3141; Kwa nini hufanyi?

Rafiki yangu mpendwa,
Unajua unachotaka kwenye maisha yako, wapi unapotaka kufika.
Pia unajua nini unapaswa kufanya ili uweze kupata unachotaka.
Lakini sasa, kwa nini hufanyi yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka kupata?

Na hata pale inapotokea unaanza kufanya, kwa nini huna mwendelezo?
Kwa nini unaanza kufanya na kuishia njiani?
Nini kinakukosesha msimamo kwenye ufanyaji?

Unapanga kabisa mpaka muda wa kufanya yale unayopaswa kufanya.
Lakini muda huo unapofika, unaahirisha kufanya.
Kwa nini inakuwa hivyo?

Miaka kumi iliyopita, ungeanza kufanya na ukafanya kwa msimamo bila kuacha, leo hii ungekuwa mbali zaidi ya hapo ulipo sasa.
Nini kimekukwamisha kufanya hivyo?

Una miaka mingine kumi mbele yako, ambayo usipokuwa na tahadhari, nayo utaipoteza kama ulivyopoteza hiyo iliyopita.

Umewahi kujiuliza kwa nini unapumua kila mara bila kuacha hata kama umetingwa kiasi gani?
Huwa huachi kabisa kula chakula hata kama kila kitu hakipo sawa.
Lakini inapokuja kwenye kufanya yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka, huwa unaruhusu sababu mbalimbali zikuzuie.
Kwa nini unaruhusu hayo?

Rafiki, kwa nini hufanyi yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka kwa namna unavyopaswa kufanya?
Weka maoni yako hapo chini ya swali hilo, kwa uhalisia kabisa kutoka ndani ya moyo wako.

Kutokana na majibu yako, weka mkakati wako wa ufanyaji bila kuruhusu kukwamishwa na chochote kile.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe