💯KCM2324044; Wajibu.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumanneYaKujikubali

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Chagua vitabu ambavyo huna kisha piga 0678 977 007 kuvipata.



💯 Neno la leo; Wajibu.

Leo ikiwa ni #JumanneYaKujikubali tunaona jinsi ambavyo unao wajibu wa kuwa wewe ili kufanikiwa.

Kwenye maisha, siyo tu mtu una haki ya kuwa wewe, bali pia unakuwa ni wajibu wako.
Kila mtu anao wajibu wa kuwa halisi kwake yeye mwenyewe ili aweze kujiamini na kujikubali.

Watu wengi sana hawajiamini na kujikubali kwa sababu hawauishi uhalisia wao. Kila wanachofanya wanakuwa wameiga kwa wengine na kufuata mkumbo. Hilo linawafanya waendelee kufuata mkumbo kwa sababu wanakuwa hawana wanachosimamia wao wenyewe.

Unapojiamini na kujikubali kwa kuchagua kuyaishi maisha yako kwa uhalisia wake, wengi wanaokuzunguka hawatakubaliana na hilo.
Watataka waendelee kukuona kama walivyozoea.
Usipokuwa na mahali imara pa kusimama, utaangushwa haraka sana.

Unachotakiwa kujua ni kwamba ni haki na wajibu wako kuwa halisi kwako mwenyewe. Hupaswi kusikiliza wengine ni nini wanachotaka kwako, bali anza kwa kujisikiliza wewe mwenyewe ni nini unachotaka.

Wanaokuzunguka wanataka uendelee kuwa vile walivyokuzoea ili wajisikie vizuri na hata kukutumia kupata kile wanachotaka. Huwezi kuendelea na hali hiyo kama unataka kufanya makubwa.

Kutokujiamini na kukosa kujikubali imekuwa ni breki inayowazuia wengi kuishi uhalisia wao na kufanya makubwa.
Watu wanakutana na changamoto na hata kukabiliana na ushindani mkali kwa sababu hawajaweza kuwa halisia kwao wenyewe.

Hakikisha unakuwa wewe halisi, hiyo ni haki na wajibu wako kama unataka kufanya makubwa zaidi ya hapo ulipo sasa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu adui yako mkuu. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/12/3268

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuwa wewe halisi ili uweze kufanya makubwa na kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.

Kocha.
💯