3221; Nani anamiliki nani?
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna utani kwenye mabenki kwamba mtu akiwa anadaiwa bilioni na benki, basi mtu huyo anakuwa anamilikiwa na benki.
Lakini mtu akiwa anadaiwa trilioni na benki, mtu huyo anakuwa anaimiliki benki.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa wateja na biashara.
Pale mteja mmoja anapokuwa anachangia chini ya asilimia 10 ya mauzo yote ya biashara, mteja huyo anakuwa anamilikiwa na biashara.
Lakini kama mteja mmoja anachangia zaidi ya asilimia 10 ya mauzo ya biashara, mteja huyo anaimiliki biashara.
Hataonekana moja kwa moja kuwa na umiliki kwenye biashara, lakini kwa namna ambavyo biashara inakuwa inamtegemea, anakuwa na nguvu ya kuathiri mipango ya biashara.
Pamoja na wajibu mkubwa ulionao wa kutengeneza wateja wakubwa na wa uhakika kwenye biashara yako ili kukuza mauzo, unapaswa pia kuhakikisha huwi na utegemezi mkubwa kwenye wateja wachache.
Kama una wateja wachache ambao ndiyo wanachangia mauzo makubwa kwenye biashara yako, ongeza zaidi aina hiyo ya wateja.
Chukua idadi ya wateja wakubwa ulionao sasa kisha zidisha mara kumi.
Hilo ndiyo linapaswa kuwa lengo lako la wateja wazuri wa kuhakikisha unakuwa nao.
Unapokuwa na mara kumi ya idadi ya wateja wazuri ulionao, unabaki na nguvu kubwa kwenye biashara yako.
Hata pale biashara inapopoteza mteja mmoja au wachache kwa sababu zozote zile, haitetereki sana.
Kumbuka umechagua kuingia kwenye biashara ili uweze kufanya kile unachotaka kufanya, kwa namna unavyotaka kufanya, kwa wakati na mahali unakotaka kufanya.
Mwanzoni unaweza usiwe na uhuru kwenye maeneo yote hayo, lakini kadiri unavyokuza biashara yako kwa namna ambavyo haikutegemei, ndivyo unavyopaswa kuwa huru zaidi.
Huwezi kupata uhuru wa kibiashara unaoutaka kama bado utakuwa tegemezi kwa wateja wakubwa wachache.
Kwa wateja wowote wakubwa ulionao, weka juhudi kutengeneza wengi zaidi wa aina hiyo, kwa kurudia kwa wingi na ukubwa yale yaliyokuletea wateja hao.
Jenga biashara yako kwa usahihi ili pia uweze kuikuza kwa usahihi na kupata uhuru unaoutaka.
Hakikisha biashara ndiyo inawamiliki wateja kwa kutoa thamani kubwa sana ambayo wateja hawawezi kuipata mahali pengine huku ikiwa na wateja wengi wakubwa kiasi kwamba wachache wakiondoka biashara haitetereki.
Hili litahitaji kazi kubwa,
Litahitaji uwe tayari kupoteza baadhi ya wateja.
Litahitaji uwe tayari kuacha fedha ambazo ni rahisi kupata.
Lakini litajenga msingi imara sana wa mafanikio makubwa ya kibiashara.
Lipambanie kwa uhakika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nimeanza na pia naendelea kutengeneza wateja wengi zaidi ili kuifanya biasha yangu kuwa imara zaidi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Natengeneza wateja wakubwa wengi zaidi
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa ushauri wako katika hili. Nimeweza kuelewa na kuona mwanga jinsi ya kukuza kipato kwa kukuza namba ya wateja katika biashara zangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni muhimu sana biashara kuwamiliki wateja na si biashara kumilikiwa na wateja.Na hapo ndipo kwenye uhuru halisi
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hili ni muhimu sana.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ukweli utabaki kuwa ukweli,kwamba kwenye biashara yangu, nahitaji kutengeneza wateja wakubwa zaidi ya nilionao kwa sasa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli kocha kuwa na wateja wachache wakubwa wanakutesa. Maana Mimi Nina ushaidi WA mteja wangu mmoja mkubwa sasa amefika mahali anataka yeye asikilizwe na atoe maamuzi kwenye biashara yangu Kwa kigezo kuwa yeye ni WA siku nyingi na ni mkubwa. Japo ukumbwa huo Mimi pia nimechangia Sana.
LikeLike
Ni muhimu sana tufanye kazi kubwa kwenye biashara zetu kuhakikisha mteja mmoja au wachache wanaokuwa na nguvu kubwa ya kuathiri biashara.
Na wateja huwa hawajali kama ukubwa wao wewe ndiyo umechangia.
LikeLike
Huwezi kupata uhuru wa kibiashara unaoutaka kama bado utakuwa tegemezi kwa wateja wakubwa wachache.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nimeanza kulipambania kwakulipia matangazo ili kupata wateja wengi zaidi
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni muhimu sana kuwa na wateja wakubwa ili uweze kuwa na uhakika lakini pia unapaswa kujenga nguvu kubwa ya kuweza kuwahudumia waweze kupata kile wanachokitaka hivyo tujenge stamina kubwa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kuwa na Wateja wachache hata kama unapata faida kubwa ni risk kubwa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante Sana kocha kwa somo hili.
Nitahakikisha sina utegemezi mkubwa kwa wateja WACHACHE.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Wateja wakubwa nilionao nikizidisha mara kumi hilo ndio litakuwa lengo langu la kupata wateja wazuri.
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi.
LikeLike
Bishara yenye afya ni ile inayo miliki wateja na si kumikiwa na wateja.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha,
Biashara inahitaji wateja mihimili wengi ili hata baadhi wakiachia, bado wanaobaki biashara iendelee kusimama.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante kocha hili nakwenda kuchukua hatua yakuwatafuta wateja wengi zaidi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakikisha biashara ndiyo inawamiliki wateja kwa kutoa thamani kubwa sana ambayo wateja hawawezi kuipata mahali pengine huku ikiwa na wateja wengi wakubwa kiasi kwamba wachache wakiondoka biashara haitetereki.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante sana, kama unamtegemea Mteja Mmoja KUFANYA mamunuzi makubwa basi huyo Mteja anaimiliki biashara
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kujenga wateja wakubwa wa uhakika na wengi zaidi ndio unapata ukuaji mkubwa kwenye biashara
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Wateja wakiwa wakubwa kuliko biashara tunapoteza mauzo pia sababu akikaamua umkopeshe na kululipa baada ya mwaka sababu ya ukubwa wake unaweza kumruhusu ili usimpoteze . Kubwa Zaidi ni kuongeza pump line x 10 kama alivyo sema Kocha. Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Somo zuri sana. Kila biashara inapaswa kuwa na wateja wakubwa wengi na siyo wachache ambao watakuwa wanaimililki biashara.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Biashara inafanya vizuri muda wote pale unapokuwa na Wateja wakubwa wengi kadiri inavyowezekana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Najenga biashara yenye wateja wakubwa wengi ili biashara imiliki wateja.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha,Ni jukumu langu kuongeza wateja wakubwa wengi ili niweze kuongeza mauzo zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kweli kabisa,
Siwezi kupata uhuru wa kibiashara ninaoutaka kama bado nitakuwa tegemezi kwa wateja wakubwa wachache.
LikeLike
Hakika
LikeLike