3238; Akili ikikosekana, haya yawepo.
Rafiki yangu mpendwa,
Warren Buffett amekuwa anasema unapotaka kuajiri, angalia vitu vitatu, uadilifu, akili na nguvu. Na anaendelea kusisitiza kama sifa ya kwanza haipo, hizo mbili zitakumaliza kabisa.
Hizo ni sifa tatu muhimu sana kuzingatia ili kupata watu sahihi.
Lakini pia ni sifa ambazo siyo rahisi kuzipata kwa walio wengi.
Hasa kipengele cha akili.
Ni watu wachache sana ambao wana akili kubwa na uwezo wa hali ya juu.
Na watu hao kuwaajiri siyo rahisi, kwa sababu labda wanakuwa wanafanya mambo yao au wameajiriwa mahali pengine ambapo wanapata maslahi mazuri.
Unapokuwa unaanza au bado upo chini na huwezi kumudu kupata wafanyakazi wenye akili kubwa na uwezo wa hali ya juu, basi hakikisha unazingatia sifa hizi tatu; njaa, unyenyekevu na uaminifu.
Njaa ni sifa muhimu sana kuiangalia kwa watu unaowaajiri au unaotaka kushirikiana nao.
Njaa ni pale mtu anapokuwa anajua kitu anachotaka na amejitoa kweli kukipambania mpaka akipate.
Watu wenye njaa ya kufika mahali fulani tayari wanakuwa na msukumo mkubwa ndani yao.
Siyo watu wa kusubiri mpaka wewe uwasukume. Njaa yao ni msukumo tosha kwao.
Utawajua wenye njaa kwa msukumo wanaokuwa nao kwenye kile wanachotaka.
Ukikutana na asiye na njaa, utamjua tu, uvivu na uzembe unakuwa mwingi na inakuwa kazi kubwa kwako kumfanya afanye kazi.
Watu wa aina hiyo ni wa kuachana nao.
Unyenyekevu ni utayari wa kujifunza na kuchukua hatua kwenye yale ambayo mtu amejifunza.
Watu wengi ambao hawana akili na uwezo mkubwa, ni wa kuelekezwa nini wanapaswa kufanya.
Kama watakuwa na ujuaji, kwa kukataa kujifunza na kufanya vile wanavyotaka wao, wanakuwa mzigo mkubwa.
Fanya kazi na wale ambao wana utayari wa kujifunza na kufuata taratibu mbalimbali ambazo umeziweka.
Epuka sana wale wajuaji na ambao wanadhani wana njia bora kuliko utaratibu ulioweka wewe.
Watu hawa huishia kutengeneza matatizo ambayo yanakugharimu kuyatatua.
Uaminifu lipo wazi, unahitaji kushirikiana na watu ambao ni waaminifu.
Na hapa pia, kama uaminifu utakosekana, hivyo viwili vya mwanzo vitakumaliza kabisa.
Fikiria una mtu mwenye njaa kali ya mafanikio na ni mnyenyekevu sana, lakini siyo mwaminifu.
Njaa yake kali itamsukuma kufanya makubwa na unyenyekevu wake utakuhadaa kumwona ni bora.
Kukosa kwake uaminifu kutakuletea matatizo makubwa.
Utaujua uaminifu wa mtu baada ya kufanya naye kazi na kuangalia kama maneno yake yanaendana na matendo.
Kama kuna mkanganyiko wowote kati ya maneno na matendo, jua wazi uaminifu hakuna.
Rafiki, sifa hizo tatu siyo za kumuuliza mtu akakujibu. Maana kila mtu tayari anajinadi kuwa na sifa nyingi nzuri.
Hizo ni sifa za kuangalia wewe mwenyewe wakati unafanya kazi na mtu.
Hivyo unapochuja watu wa kufanya nao kazi, kuwa na maswali ambayo yatakusaidi kupata wale ambao unaona watakuwa na sifa hizo.
Lakini kazi hasa ya kujua kama sifa hizo zipo ni pale unapofanya nao kazi.
Unapaswa kuendelea kuwafuatilia watu unaojihusisha nao mara zote na kuangalia kama hizo sifa zipo.
Pale unapojidhihirishia bila ya shaka yoyote kwamba kuna sifa kati ya hizo tatu zinakosekana kwa mtu, usiendelee naye.
Unaweza kujiambia mtu atabadilika na hata yeye mwenyewe kukuahidi hivyo.
Lakini mabadiliko siyo rahisi kiasi hicho.
Hivyo usipoteze muda na nguvu na watu ambao siyo sahihi kwako.
Una kazi kubwa zaidi kwako kufanya kuliko kuwabadili watu.
Fanya kazi na wale ambao tayari wanazo sifa unazozitaka.
Na usihofie kwamba huwezi kuwapata.
Hii dunia ina watu wengi sana.
Na kati ya hao wengi, wapo wale ambao wana sifa unazotaka.
Ni wewe kuweka kazi kuhakikisha unawapata na kufanya nao kazi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakika hizi ni sifa muhimu sana katika ukuaji wa kibiashara na kwa lengo la kufikia ubilionea
LikeLike
Ndiyo, tuzizingatie.
LikeLike
Uadilifu, akili na nguvu.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Na akili ikikosekana, basi njaa, unyenyekevu na uaminifu viwepo.
LikeLike
Uadilifu,Akili, na nguvu, hizi ni sifa muhimu sana japo ni changamoto na hasa kwenye biashara changa,
LikeLike
Njaa, unyenyekevu na uaminifu siyo vigumu kupatikana.
LikeLike
Unapokuwa unaanza au bado upo chini na huwezi kumudu kupata wafanyakazi wenye akili kubwa na uwezo wa hali ya juu, basi hakikisha unazingatia sifa hizi tatu; njaa, unyenyekevu na uaminifu.
Lengo kuu ni kuambata na wenye sifa hizi…1.UADILIFU, 2. AKILI, 3.NGUVU.
Japo katika mazingira yetu hasa Africa, hii sifa ya UADILIFU!! Tuendelea Kujenga mifumo ambayo tabia za MTU haziwi kikwazo katika ukuaji wetu . Propaganda ni nyingi kila mahali na zinakuwa na malengo yaliyojificha na hayasemwi au kuhubiriwa waziwazi..hata kwenye nyumba za Ibada.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimekuwa nikidhani sifa hizi tayari ndugu/familia watakuwa nazo kweye biashara au kile ninachofanya kwa manufaa yetu wote. Kwa uzoefu wangu hakuna uhakika huo. Wanafamilia/ndugu siyo kigezo cha kuwaweka kwenye biashara. Uadilifu, akili na nguvu ni sifa muhimu kwa wale utakaokuwa nao kwenye kuendesha biashara.
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Kila ninapotafuta watu wa kushirikiana nao nitazubgatitia njaa,unyenyekevu na uaminifu.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Njaa, unyenyekevu na uaminifu nitajitahidi kuyafuatilia haya kwa wale ninaofanya nao kazi hasa uaminifu. Asante kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kila Mara sifa moja Wapo haipo, au ni dhaifu, kujenga timu ni zoezi la kudumu kwa uhakika.
LikeLike
Kabisa, inahitaji kazi na kutokuridhika au kukata tamaa haraka.
LikeLike
Njaa, unyenyrkevu na uaminifu ni Mambo nitakayoyaangalia Sana katika kuajiri.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kila wakati nitatafuta watu wenye sifa za uaminifu ili kushilikiana nao . watu waaminifu huwa pia ni wanyeyekevu na wanaakili, sintaogopa kufukuza wasio waaminifu ninaamini watu waaminifu wapo japo nivigumu kuwapata.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Hakika, watu wapo, tuweke kazi kwenye kuwatafuta.
LikeLike