Rafiki yangu mpendwa,
Nina malengo makubwa mawili ninayoyapambania kwenye maisha yangu.

Lengo la kwanza ni kuwa Bilionea (wa dola za Kimarekani)

Na lengo la pili ni kuwa Rais wa Tanzania.

Malengo haya mawili ni lazima nitayafikia, au nitakufa nikiwa nayapambania.

Rafiki, malengo haya makubwa sana sitaweza kuyafikia peke yangu.
Nahitaji sana ushirikiano wako wa karibu katika kuyatimiza.

Kwa sababu falsafa yangu kuu ya maisha ni hii; NAWEZA KUPATA CHOCHOTE NINACHOTAKA, KAMA NITAWASAIDIA WENGI ZAIDI KUPATA WANACHOTAKA.

Timu inayoendesha programu ya CHUO CHA MAUZO, karibu tufanye kazi pamoja na uwe muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea.

Ninachotaka kwako rafiki yangu ni uniambie nini unachokitaka sana kwenye maisha yako.
Ni malengo gani makubwa ambayo upo tayari kuyapambania kwa maisha yako yote mpaka uyafikie.

Kisha kwa pamoja tutashirikiana kwa karibu, mimi nikuwezeshe wewe kufikia malengo yako, ili na mimi niweze kuyafikia malengo yangu.

Hivyo basi rafiki, hapa kuna ngazi 5 za wewe kuweza kushirikiana na mimi kwenye hii safari ya mafanikio makubwa.
Zijua ngazi hizi tano, kisha chukua hatua mara moja kwenye ile ngazi ambayo inakufaa.

Nimeyatoa maisha yangu kuhakikisha nayafikia malengo yangu makubwa.
Na hivyo pia nimeyatoa kuhakikisha wewe unayafikia malengo yako makubwa.

Karibu tushirikiane rafiki, haya mafanikio makubwa ni ya uhakika kwetu.

Kuzijua ngazi tano za kushirikiana na mimi kwenye safari ya mafanikio, angalia video hii; https://youtu.be/aew1aQ5yVuc

Niko hapa kwa ajili yako rafiki yangu, nakusubiri uje tuambatane pamoja kwenye hii safari ya mafanikio makubwa.

Usichelewe, chukua hatua sasa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr Makirita Amani
http://www.amkaconsultants.co.tz