3247; Kama ungeanza upya.
Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya vikwazo vinavyowazuia watu kufanikiwa ni mwili na roho kutokuwa sehemu moja.
Unakuta kile ambacho mtu anafanya na kile ambacho angependa kufanya ni tofauti kabisa.
Mtu anakuwa anafanya kitu ambacho kama angekuwa anaanza upya kufanya, asingekifanya.
Kinachomfanya aendelee kuwa kwenye kitu hicho ni kwa sababu ameshazoea na anaona hawezi kwenda kuanza kitu kingine upya.
Muda unaonekana kuwa kikwazo kikubwa kwake.
Kuna mambo mawili ya ukweli ambayo wengi wanayaruka kwenye hili.
Moja ni huwezi kupata mafanikio makubwa kwenye kitu ambacho hujajitoa kweli kweli kwenye kukifanya.
Kama unafanya kitu ambacho mwili wako na roho yako havipo pamoja, unapoteza muda na nguvu zako.
Kama unafanya kitu hiki, lakini fikra zako zipo kwenye kitu kingine, unajikwamisha.
Mbili ni unaweza kuanza upya wakati wowote na ukazalisha matokeo bora, pale unapojitoa kweli kweli katika kukifanya kitu.
Haijalishi umechelewa kiasi gani, pale unapoamua kubadilika na kupeleka juhudi zako zote kwenye mabadiliko hayo, yanakuwa na tija kubwa.
Hivyo basi rafiki, kama leo hii ungepewa fursa ya kuanza upya usingeanza kufanya kile unachofanya sasa, jua upo kwenye njia ambayo siyo sahihi.
Kama kwa kila taswira ya mafanikio unayojijengea hujioni ukiwa unafanya hicho unachofanya sasa, unapoteza muda wako.
Unapaswa kuwa pale ambapo kama ungekuwa unaanza upya leo, ungeanza kufanya kitu hicho hicho na usingehangaika na kingine chochote.
Ni pale unapopata kitu ambacho roho yako inakikubali kweli na ukakifanya kwa ukubwa na kwa muda mrefu ndiyo unakuwa na uhakika wa kutengeneza mafanikio makubwa.
Kwa dhana hii, tunaweza kuyaelezea mafanikio makubwa kuwa ni kufanya kitu kimoja kwa ukubwa na kwa muda mrefu, huku ukikipa kitu hicho kila ulichonacho.
Hapo ndipo mafanikio yako makubwa yalipo, ukiweza kupang’amua, utafanya makubwa sana.
Swali muhimu sana kwako kujiuliza kila siku ni kama ungekuwa unaanza upya leo, je ungeanza tena kufanya kile unachofanya sasa?
Kama jibu ni ndiyo basi endelea kukifanya kwa ukubwa na kwa msimamo.
Na kama jibu ni hapana kwa muda mrefu, yaani kila unapojiuliza swali hilo jibu linakuwa ni hapana, unahitaji kufanya mabadiliko.
Kwenye maisha, mabadiliko huwa hayana kuchelewa, bali yanakuwa na wakati sahihi wa kuyafanyia kazi.
Unapofika wakati wa mabadiliko, utambue na kuufanyia kazi.
Hivyo ndivyo unavyoweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya.
Swali muhimu sana kwako kujiuliza kila siku ni kama ungekuwa unaanza upya leo, je ungeanza tena kufanya kile unachofanya sasa?
Kama jibu ni ndiyo basi endelea kukifanya kwa ukubwa na kwa msimamo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Jibu ni ndio, nitaendelea kufanya kama ninavyofanya sasa.
LikeLike
Safi, fanya mpaka kifo.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza kuwa haijalishi nimechelewa kwa kiasi gani, pale Nitakapoamua kubadilika na kupeleka juhudi zangu zote kwenye mabadiliko hayo, ndiyo nitakuwa na tija.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Fanya kile unachokipenda Kwa ukubwa na kwa muda mferfu mafanikio yatakuwa Yako
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Roho na mwili vimeungana ili kufanikisha kile nakifanya Sasa, hata Kama nikuanza upya nitafanya hikihiki ninachofanya.
Shukrani kocha.
LikeLike
Safi sana, fanya kwa ukubwa.
LikeLike
Asante sana Kocha ni kufanya kwa ukubwa na kwa muda mrefu,hii inatosha sana kunifikisha kwenye mafanikio makubwa. ✍️
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Swali muhimu sana kwako kujiuliza kila siku ni kama ungekuwa unaanza upya leo, je ungeanza tena kufanya kile unachofanya sasa?
Ndiyo
LikeLike
Safi sana, fanya kwa ukubwa mpaka kifo.
LikeLike
Moja ya vikwazo vinavyowazuia watu kufanikiwa ni mwili na roho kutokuwa sehemu.
Kama ningekuwa naanza leo ningeanza kufanya biashara na kuwekeza.
LikeLike
Safi sana, kaa humo.
LikeLike
Hakuna kuchelewa bali wakati sahihi wa mabadiliko nitaufanyia kazi Asante Kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kama nikianza upya Leo nitaendelea kufanya kile ambacho nimekuwa nafanya.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike