3229; Usivyoweza kununua.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kuwalipa watu na wakakusaidia kwa namna ambayo unarahisisha na kuharakisha matokeo.
Unaweza kuwalipa watu wakufundishe na kukuonyesha kile unachopaswa kukifanya.
Unaweza kuwalipa watu wakusaidie kwenye kufanya kile unachopaswa kufanya na ukaweza kuzalisha matokeo makubwa zaidi.
Hivyo ndivyo ukuaji mkubwa huwa unapatikana, kupitia kutumia rasilimali za watu wengine ambazo unaweza kuzinunua.
Lakini kuna kitu kimoja kinachohitajika sana kwenye mafanikio ambacho huwezi kukinunua kwa gharama yoyote ile.
Kitu hicho ni ile nia ya ndani ya kutaka kufanikiwa.
Ule msukumo wa ndani wa kutaka kufanikiwa, unaokufanya uwe tayari kuchukua hatua na kuvumilia magumu ni kitu ambacho huwezi kulipa wengine wakakupa.
Hicho ni kitu ambacho kinaanzia ndani ya mtu pekee.
Ndiyo kitu kinachomsukuma mtu kufanya mengine muhimu anayoyahitajika kufanya ili kufanikiwa.
Kuna kitu kingine ambacho pia ni vigumu kuweza kukinunua kwenye safari yako ya mafanikio.
Kitu hicho ni kasi ya kupata matokeo.
Mara nyingi umekuwa unayataka matokeo kwa haraka sana.
Na unakuwa tayari kuingia gharama mbalimbali ili upate matokeo makubwa kwa haraka.
Kitu unachopaswa kujua ni kwamba huwezi kununua kasi ya kupata matokeo makubwa unayoyataka.
Matokeo yote unayopata yanajengwa kupitia mkusanyiko wa hatua mbalimbali zinazokuwa zimetangulia.
Kila juhudi inayowekwa, inakuwa na mchango kwenye matokeo yanayokuja kupatikana.
Hakuna njia ya kuharakisha mchakato huo wa hatua mbalimbali kujikusanya na kuzalisha matokeo makubwa.
Kuna watu wanauza siri mbalimbali za mafanikio.
Vitu vingi kuhusu mafanikio viko wazi, lakini kwa sababu watu wanathamini zaidi siri, kilicho wazi kikiitwa siri wanakuwa tayari kukilipia.
Ukishajikuta unatumia muda mwingi wa kutafuta siri za kitu chochote kile, jua tayari umeanza kupotea.
Utapoteza gharama nyingi kulipia vitu ambavyo haviwezi kufanya kazi kwa namna yoyote ile.
Ijue misingi sahihi ya kila kitu na ifuate hiyo.
Kwa sababu misingi huwa haitetereki, ukiifuata hiyo utakuwa salama muda wote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Msukumo na kasi.Hivi vinatoka kwangu na si vya kununua popote.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Msukumo wa ndani na Kasi yakupata motokeo vinatoka ndani yangu na sio vya kununua OK Asante sana kocha
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Matokeo yote unayopata yanajengwa kupitia mkusanyiko wa hatua mbalimbali zinazokuwa zimetangulia.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakuna njia ya kuarakisha mchakato huo wa kujikusanya na Kuzalisha matokeo makubwa.
Na ukijikuta unatumia muda mwingi kutafuta siri za mafanikio jua tayari umepotea.
Asante kocha kwa ukurasa bora Sana.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitaifuata misingi sahihi ili nisitetereke kwenye safari ya mafanikio. Msukumo na kasi ya kwenye mchakato viko ndani yangu, hakuna mahali pa kuvinunua.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Hakuna njia ya kuharakisha mchakato. Asante Kocha. ✍️
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli huwezi kununua nia ya wew kufanikiwa hiyo inatoka ndani ya moyp wako tu na kuweka juhudi
LikeLike
Hakika
LikeLike
Msukumo uliopo ndani ya mtu,nia ya ndani ya mtu ktk safari ya mafanikio vinabaki kuwa ndani ya mtu husika.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Msukumo wa ndani na kasi havinunuliki.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Hatuwezi kununua kasi ya kupata matokeo makubwa tunayoyataka, kwani matokeo tunayoyataka yanajengwa kupitia mkusanyiko wa hatua mbali zinazokuwa zimetangulia.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike