3140; Chukua picha nyingi zaidi.
Rafiki yangu mpendwa,
Siku moja ya tarehe 10 Disemba mwaka 1914, Thomas Edison akiwa nyumbani kwake alipata taarifa kwamba maabara yake kubwa ilikuwa inaungua moto.
Aliongozana na kijana wake kwenda kuangalia hilo na kukuta kweli maabara ikiteketea kwa moto.
Baada ya kuona kinachoendelea, Edison aligeuka na kumwambia kijana wake; “Nenda kamwite mama yako na marafiki zake wote, hawatakuja kuona moto mkubwa kama huu tena.”
Kuna mengi sana ya kujifunza kupitia namna Edison alivyokabiliana na taarifa hiyo mbaya.
Lakini moja muhimu sana ambalo nataka wote tuondoke nalo hapo ni umuhimu wa kuweka kumbukumbu kwa hali zote ngumu tunazopitia, kwa sababu hazitakuja kujirudia tena.
Kuna hatua nyingi ngumu ambazo tunakuwa tunapitia kwenye hii safari yetu ya mafanikio.
Hatua ambazo nyingi hatutakuja kuzirudia tena.
Lakini pia ambazo zitatengeneza hadithi nzuri sana ya kule tulikotoka mpaka tulikofika.
Njia nzuri kwa hizi zama zetu ya kuweka kumbukumbu za hatua zote tunazopitia ni kuchukua picha za kila hatua tunayopitia.
Simu zetu za mkononi ni kifaa kinachoweza kuchukua picha nzuri sana.
Na pia tuna mitandao ambapo tunaweza kutunza picha zetu zisipotee, hata pale tunapopoteza simu zetu au vifaa vingine vyenye hizo picha.
Hivyo basi, wajibu wetu ni kuchukua picha nyingi zaidi za hali zote tunazopitia.
Chukua picha ya biashara yako tangu ikiwa ndogo na kadiri inavyoendelea kukua.
Chukua picha na watu unaoshirikiana nao tangu hatua za chini kabisa, washirika, wafanyakazi, wateja n.k.
Chukua picha za eneo unaloishi na kufanyia kazi zako.
Chukua picha ya salio lako la benki na uwekezaji kama wa UTT kwa hatua zote tangu unapoanzia chini na unavyoendelea kwenda.
Kwa kifupi, chukua picha za kila kitu unachopitia sasa na unachoendelea kupitia kwenye safari yako ya kujenga mafanikio makubwa.
Zoezi la kuchukua picha kama sehemu ya kumbukumbu za maisha siyo geni, lilikuwepo sana tangu zamani.
Lakini zama hizi za simu janja na mitandao tunalichukulia poa, wakati ndiyo tungepaswa kulipa uzito zaidi.
Kwani kwa zama hizi unaweza kuchukua na kutunza picha nyingi zaidi na kwa gharama ndogo zaidi.
Lakini pia unaweza kuchukua na kutunza sauti pamoja na video za kila hatua unazopita.
Unachukua na kutunza hayo kwa kumbukumbu zako binafsi na vizazi vyako.
Lakini muhimu zaidi ni kuna watu watakuja kuongea ujinga sana siku za mbeleni huko utakapokuwa umefanikiwa.
Watasema una bahati au kuna namna ulipita njia za mkato.
Wajinga kama hao huhitaji kubishana nao kwa maneno, bali kwa kuonyesha ushahidi wa picha ulizochukua kwenye kila hatua.
Japo siyo lengo, lakini ni hadithi nzuri na yenye nguvu.
Lakini pia sisi binadamu huwa tuna tabia ya kusahau mambo haraka.
Tunaweza kutokea chini kabisa, tukapambana na kufika juu, halafu tukajisahau, kitu kinachotupa anguko kubwa.
Kwa kuwa na kumbukumbu halisi za kule tulikotoka, ambazo tunaziangalia mara kwa mara, tunakuwa wanyenyekevu na kuendelea kuweka juhudi bila kuruhusu mazoea.
Na kama kuna picha zako za nyuma ambazo ulipiga na zikachapwa kwa nakala ngumu, zigeuze kuwa nakala laini na tunza kwenye maeneo uliyochagua ya kutunza picha zako ili zisipotee.
Kitu kimoja tunachokijua bila ya shaka yoyote ni kwamba tutapiga hatua kubwa sana zaidi ya pale tulipo sasa.
Ni muhimu sana tuweke kumbukumbu zetu sawa kwa kila hatua tunayopiga kwa ajili ya matumizi mazuri ya baadaye.
Kwa sababu ni hatua ambazo hatutakuja kuziona tena na wale tunaokuja kukutana nao huko mbele pia hawatakuwa wameziona.
Haijalishi umefanikiwa kiasi gani, hakikisha una kumbukumbu zote za hatua ulizopitia kufikia mafanikio hayo.
Hilo litakusaidia kuendelea kuwa mnyenyekevu na hata kuwaonyesha wengine ambao hawakuwepo wakati unapiga hatua hizo.
Hivyo chukua picha nyingi zaidi kwa kila hatua unayopiga kwenye maisha yako, ni muhimu sana kwa maendeleo yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kweli picha za msoto wako itakuja kukuonyesha kuwa ukicheza tu unarudi huko uikotoka hii ina maana kuwa tuongeze bidii zaidi na kuweka rekord zetu za kuvuka ngazi zote tena umenikumbusha kuna maeneo natakiw kuchukua picha zake nakuhifadhi
LikeLike
Safi sana, fanya hivyo.
LikeLike
Kwenye hili la kuchukua picha nadhani bado sijalitendea haki. Picha zinatunza taarifa nyingi muhimu kwani zinahifadhi mpaka hisia ambazo mtu anakuwa nazo wakati husika.
LikeLike
Kabisa, hilo eneo la hisia.
LikeLike
Mchakato wa kuelekea kwenye ubilionea ni mgumu sana. Ni muhimu sana kuweka kumbukumbu ili utakapofanikiwa watu wajue si bahati pekee umepata bali ulifanya na maandalizi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kupiga picha nzima ya mafanikio yangu ili mwisho wa siku niwe na ushaidi nilikotoka na hatua niliyofikia.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
ahsante kocha,
hili nalianza leo hii. maana huko nyuma nilikuwa mvivu katika eneo hilo.
LikeLike
Vizuri, litekeleze.
LikeLike
Hili swala la picha ni muhimu sana, mara nyingi tunapo kuwa kwenye projects huwa napenda kuchukua picha na baada ya miaka tukitaka information (ambazo mara nyingu tumesahau) huwa mkombozi huwa ni picha hapa nimelipia 200GB cloud storage nafikiri ni muda wa kuchukua oicha zaidi.
LikeLike
Vizuri sana, tekeleza hilo.
LikeLike
Hakika kocha nitahakikisha ninachukua picha nyingi zaidi iwezekanavyo ili kupata ukumbusho ambao utasaidia kuweka ukumbusho kwa wengine
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitachukua picha nyingi katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu ya baadae.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwa kuwa sisi ni wauzaji bora kuwahi kutokea, kuchukua picha ni muhimu sana kwa ajili ya kuonesha ushuhuda katika mambo 16 ya kuzingatia wakati wa MAUZO.
Na kwa kuwa MAUZO NI MAHUSIANO, tutatumia picha kama ushahidi wa kuwaonesha wale tunaohusiana nao.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Picha ni kumbu kumbu muhimu Kwa tukio tunalofanya hasa Kwa safari hii ya ubilionea tunapo anzia chini kabisa.
Asante sama
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ahsante sana Dr Amani,
Tunayoyaputia yalikuepo ni vile hatuna kumbukumbu kama muongozo kwa hatua za kuchukua kwa yanayotokea kwa kua si mageni bali sisi ndo wageni.Jukumu letu ni kuchukua picha kuanzia sasa
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kuchukua picha nyingi zaidi kwa kila hatua unayopiga kwenye maisha yako, ni muhimu sana kwa maendeleo kweli. Maana hayo ndiyo yataonyesha au kukuonyesha ulikotoka wewe na familia yako.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Sana kwa kuelekeza umuhimu wa kuchukua picha , nitalizingatia kikamilifu kulitekeleza
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Haijalishi nitakuwa nimefanikiwa kiasi gani, lazima nihakikishe nina kumbukumbu zote za hatua nilizopitia kufikia mafanikio hayo.🙏🙏
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana kocha,huwa mvivu kwenye kuchukua na kitu za kumbukumbu,ila Hadithi au kisa hicho cha Thomas Edison kimenipa Elimu kubwa,kwanza uwezo wa kupokea jambo kubwa zito kama hilo, Elimu ya Falsafa ya ustoa naimani ilimwongoza.
LikeLike
Hakika, alitumia sana Ustoa kulikabili hilo.
LikeLike
Kumbukumbu za picha pamoja na taarifa mbalimbali ni muhimu sana ktk historia ya ukuaji au mabadiliko ya kimchakato. Asante sana kwa kunikumbusha. Nitafanya hivyo mara kwa mara na kuhifadhi vizuri
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kuna haja kubwa ya kutengeneza database ya picha kwaajili ya kumbukumbu mbalimbali. Hilo ni la muhimu sana
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante sana Kocha, nitapigwa picha mara zote Ili kutunza kumbukumbu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mtajitahidi kuchukua picha zaidi ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye safari hii kama sehemu ya kumbukumbu bora kabisa
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kwa hili kocha nitaanza kupiga picha kwa kila hatua inayopitia
LikeLike
Vizuri
LikeLike