3269; Usiwajengee kushindwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi waliopo kwenye biashara hawapati ule uhuru ambao walitegemea kuupata wakiingia kwenye biashara.
Na hiyo ni kwa sababu biashara zinakuwa zinawategemea kwa kila kitu.
Biashara zinakuwa zinawategemea wao kwa kila kitu kwa sababu wanakuwa hawana timu.
Au hata kama wana timu, inakuwa siyo timu inayoweza kuendesha biashara vizuri.
Ambao hawana timu kabisa inaeleweka wazi kwa nini wanakosa uhuru, wao ndiyo wanakuwa watendaji wakuu.
Ni ambao tayari wana timu ndiyo wanashindwa kuelewa kwa nini licha ya kuwa na watu bado biashara zinawategemea.
Na sababu kuu imekuwa ni wanakuwa wamezijengea timu zao kushindwa.
Wanakuwa wameajiri watu, lakini wamewaweka kwenye mazingira ambayo hawawezi kutekeleza majukumu yao bila kumtegemea mmiliki wa biashara moja kwa moja.
Hilo la kuwajengea timu kushindwa linasababishwa na mambo matatu.
Moja ni kuajiri watu ambao wana uwezo wa chini sana kiasi kwamba hawajiwezi kabisa kwenye kufanya maamuzi bora ya biashara. Watu wenye uwezo wa chini hata wafanyweje, bado tu watashindwa.
Mbili ni kuajiri watu wenye uwezo wa kawaida lakini hawapewi mafunzo na miongozo sahihi ya jinsi ya kutekeleza majukumu yao. Hivyo hao wanakuwa wanajiendea tu kwa kubahatisha, kitu ambacho kinawapelekea kushindwa.
Tatu ni kuajiri watu wenye uwezo mkubwa lakini kukosekana kwa mfumo mzuri wa kuwazuia wasilete madhara kwenye biashara. Biashara inakuwa na mianya ambayo watu hao wenye uwezo wanaweza kuitumia kujinufaisha. Tamaa inawaingia, wanatumia mianya hiyo na hilo linawapelekea kushindwa.
Ukiangalia yote matatu, unaona wazi kabisa ni mmiliki wa biashara ndiye anakuwa amewaandaa watu wake kushindwa.
Lakini wanaposhindwa, anakuwa wa kwanza kulaumu kwamba hakuna watu wazuri.
Ni kweli kuna changamoto ya kupata watu wazuri, lakini changamoto kubwa zaidi ni wamiliki wa biashara kuwaandaa kushindwa wale ambao wangeweza kuwa wazuri na kuisaidia biashara.
Kuhakikisha unajenga biashara yenye mafanikio na inayokupa uhuru unaotaka, geuza hayo matatu yanayopelekea timu kushindwa ili ipate ushindi.
Moja ni ajiri watu ambao tayari wana uwezo mkubwa. Hawa itakuhitaji uweke kazi na muda kuwapata. Lakini pia utalazimika kuwalipa zaidi. Vizuri havipatikani kwa urahisi.
Mbili ni wape mafunzo endelevu ya kuzidi kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao vizuri. Mafunzo endelevu yanawafanya watu kuendelea kuwa bora.
Tatu ni weka mfumo mzuri wa kuiendesha biashara yako kiasi kwamba unaziba mianya yote ya watu kujinufaisha binafsi na kuidhuru biashara.
Mambo hayo matatu yatakupa kazi ya ziada ya kufanya, lakini matokeo yake yanakuwa na manufaa ya kukuweka wewe huru.
Kupata uhuru kwenye biashara kuna gharama ya kulipa.
Huwezi kutegemea kujenga biashara inayokupa uhuru mkubwa kwa kuiendesha kwa mazoea.
Kama umekuwa unafanya makosa tuliyojifunza hapa, anza kuyarekebisha sasa ili uweze kujenga biashara bora ya kuijengea timu ushindi ili pia biashara ipate ushindi na kukupa wewe mafanikio na uhuru.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kupata uhuru kwenye biashara kuna gharama ya kulipa.
Huwezi kutegemea kujenga biashara inayokupa uhuru mkubwa kwa kuiendesha kwa mazoea.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kupata watu wenye uwezo inahitaji kazi,muda na malipo mazuri.
🙏🙏🙏
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ajiri wenye uwezo walipe vizuri,waendelee na weka mfumo wa biashara simamia vizuri
Asante
LikeLike
Mkakati ndiyo huo.
LikeLike
Ili kupata uhuru kwenye biashara:-
1. Ajiri watu wenye uwezo mkubwa
2. Wape mafunzo endelevu
3. Weka mfumo mzuri wa kuiendesha biashara yako kiasi kwamba unaziba mianya yote ya watu kujinufaisha binafsi na kuidhuru biashara.
LikeLike
Tukae humom
LikeLike
Napambana kutoa mafunzo endelevu kwa watu Bora na sahihi huku nikijenga mfumo bora utakaozuia mianya yote ya uharibifu na upotevu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kupata uhuru kwenye biashara kuna gharama ya kulipa.gharama zenyewe ni kuajiri watu wenye uwezo mkubwa,wape mafunzo endelevu na weka mfumo imara. Asante Kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakika tunahitaji kujenga timu bora na inayopata mafunzo endelevu.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli mafunzo yanasaidia huku ikishirikiana na mfumo wa biashara hiyo na pia kiwaelekeza wafanye wenyewe
LikeLike
Ndiyo
LikeLike