata pale ambapo wengi walitarajia tofauti.
LikeLike
Nitaweka juhudi kuhakikisha nategemewa kwa uhakika ili kufanya maisha ya wengine kuwa rahisi
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kuwa na uhakika kwa kutegemewa bila ya Shaka ni kitu muhimu katika mafanikio.Najaribu kuwaza vipi kwa mtu ambaye labda ni mwajiriwa au ni mfanyabiashara ambaye watu wamejijengea kumtegemea hadi kwenye majukumu madogo madogo kiasi cha kwamba akawa anazidiwa na majukumu au labda kuwafanya wengine kazini au kwenye biashara kutokujituma kwa kujua yupo fulani ambaye atashughulika na kila kitu?
LikeLike
Hilo si ndiyo zuri? Kwa sababu linakupa nguvu ya kutaka ulipwe zaidi na kwa sababu watu wanakutegemea zaidi, hawatataka kukupoteza, hivyo watakulipa zaidi.
Kutegemewa kwa mengi ni manufaa makubwa, ndiyo kutakupa majukumu mengi, lakini pia kutakupa nguvu kubwa ya kuchagua nini unataka.
Tukae zaidi upande huo.
LikeLike
Ni asilimia 1 tu ya watu ndiyo wanaoweza kutegemewa kwa uhakika kwenye jambo lolote lile.
Hawa ndiyo wanaotekeleza kila wanachopanga na wakipewa jukumu wanakamilisha kama wanavyotegemewa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuweza kutekeleza kila unalopanga na kuahidi na kuweka mipango yako wazi
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha kweli tunahitajia tujijengee sifa ya kutegemewa kwa uhakika bila ya shaka yoyote ile na tutaweza kupata chochote tunachotaka.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Mara zote nitajenga hali ya Kutegemewa kwa uhakika bila ya shaka yoyote.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitahakikisha nategemewa kwa wakati wote na kujitahidi kutowaangusha wengine.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitajenga uaminifu kuhakikisha kuwa nategemewa bila ya shaka yoyote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitajitahidi kufanya kila kitu kama nilivyoahidi na kutengeneza mazingira ya kutegemewa. Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kutegemewa Kwa uhakika Kwa kile unachokifanya ni jambo Bora sana kufikia mafanikio tunayoyataka.
Ili kufikia hapo ni kukaa kwenye mchakato bila ya kuweka sababu
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kutegemewa Kwa uhakika Kwa kile unachokifanya ni jambo Bora sana kufikia mafanikio tunayoyataka.
Ili kufikia hapo ni kukaa kwenye mchakato bila ya kuweka sababu
Asante sana
LikeLike
Natakiwa kuanza kujijengea tabia ya kutegemewa kwa uhakika bila shaka yoyote kwa:
1. Kutimiza kile nilichoahidi na kwenda hatua ya ziada
2. Kuhudhuria zaidi ya ninavyotegemewa kuhudhuria, kwa wakati, hata pale ninapokuwa na sababu za kunizuia nisihudhurie
3. Mara zote nizalishe matokeo bora kabisa zaidi ya inavyotegemewa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Natengeneza uhakika usio na shaka yoyote kwa wateja wangu kwa kuwa na bidhaa bora muda wote na kuwahudumia kwa ubora wa hali ya juu wakati wote hii itanijengea imani kubwa kwa wateja na kunitegemea kwa kuwa na uhakika kuwa wakihitaji bidhaa muda wote inapatikana.
Ninapoahidi kutekeleza jambo fulani inabidi nilitekeleze kama nilivyo ahidi bila kutoa sababu yoyote kwa kufanya hivi watu wataniamini na kunitegemea.
Asante sana kocha kwa makala hii.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nahakikisha nakuwa kama jua, nategemewa kwa uhakika kwenye mambo yangu yote.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana, nimewatengenezea wateja wangu uhakika WA huduma kila siku kuanzia JUMA pili Hadi ijumaa
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Timiza kwa kila unachoahidi kwa kwenda hatua za ziada
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuweza kutegemewa kwa uhakika kama jua.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha, kwenye Somo la Leo, nimejifunza hasa kujijengea sifa ya uhakika ya kutegewewa,na hii haitakuja ghafla inahitaji maandalizi ya kutosha, kuhakikisha unatekeleza kile unachohaidi na kufanya kwa Nidhamu Kali ya kuamua na kufanya kwa msimamo.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitahakikisha nategemewa kwa uhakika ili kufanya maisha ya wengine kuwa rahisi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitaweka juhudi kufanya yote yatakayoniwezesha kutegemewa kwa uhakika ili kufanya maisha ya wengine kuwa rahisi
LikeLike
KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA
1. Timiza unachoahidi
2. Nenda hatua ya ziada
3. Hudhuria unapotakiwa kidhudhuria bila kuwa na sababu za kujitetea
LikeLike
Imeisha
LikeLike
KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA
1. Timiza unachoahidi
2. Nenda hatua ya ziada
3. Hudhuria unapotakiwa kidhudhuria bila kuwa na sababu za kujitetea
Asante Sana kocha
LikeLike
Nitahakikisha kila nachofanya nafanya kwa uaminifu na mwendelezo ili kuweza kutegemewa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Bila watu kukutegemea huwezi kuwa mtu muhimu.
Wate wanatafuta watu wanaoweza kuwategemea.
Kama hakuna anaweza kukutegemea Bado Kuna safari ngumu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitatoa matokeo baora zaidi ili niweze kuaminika kwa kwenda hatua ya ziada
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ukiwa unazalisha matokeo bora kwa muda wote kitachokuzuia kufikia mafanikio ni muda tu
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwa kufanya kwa ubora muda wote kitakachozuia mafanikio ni muda tu
LikeLike
Asante kocha, ninaenda kutegemewa mara zote
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kipanga, napaswa kufanya. Hii itanijengea imani kwa wengine. Asante sana Kocha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike