Mpendwa mstoa mwenzangu,
Jana kwenye falsafa ya kwanza ya Ustoa tulijifunza umuhimu wa kuwa na afya ya akili, mwili na roho. Na tuliona kwamba , binadamu huwezi kukamilika kama hujakamilika kwenye maeneo hayo. Eneo la kiroho ndiyo eneo ambalo watu wengi bado hawajalipatia na linawafanya watu wengi kukosa shukrani na kile ambacho wanacho.
Sina uhakika kama itakufaa lakini hakuna dini ambayo ni bora kuliko nyingine. Kila mtu yuko sahihi kadiri ya imani yake na kile anachokiamini yeye. Na siko hapa kufungamana na dini yoyote ile.
Hata Yesu Kristu na mtume Muhammad angefufuka leo, asingeweza kuishi kwenye dini yoyote ile kulingana na misingi yao waliyoanzisha na vile watu wanavyoishi sasa ile misingi yao ya kiimani kwa sasa.
Watu wamekuwa wanagombana na kuzozana sana katika mambo ya dini badala ya kufanya kazi. Hakuna ushindi wowote utakaoupata katika kubishania mambo ya kidini lakini utapata ushindi tu pale utakapofokasi katika mambo yako muhimu yanayokupatia fedha za kulipa bili mbalimbali za maisha yako.
Tunapaswa kuelewa kuwa kila mtu achwe vile anavyoamini yeye na siyo dini kuwashurutisha watu kufanya vitu ambavyo vinakuwa vinajali matakwa ya viongozi.
Watu wengi kwa sasa wamekuwa ni watumwa kwa dini. Dini zimewashika watu kiasi kwamba wanakosa hata uhuru wa kufanya mambo yao binafsi. Wakiambiwa kitu na viongozi wao wa kiroho jibu ni ndiyo, hata kama siyo sahihi wanakubali tu kufanya bila kuhoji.
Dini haziwajengi watu kiimani, bali zinawakandamiza watu kuwa tegemezi kwenye dini kwa kuwajengea hofu kama vile usipoenda jumuiya, usipoenda kanisani, usipoenda msikitini, basi ukifa hautazikwa. Watu wengi wamekuwa wanafungwa na dini na wanalazimika kutumikia kubaki kwenye mateso ambayo hata wao wenyewe hawataki ili tu wakifa wapate kuzikwa.
Aliyekuwa mwalimu na mwanafalsafa wa Ustoa Epictetus yeye ana haya ya kusema juu ya dini;
Dini zote zinapaswa kuwa na uvumilivu… Kwa kila binadamu ataenda mbinguni kwa njia yake mwenyewe.
All religions must be tolerated… for every man must get to heaven in his own way.
Epictetus
Kama kila binadamu ataenda mbiguni kwa njia yake mwenyewe, tunapaswa kuwa wavumilivu kwenye mambo ya kidini , dini isiwatumie waumini wake vibaya na wala wewe usitumike vibaya na dini kutimiza matakwa ya viongozi wa kidini.
Dini ya kweli ni upendo, tunapokuwa tuna upendo ndani yetu tuna muona Mungu mwenyewe. Tukiweza kujipenda sisi wenyewe, kuwapenda wengine na kupenda kile tunachofanya.
Lakini, dini zinawafanya watu kuwa watumwa na kushindwa kutumia fikra zao kwa usahihi. Aliyekuwa mtawala wa Ufaransa na jemidari wa kijeshi Napoloen Bonaparte aliwahi kunukuliwa akisema dini zinawafanya watu kuwa masikini, na masikini kuwachukia matajiri, ukiliangalia hilo kwa undani ni kweli, badala ya watu kufanya kazi, wanakesha kwenye nyumba za ibada kuomba na kutafuta miujiza ya haraka bila kazi.
Usipoteze muda wako kuhukumu mambo ya kidini, kuingilia mambo ya kiimani ni suala ambalo liko nje ya uwezo wako, ukiona watu wanabishania dini chukua jembe nenda ukalime au kafanye kazi kama waswahili wasemavyo, ukiona ndugu wanagombana chukua jembe nenda ukalime, tuwe wavumilivu.
Religion is regarded by the common people as true, by the wise, as false and by the rulers as useful. Seneca
Seneca anasema, dini inachukuliwa na watu wa kawaida kuwa ya kweli, na wenye hekima, kuwa ya uwongo na kwa watawala kuwa yenye manufaa.
Hapo unapata picha kwamba, watawala wanatumia dini kupata kile wanachotaka au kifupi kujali maslahi yao.
Dalai Lama naye aliwahi kunukuliwa akisema, dini yangu ni rahisi. Dini yangu ni ukarimu.
My religion is simple. My religion is kindness.
Naye aliyekuwa raisi wa marekani Abraham Lincoln aliwahi kunukuliwa akisema, pale napofanya vizuri, najisikia vizuri, pale napofanya vibaya najisikia vibaya na hiyo ndiyo dini yangu.
When I do good, I feel good, when I do bad I feel bad and that’s my religion – Abraham Lincoln.
Wabudha nao waliwahi kunukuliwa wakisema, haijalishi maneno mangapi unasoma, unaongea, ni mazuri gani hayo unayofanya kama huyafanyii kazi?
Kwenye suala la dini, tunapaswa kuwa wavumilivu kutokuwahukumu wengine kwa sababu kila mmoja wetu ataenda mbinguni kwa njia yake mwenyewe.
Kwenye kitabu cha Yakobo, anasema dini iliyo safi na isiyo na hililafu mbele ya Mungu Baba ni hii, kuwasaidia yatima, wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Watu wengi siku hizi wanajificha kwenye miamvuli ya dini, kwa kukwepa kufanya kazi na kusingizia dini. Muda wote kwenye nyumba za ibada kwa kufanya hivyo unafikiri utatoboa?
Hatua ya kuchukua leo; Usiwe mtu wa dini, kuwa mtu wa imani na utaweza kufanya makubwa sana.
Dini inawafunga watu lakini ukiwa mtu imani unakuwa huru kufanya kile unachotaka kadiri ya imani.
Kwahiyo, watu wengi wanapenda kuwa watu wa dini kuliko kuwa watu wa imani.
Dini haimpeleki mtu mbinguni bali kila mtu atakwenda kwa njia yake mwenyewe, matendo na imani yako ndiyo yatakufikisha mbinguni.
Shabaha kubwa ya falsafa ya Ustoa ni kukutaka wewe ufokasi kwenye mchakato wa BILIONEA MAFUNZONI na CHUO CHA MAUZO.
Kwa kuwa umeujua ukweli, usikubali kuyumbayumba tulia na fanya kazi.
Rafiki yako katika falsafa ya Ustoa,
Mwl. Deogratius Kessy
shukrani mwl Deo kwa andiko la leo dini ,ustoa na IMANI mtu anav yoweza kuvitumia na kufanya makubwa.
barikiwa sana
LikeLike
Asante sana Mr Christopher Mwijage. Pole kwa Changamoto ya ajali na karibu sana.
LikeLike
Kwenye dini tunapaswa kuwa wavumilivu,na kutokuwahukumubwengine kwani kila mtu ataenda mbinguni kwa njia yake mwenyewe
-Watawala wanatumia dini ili kuwatawala wafuasi wa dini hizo kwa maslahi yao binafsi
Nimechagua kuwa mtu wa imani ili imani iweze kunisaidia na kuniongoza kufanya mambo kwa usahihi kadiri imani yangu inavyoniongoza.
Asante Mwalimu Deo
LikeLike
Vizuri sana Bilionea Notbruga Basil kwa kuchagua kuwa mtu wa Imani
LikeLike
Usiwe mtu wa dini kuwa mtu wa imani
Asante sana
LikeLike
Vizuri sana Mr Bosco Mlomo. Kuwa mtu wa imani na usiwe mtu wa dini.
LikeLike
Asante sana mwalimu Deo kwa falsafa ya Leo Dini na imani kwa kweli hii imenifungua akili kuna marafiki zangu walikuwa naniambia kwamba kwasababu mimi huwa siendi kanisani sitazikwaga na Watu wengi kumbe ni watu wa dini ndiyo wanawajengea Watu hofu ili wapate kile wanachotaka
LikeLike
Vizuri Mr Kizito, endelea kuwa imara kwa kuwa mtu wa imani
LikeLike
Kwa ufupi Falsafa ya ustoa ni ni kitu kinachokuweka katika mchakato wa mafanikio
LikeLike
Hakika Mr Hassan
LikeLike
Napaswa kuwa mtu wa Imani na siyo mtu wa dini, lakini ukweli kwa sasa dini ni kitimu timu bora hata sisi tunapata Elimu ya Falsafa ya ustoa.
LikeLike
Umesema kweli Mr Beatus Elias
LikeLike
Dini ni unyonyaji kwa maslahi ya wachache kupitia kupumbaza watu wengi kwa hadaa na hofu. Dini zimekuwa pia ni daraja la wanasiasa kufanikisha agenda zao kiurahisi kwa gharama ya maisha ya wengi.
Hatuna budi kusimama kwenye mitazamo huru isiyotawaliwa na hofu, ili kuweza kuishi maisha yetu kwa namna bora zaidi na kufanikisha ndoto kubwa sana tulizonazo badala ya kutumikia vifungo vya dini vinavyosababishwa na uduni wetu wenyewe wa kufikiri.
LikeLike
Umesema vizuri sana Mr Sebastian
LikeLike
Asante sana mwl deo Leo umeleta jambo jema na linaweza kuwafumbia watu ili wapate kujua ukweli wa mambo na kufanya maamuzi sahihi Kwa Dunia hii ya Leo
Asante sana
LikeLike
Asante sana Mr Ernest
LikeLike